Ludovick Utouh: Tusijikombe sana, fedha ni za Umma sio za Rais

Upo sahihi Mkuu, Uchawa ndio sababu ya haya kutokea.

NAAMINI HATA RAIS HUWA ANACHUKIA JINSI TUNAVYOMTUKUZA KUPITA KIASI.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Ukiona hata Waziri Mkuu akimshukuru Rais Dr Samia kwa kufadhili mradi fulani, basi unajieliza treni la siasa za chama zilitoka vipi kwenye reli.
 

Ungempa na Hadhi yake ni profesor Utoh
 
Hii nchi imelaaniwa
Na mambo yanaendelea kuwa mabaya zaidi, nchi inaendelea kupoteza kile kizazi cha watu makini, watu walioweza kusimama na kusema kama haya aliyosema CAG mstaafu.

Na hii anayosema CAG inatokana na wateule wengi wa Rais kutokujiamini na unafiki mwingi. Viongozi wengi wamepata vyeo kwa connection na kujikombakomba kwa mamlaka za juu, hii inapelekea waamini bila kumsifia sifia Rais inaweza kupelekea kupoteza nafasi zao.

Ukipata kazi kutokana na elimu na ubora wako kiutendaji, huwezi kuwa chawa maana unajiamini. Viongozi wanaojikombakomba kwako sijui wanaweza kukushauri kitu gani.

Tuliona jinsi walivyojifanya wanaunga mkono msimamo wa Magufuli wa kukataa chanjo na barakoa enzi ya Covid19, alipoondoka wakaanza kukimbilia barakoa na chanjo. Kuzungukwa na watu wanaojikomba sana kwako sio jambo jema, utaangamia.

Tunatengeneza taifa la machawa na hii itatugharimu zaidi huko mbeleni. Ukiona mteule wako anakusifia sifia sana ujue hatimizi wajibu wake kama inavyotakiwa na anatumia sifa nyepesi kukupumbaza.
 
Huyu nae mnafiki tu...mbona hakusema hayo kipindi cha mwendazake?
Maana hii misemo ilianza kipindi cha jiwe..

Wasomi wetu mirija ikianza kikata ndo wanajifanya great thinker...
Better late than Never
 
Huyo anaekubali kusifiwa kwa vitu ambavyo sio vyake ndio tatizo
Angekemea kwq nguvu tena kuwakataza pindi wanapobinua midomo yao basi wangeacha
Sipendi mtu aniite tajiri au majina ya kinafiki
Kwanini akubali sifa ambazo ni za Mungu tu
 
Tatizo la watanzania kwa zaidi ya miaka 60 tumezidi kuwa maskini wa Mali na akili na maskini wenyewe ndio watakaokupinga.Wanajiita chawa. kwao ni ufahari
 
Hiyo yote ni pale mfumo wa uongozi wa taifa unakua corrupted ,hivyo kukosa watu wenye uweledi katika ngazi mbalimbali za uongozi hivyo kupelekea kuwepo kwa viongozi machawa na wanafiki.Rais hana biashara inayompatia fedha za kuendesha taifa hadi apewe shukrani personal na wote wanaofanya hivo ni kudharau jasho la wananchi.
 
Ameamza kulifahamu jambo hilo lini jana? Ndio, leo ndio anasema!?
 
Ngoja VYAWA wakusikie🙁
 

Chawa mkuu in da house [emoji23]
 
These are the brains we need
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…