Unanikosea heshima sana mkuu 'Allency', juu ya hili; kwani nakufahamu siku zote kuwa tofauti na ulivyonielewa kwenye mada hii.
Utaanzia wapi kunifananisha na Bashite, kwa mfano! Kwa vile tu namwona Luhaga Mpina kuwa tofauti ndani ya CCM sasa hivi?
Rudi nyuma uangalie ni mara ngapi umekubaliana nami humu humu JF kwa kukubali nilichochangia kwenye mada mbalimbali, halafu leo kwa sababu ya Luhaga niwe kama Bashite?
Nasema hivi, mkuu wangu 'Allency', inapohusu ilipotufikisha CCM hii, nipo tayari kukubali lebo yoyote ili mradi nisiwe sehemu ya chama hiki kinachotudidimiza sote.