Low IQ Tanzania, wanafurahia Polisi kuondolewa barabarani!

Mpumbavu wewe, ajali za mijini ni ngapi.
Au nawe unakurupuka na kuja kuleta hoja za kijinga hapa.
Kinana kasema ma trafiki waondolewe mijini
taifa lina watu makalio sana,wewe unazijua takwimu za ajali mji wote huu kwa siku???

au ajali kwako ni mtu kukosea tundu nyuma huko???
 

Pita kule koplo
Tafuta income nyingine
 
Ila ukweli utabaki palepale hao jamaa ni wala rushwa sana barabarani kuliko kusimamia vyombo vya moto...
Wapunguzwe tu..
 
Ila ukweli utabaki palepale hao jamaa ni wala rushwa sana barabarani kuliko kusimamia vyombo vya moto...
Wapunguzwe tu..
ukiwa road una chaguo mbili,kulinda usalama wa nafsi yako na wengine au kulinda buku mbili isiondoke.

sababu ya ujinga vichwani mwa wengi,buku mbili mbili ndio zinawapeleka orgasm kwenye kauli ya kinana.
 
Kuweka kamera kila mahali ni gharama na hawawezi kumudu na ndiyo maana badala yake Polisi wanakaa barabarani, nchi nyingine hauoni Polisi kwa maana wana teknolojia lkn hata hizo nchi kabla ya kutajirika ziliweka polisi barabarani pia!
msitetee vitu kama hivi hamna uzoefu navyo, gharama za camera zinazidi yale ma v8 na 1HZ za makatibu wa mikoa wa CCM?

Hapa Uganda sehemu nyingi sana wamefunga camera na hakuna kabisa usumbufu wa askari barabarani na hata matukio ya ajali. hakuna kaa kwetu.

Ukitaka kujua kuwa askari wetu wamezidi usumbufu ingia barabarani na magari tofauti tofauti halafu uone kama haya yanayosemwa ni uongo ama kweli.

Binafsi nimetumia vyombo vingi vya usafiri kwenye majukumu yangu hivyo najua adha iliyopo kuna magari nikitumia huwa sisimamishwi wala kusogelewa na askari zaidi atakuita upite haraka na kuna gari nikitumia askari akiiona tu udenda unamtoka.

Ni muda wa kuwa na sheria kali kwa madereva wazembe na wavunja sheria makusudi na ni muda wa kuweka camera kuepukana na kero ya askari hao cha msingi mifumo iwe active muda wote.
 
Wingi wa TARURA Mabarabarani pia imekuwa ni kero ya ajabu, ukipaki kwa ajili ya dharura labda unabadilisha gurudumu wanakuja na kukupiga faini.
 
Hapo umenena. Nchi zetu hizi watu hatujastaarabika sana, kwa hiyo bado tunahitaji usimamizi wa karibu sana.

Sasa anatokea mlevi mmoja tu eti Police wamejazana mno Barabarani, watu wanashangilia.
Ni shida kweli kweli.
Mbona JPM hakupendwa na wapigaji? Ni kweli watanzania bado sana kuwa na kiongozi anayewarumbulia macho. Anatakiwa chuma kwelikweli.
 
Kinana hakusema anataka waondolewe wote hapana,nikwamba wapunguzwe kuna haja gani safari yako ya km 4 iwe na vituo vinne vya askari na wote na wote wanakusimamisha?na mimi naongezea hapo je,kuna tafiti gani walifanyaga ikawaonyesha pick up,fuso,canter hiace ndio gari zisizo ruhusiwa kupita bila kupigwa mkono?
 
Kimara hadi Ubungo kuna vituo vitatu vya askari wa barabarani...

Kazi yao kukusanya mpunga tu
stop over,bucha na ubungo maji, ukikunja kulia unawakuta river side,external,mwananchi,tabata njia panda ya segerea,buguruni_tazara,sokota,taifa na uhasibu. imagine hapo sio kilomita hamsini tazama uwingi wao.

Si kwamba askari wasiwepi bali wapunguzwe na wawe wanaingia pale inapotokea brake down au ile mida ya peak.
 
Wewe ndio low IQ Kinana ameshauri wapunguzwe sio waondolewe,kama suala la ulevi Traffic wamchek dereva kabla hajatoka stand. Pamoja na huo wingi wa traffic Kila Siku wapo mbona ajali Bado zipo
 
Ni kweli kabisa... Tatizo sio kuwa na askari wengi barabarani bali tatizo ni vizuizi barabarani... Hata ukipunguza askari barabarani vizuizi vikabaki vile vile tatizo lipo pale pale tena wakiwa wachache ndo rahisi zaidi kuchukua rushwa
 
Kukomesha ushenzi wote kutoka pande zote zinazosimamia matumizi ya barabara ni muhimu tufuate ushauri wa DCP mmoja aliyewahi kushauri ufungwaji na matumizi ya Camera ambapo alisema hiyo pia itakuwa ni muarobaini kwa bodaboda lakini bahati mbaya ushauri wake ulitupwa na yeye akang'olewa pale juu ..Binafsi sioni kama uwingi wa Traffic ni tatizo bali tumelemaa mno na traditional tactics badala ya kwenda kidigitali
 
Kwanza si kweli kuwa uwingi wa trafiki barabarani ndio njia pekee ya kupunguza ajali..zipo njia nyingi sana, lkn la kwanza ni kujua vyanzo vya ajali ni nini..barabara nyembamba, magari ya mizigo ni mengi, mwendo kasi, ulevi madereva nk njia rahisi ni kama zifuatazo..
1. Uwepo utaratibu wa kusimamisha malori kila inapofika saa 12 asubuhi hadi saa 4 na kila inapofika saa 10 jioni hadi saa 4 usiku ili magari ya abiria na magari madogo yatumie muda huo kufika wanakokwenda bila lazima ya kuovertake kila mara..
2. Adhabu kali kwa madereva wazembe, hasa walevi, ikiwemo kifungo na kufutiwa leseni kabisa.
3. Trafiki wapunguzwe barabarani, na kuwepo utaratibu wa ukaguzi, wenye kukagua magari ya abiria wawepo kwa umbali maalum, magari madogo pia, na wenye kukagua malori nao pia na waweke vibao kabisa kuonyesha hii ni roadblock ya malori, au magari madogo ili wengine wasisimame sababu haiwahusu wasimame pale panapostahili tu kukaguliwa..jambo lolote linapokosa utaratibu linasababisha fujo, rushwa, uhalifu nk na wakati mwingine polisi hawataki uwepo utaratibu sababu utaziba mianya ya wao kupata wanachopata ndio maana wanatetea hali ya kutokuwepo order ya wao kupunguzwa barabarani.
 
Kwa dar waweke kamera. Lkn swali hivi katikati ya miji yetu kunakuaga na ajali sana. Make ajali nyingi hutokea nje ya mji ambapo magar hua yanakimbia sana.

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…