Denis samwel
Member
- Aug 15, 2016
- 52
- 15
- Thread starter
- #81
Itatuchukua miaka mingi sana kama taifa kupiga hatua. Watanzania ni wepesi wa kukosoa lakini hawapendi kukosolewa hata kidogo.
Unapowasilisha hoja kwa lugha isiyokuwa yako, sio dhambi kukosea. Hata kiswahili chanyewe tunakosea sana sema tu kwakuwa tunachukulia poa.
Hata hivyo tatizo ni pale unapoambiwa kuwa lugha uliyotumia hukuitendea haki halafu unakuwa mkali. Badala ya kuichukulia hiyo kama changamoto unageuza mjadala unakuwa wa matusi. Hii sio sawa na haitakusaidia.
Tuelezane ukweli pale inapobidi. Tujifunze kuwa na majibu ya staha, na tuache kudhani kuwa hatukosei. Ukifuatilia mjadala utagundua kuwa umehamia kwenye matusi tu na sio kwenye ushauri wa kutatua hoja iliyokuwa mezani.
Ukweli ni kuwa mleta mada amekosea sana kwa namna anaojibu hoja.
Ushauri wangu:
Mleta mada, maisha hayahitaji mashindano na hupotezi chochote kwa kujishusha. Kuwa muungwana, waombe radhi ulowakwaza kisha walio kukwaza naamini nao watakuomba radhi kwakuwa wengi walifanya kama ku "retaliate " tu na sio vinginevyo.
Kumbuku, hii ni JF kuna siku uzI huu unaweza kuja kuwa kikwazo kikubwa sana hapo baadae kwenye harakati zako.
Kila la kheri kwako mkuu.
Asante kwa maneno yako ya Busara na yasiyo na Matuc ila Naomba nami nikukumbushe kitu Kukosolewa sio dhambi ila Dhambi ni Kutukanwa ama lugha za Matuc juu ya Mwandishi.
Mtu anapokosolewa inamsaidia kujua kile alichokikosea Ila Anapotukanwa Ina msaidia nini