Mara . Waziri Mkuu wa
zamani, Edward Lowassa jana
alisema kuwa muda wa
mabadiliko aliyotabiri Baba
wa Taifa, Mwalimu Nyerere ni
sasa na kwamba yeye ndiye
anayeweza kuyaongoza.
Wakati Lowassa akisema
hayo mjini Iringa, kada
mwingine anayewania urais
kwa kupitia chama hicho,
William Ngeleja alikuwa
mkoani Mwanza ambako
alisema kuwa ana dhamira ya
dhati na nia ya kuleta
mabadiliko kwa maisha ya
Watanzania.
Mjini Iringa, Lowassa alisema
kuwa kwa sasa CCM inahitaji
mabadiliko makubwa na
akanukuu kauli ya Mwalimu
Nyerere aliyoitoa mwaka
1995 alipozungumzia haja ya
chama hicho kujisahihisha.
Baba wa Taifa alisema kuwa
Watanzania wanahitaji
mabadiliko na wasipoyapata
ndani ya CCM watayatafuta
nje ya CCM, alisema mbunge
huyo wa Monduli kwenye
hafla hiyo iliyofanyika Uwanja
wa Samora mjini Iringa.
Huu ni wakati wa
mabadiliko. CCM ikijipanga
inaweza kuleta mabadiliko na
mtu wa kuleta mabadiliko
hayo ni mimi, alisema.
Lowassa alisema aliamua
kuingia kwenye mbio za urais
kwa sababu tatu, ambazo ni
kufanya mabadiliko ndani ya
CCM, kufanyia kazi tatizo la
umaskini na kushughulikia
tatizo la ajira kwa vijana.
Kwa mujibu wa katibu wa
CCM wa Wilaya ya Iringa Mjini,
Zongo Lobe Zongo, jumla ya
wanachama 58,562 kutoka
wilaya zote walijitokeza
kumdhamini.
Mjini Mwanza, Ngeleja alipata
wadhamini 1,253 na
kusisitiza hajatumwa na mtu
kugombea urais na wala
hana kundi.
Naomba ifahamike kwamba
mimi kugombea kwangu
urais sijatumwa na mtu, wala
sipo kwenye kundi la mtu
yoyote. Naona natosha na
uwezo huo ninao kama
Mungu atanijalia kupata
nafasi hiyo nitadhihirisha kwa
vitendo, alisema Ngeleja.
Mambo niliyoyafanya nikiwa
msaidizi wa Rais Kikwete
yanatosha kuonyesha wazi
kwamba nina uwezo wa
kuboresha mambo
mbalimbali na kukuza
uchumi wetu, alisema
ambaye alikuwa Waziri wa
Nishati na Madini.
Ngeleja alirudia kutaja
vipaumbele vyake kuwa ni
kudumisha amani na
utengamano wa kitaifa,
kupiga vita ufisadi, rushwa na
mmomonyoko wa maadili,
kuboresha sekta za kilimo,
uvuvi, ufugaji, viwanda,
miundombinu na elimu.
Mkoani Mara, Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, Bernard
Membe amesema ni
wanaume wachache wa
kuigwa kama Makongoro
Nyerere wenye uthubutu wa
kusema ukweli kwa uwazi na
kwa kujiamini kuhusu
mambo yanayoendelea ndani ya CCM.
source: mwananchi