Live Updates: Simba Sc-Wenye nchi tunaiweka nchi mbele

Nchi ina wizara na wizara Ina bajeti yake... Watoe bajeti watangaziwe hakuna kitu Cha bure hapa Duniani. Zama za kijinga zibaki kwq Simba sio kwa yanga.
 
Usikariri Mambo.
 
Timu ya wananchi itabaki kuwa moja tu
 
Japokuwa Simba damu, ila huyu vunjabei mkataba wake ukiisha, please hii zabuni apewe mtu mwengine angalau tupate taste mpya, mwamba anapwaya sana, ubunifu mdogo yani kinyonge sana ..
Mmechoka kuvaa madekio eeeh[emoji23][emoji23]
 
Yanga wamezindua jezi, tumeona mashati tu yaliyovaliwa na mamodel wa mchongo wakati jezi iwe imekamilika ni shati, bukta na soksi. Yanga hawana umakini katika mambo yao.
Daah.. mkuu mbona toka mwanzo we unahangaika na Yanga wakati humu tunazungumzia uzinduzi jezi ya Simba? jitofautishe basi na wale mbu3 aliowasema mwenyekiti wetu Aden rage
 
Kwahiyo pasipo kuwepo kwa neno Tanzania, hayo uliyoyataja yasingefanikiwa?
 
Nchi ina wizara na wizara Ina bajeti yake... Watoe bajeti watangaziwe hakuna kitu Cha bure hapa Duniani. Zama za kijinga zibaki kwq Simba sio kwa yanga.
Kwenye masuala ya branding, kila unachofanya lazima kishabihiane, mambo yako yakikinzana unafeli. Hauwezi kujiita "classic restaurant" halafu mteja akija anakuta sehemu yako imejaa inzi.

Kujiita timu ya wananchi kunaendana na matendo na si maneno tu.

Pia Yanga hana historia nzuri kumzidi Simba kwenye masuala ya kuijua pesa. Simba aliachana na SportPesa baada ya SP kutaka kuipa udhamini Simba unaofanana na wa Yanga wakati thamani ya timu hizi mbili haikuwa sawa.
 
Zungumzieni tukio la Simba. Mbona uzi unaanza kutawaliwa na habari za YANGA?
Ilo ndio limenishangaza badala ya kujadili tukio lillilopo wanaenda kutoa taarifa za tukio la Yanga.
 
Aisee umewezaje kuni quote wakati kichwani ni empty set[emoji848][emoji848][emoji23][emoji23]
 
Yanga inajua karaha ya kutembeza bakuli kwahiyo haitaki kurudi huko tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…