Ludovick Utouh: Tusijikombe sana, fedha ni za Umma sio za Rais

Kichaa katoka mafichoni.

Kwanza kwa mtu anayejitambua, kusifiwa na kichaa au punguani, inakuwa ni kama balaa. Ni sawa mtu utoke nje, uone fisi wanatikisa mikia kukufurahia.

Pongezi yenye thamani ni ile unayopewa na mtu mwenye akili timamu na kwa jambo halisia. Hivi usifiwe na Mwashambwa unaweza hata kutoka mbele ya watu na kusema kuna watu wamenipongeza?
 
Napenda Msimamo wako!!
 
Mimi sikubaliani nawe.
Huwezi kuilinganisha CCM ya leo na CCM ya miaka iliyopita na kutoa lawama zilezile. Laumu CCM hii ya leo iliyotoka kwenye kuwa chama cha wafanyakazi na wakulima na kuwa chama malaya, yeyote anatumia anavyotaka mwenyewe.
 
Hii tabia haiwezi kukoma mpaka mhusika akatae mwenyewe, kama ilivyokuwa kwa Rais mkapa na vyombo vya habari, katika usomaji wa taarifa ya habari huwa kuna mpangilio wa habari ya 1, 2, 3, nk kulingana na umuhimu wake na vyombo vya habari vilizoe kila taarifa ya habari inayomhusu rais ilikuwa inawekwa namba 1, Mkapa akasema hii sio sawa, iwe ni ya kwanza kama ina sifa hizo, toka hapo wakaacha kufanya hivyo.Rais Mwinyi alipoingia madarakani alikuwa akiitwa Mtukufu rais baadae akakataa akasema yeye ni mheshimiwa kama viongozi wengine, tangia hapo MTUKUFU halitumiki tena Tanzania.
 
Kila siku Mr Tundu Nguli anatufunza kwamba bili yoyote yaani mada yoyote y hela ya umma lazima ipitishwe na Rais. Kwa vile Rais kaipitisha na kweli tumepata madawati Tandahimba, kwa nini tusimshukuru? Si angeweza kukataa? Asiyeshukuru ni kafiri.
 
Kina Mwasha mbwa jawawezi kuelewa
 
Wewe ni kunguni kabisa wa kitanda cha mama
 
Hii tabia tunayoisikia ya tunamshukuru sana Mhe. Rais na hata kupiga magoti, this is not right (hii si sawa) kwa kuwa hatuwezi kumshukuru Rais.

Kwa kuwa Tanzania tuna culture (utamaduni) ya shukrani basi tuishukuru Serikali na tusimshukuru mtu kwa kuwa hizi fedha na rasilimali ni fedha zetu sisi wananchi, sio matumizi yake ni matumizi ya fedha zetu wananchi na hivyo hatuwajibiki kumshukuru an individual (mtu).

Na siku hizi tumeanzisha tabia ya kujikomba na kujipendekeza nafikiri haitusaidii sana kwa kuwa haitupeleki mbele inaturudisha nyuma.

Pale kwenye ukweli tuseme ukweli, tusiwe wachochezi wala tusiweke chumvi kwenye yale tunayoyazungumzia.

Kama fact tuseme tu na tusiogope kusema"
 
Chawa wa mama wanakuja
 
Chawa wa mama wanakuja
 
ChoiceVariable, Lucas mwashambwa, na chawa wa mama mada kama hii mkiiona huwa mnaipita kimya kimya.

Ni wakati wenu huu sasa wa kuurejesha ubongo mahali pake sahihi (kichwani), kutoka huko kwenye matumbo yenu yaliyojaa minyoo ya kila aina.
Huyo kama anaona wivu kwa mamilioni ya watanzania kumpongeza mh Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania kwa kazi nzuri anayoifanya na iliyoleta tabasamu na matumaini katika mioyo ya watanzania basi na yeye aende akagombee Urais aone kitakacho mkuta.

Kwa hiyo anataka tusimpongeze Rais wetu? Anataka tumkatishe tamaa mh Rais? Kwani hajuwi mamlaka ya Rais katika utokaji wa mabilioni ya fedha kwenda katika miradi au huduma za kijamii? Hajaona mahali unakuta kuna mradi unasuasua kwa kukosa pesa lakini Rais akifika na kutoa amri na kuelekeza pesa zipelekwe mahali hapo zinatoka haraka sana na mradi kuendelea kujengwa na kukamilishwa? Sasa kwanini tusimpongeze mh Rais?
 
Kuna tofauti kati ya kumpongeza na kujikomba komba, mambo mengine unayoyaeleza hata hayawai kufanyika sasa sijui kwa uhalisia huo ni kumpongeza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…