Luhaga Mpina: Kuundwe Tume ya kuchunguza 'Utata' wa kifo cha Hayati Magufuli

Luhaga Mpina: Kuundwe Tume ya kuchunguza 'Utata' wa kifo cha Hayati Magufuli

Rekodi gani? Anachopigania ni uwaziri, nimeshasema humu nasubiri siku atakayoteuliwa ndio mtaona atakavyokana kauli zake zote!!

Ni mnafiki tu huyo Mpina hana tofauti na majizi mengine yaliyojazana CCM.
Hapana.
Mimi simwangalii Mpina kama unavyomwona wewe. Mpina alishawahi kuwa waziri, rekodi yake ya wakati huo ipo, hata kama wewe utaiona ina madoadoa. Kama alifanya 'wizi' kama unavyodai hapa, eleza matukio kwa ushahidi ulio nao wewe.
Mpina sasa hivi anafanya kazi kubwa ya upinzani kuliko vyama vyote vya upinzani, ikiwemo CHADEMA yenyewe tuliyo tegemea ingefanya kazi hiyo.
Sasa wewe hapa unakuja na madai ambayo hayana ushahidi wowote, halafu unataka tukuamini wewe, ambaye umejibainisha humu humu kuwa na maslahi na CCM hii hii inayotawala sasa?
 
Jamaa huwa anatokea kuziba, kufifisha hoja.
Kwani hata ikiwa kweli kuna shida gani? yeye si ndo mwanzilishi wa mauaji?
Basi si ndio tujue kama kina Ben Saanane, Mbowe, ama Tundu Lissu walihusika?

Hatahivyo Hayat Rais Magufuli hajaanzisha mauaji katika Dunia hii.
=======
Halikadhalika kama kina Ben wamekufa shida ipo wapi? Tundu Lissu kupigwa Risasi shida ipo wapi?

Nye nye nye
 
Iundwe kamati huru kuchunguza kupotea kwa Ben Saanane na Azory Gwanda .
Kwani wakipotea kuna shida gani?
Kifo cha Leopold Lwajabe.

Shambulio la Tundu Lissu Dodoma.

Kutekwa kwa Roma Mkatoliki na Mohamed Dewji.
Mo inasadikika alijiteka, kama ilivyo Mdude
Sababu za kuvamiwa Clouds Media Group studio.

Case closed
Hapa itakuwa tumeutendea haki umma wa watanzania na familia za hao watu.
Familia ya Hayati Magufuli ni ya Watanzania wote na wapenda uhuru na haki wa Afrika nzima
 
Kwani wakipotea kuna shida gani?
Mbona na wewe hujapotea??
Mo inasadikika alijiteka, kama ilivyo Mdude
Kuna mahali niliandika Mdude hapo?

Nimeandika Roma Mkatoliki na kufariki Leopold Lwajabe mbona hujajibu nilioandika.

Mo alijiteka vipi hotelini alipoenda na gari yake kwa ajili ya mazoezi , wewe unaweza kwenda gym na gari yako halafu ujiteke uiache parking ???
Case closed
Nothing is closed it just the beginning.
Nani alikudanganya??

Mbona kuna watu walisherekea kifo chake hadi wakakamtwa na rekodi zipo na tangazo likatoka watu wakazuiwa kusherekea??
Familia ya Hayati Magufuli ni ya Watanzania wote na wapenda uhuru na haki wa Afrika nzima
Mtu aliyeminya uhuru na kutaka aongee na kusikilizwa yeye pekeyake anawezaje kupendwa na wapenda uhuru?

Rejea siku anamuapisha Mwakyembe aliwaambia wanahabari wasidhani wako huku akasema " not to that extent"
 
Desert Mission.
 
Attachments

  • Screenshot_2023-09-21-21-30-01-827_com.facebook.katana.jpg
    Screenshot_2023-09-21-21-30-01-827_com.facebook.katana.jpg
    175.2 KB · Views: 5
Mbona na wewe hujapotea??
Kwani ulikuwa unanizungumzia mimi-jikite kwenye mada
Kuna mahali niliandika Mdude hapo?
Nimeandika mimi, unabisha nini?
Nimeandika Roma Mkatoliki na kufariki Leopold Lwajabe mbona hujajibu nilioandika.
Si ndio hiyo tume itachunguza-Cause and Efrect-Roma amekufa?
Mo alijiteka vipi hotelini alipoenda na gari yake kwa ajili ya mazoezi , wewe unaweza kwenda gym na gari yako halafu ujiteke uiache parking ???

Nothing is closed it just the beginning.

Nani alikudanganya??

Mbona kuna watu walisherekea kifo chake hadi wakakamtwa na rekodi zipo na tangazo likatoka watu wakazuiwa kusherekea??
Walikamatwa na nani? Kama kweli unautenga Utawala huu na wa Hayati?
Mtu aliyeminya uhuru na kutaka aongee na kusikilizwa yeye pekeyake anawezaje kupendwa na wapenda uhuru?
Huo ni Uzushi- Infwakt, ni Uwongo.
Rejea siku anamuapisha Mwakyembe aliwaambia wanahabari wasidhani wako huku akasema " not to that extent"
Kwahiyo? Hoja yako ni ipi Matrix? Kubali tu, tume iundwe utapata majibu ya maswali yako.
 
Mpina alishawahi kuwa waziri, rekodi yake ya wakati huo ipo, hata kama wewe utaiona ina madoadoa
Rekodi ipi mbona JPM alimtumbua uwaziri? Nachojua alikua anachoma nyavu za wavuvi tu kama haumpi pesa na hilo liko wazi huku kanda ya ziwa tunafahamu. Kama unabisha nenda leo kamtafute mvuvi yoyote mkubwa iwe mwanza au mara alafu muulize kuhusu hili, na hiki ndio kilimfanya JPM amtumbue. Sasa kama mnaamini JPM alikua mzalendo sijui mpinga ufisadi je alikosea kumtumbua Mpina? Yaani mzalendo amtumbue mzalendo?
Mpina sasa hivi anafanya kazi kubwa ya upinzani kuliko vyama vyote vya upinzani, ikiwemo CHADEMA yenyewe tuliyo tegemea ingefanya kazi hiyo.
Kazi ipi? Kuongea kwenye press utalinganisha na chadema wanaoenda barabarani na majukwaani? Mpina ni mitandaoni tu kwanini asifanye mkutano jangwani au hata Furahisha akaongea na wananchi? Huyu ana uchungu tu na uwaziri so anatafuta madhaifu ya serikali ili wakitumbuliwa apewe nafasi. Hii strategy alitumia Bashe na akafanikiwa.
ambaye umejibainisha humu humu kuwa na maslahi na CCM hii hii inayotawala sasa?
Maslahi yapi? Yaani kusema Biteko kafeli kuliko January ndio maslahi? Get serious. Mimi siikubali CCM lakini inapokuja suala la Sukuma Gang kutafuta political mileage nikiwapinga basi inaonekana kama nimekua CCM hivi. But huyo Mpina is useless ndio maana alikataliwa NEC na wapiga kura cha ajabu wewe ndio unajua influence yake kuliko wajumbe wa CCM mkoa?
 
M nadhani kwanza iundwe tume ichunguze kifo cha Mkapa Benjamin,tume ichunguze pia walipo kina Azory Gwanda na Ben saa 8 kisha itoe majibu kuhusu wale waliofungwa kwenye viroba.
Mwisho kabisa ituletee jibu kuhusu Jiwe aliyekuwa mgonjwa tangu akiwa chuo pale Udsm.

Tulio kuwa tunamjua tulisema kwamba hatamaliza 10 yrs
 
Rekodi ipi mbona JPM alimtumbua uwaziri? Nachojua alikua anachoma nyavu za wavuvi tu kama haumpi pesa na hilo liko wazi huku kanda ya ziwa tunafahamu. Kama unabisha nenda leo kamtafute mvuvi yoyote mkubwa iwe mwanza au mara alafu muulize kuhusu hili, na hiki ndio kilimfanya JPM amtumbue. Sasa kama mnaamini JPM alikua mzalendo sijui mpinga ufisadi je alikosea kumtumbua Mpina? Yaani mzalendo amtumbue mzalendo?
Hilo la kuchoma nyavu haramu za wavuvi linafahamika sana, nami ningekuwa kwenye nafasi hiyo ningefanya hivyo hivyo; na wavuvi wenyewe wanalijuwa. Kama walikuwa wakimpa pesa atazame pembeni, inakuwaje walalamike anapochoma hizo nyavu?
Mimi sibishi kuhusu hilo la kuchoma nyavu, kwani ninalijuwa vizuri na nililiunga mkono, na leo hii likifanyika nitaliunga mkono. Kama huelewi ninacho andika juu ya hili, au upende tu kupindisha ili uonekane ku'score' point' hilo halinipi shida hata kidogo.

Hilo la "uzalendo wa Magufuli", msimamo wangu juu yake haujifichi humu JF, kwani maandishi yangu juu yake yamejaa tele, na sibadili chochote juu ya hilo kama ushahidi upo. Nionyeshe huo ushahidi.
Mwisho, sijui sababu iliyomfanya Magufuli amtumbue Luhaga Mpina. Kama usemavyo wewe kuwa ni kwa sababu ya ufisadi aliofanya Mpina, sina la kumtetea juu ya hilo.
Ila kwa sasa hivi, anayoyazungumzia Bungeni, na ninayoyajua juu ya utumishi wake tokea huko nyuma, sina sababu ya kunifanya nisiungane naye.
 
la kuchoma nyavu haramu za wavuvi linafahamika sana,
Issue kwani ni kuchoma nyavu haramu au kudai pesa? Waliohonga mboana hawakuchomewa au kukamatwa/kufutiwa leseni? Ni sawa tu na JPM anakamata mafisadi ambao sio CCM ila yale majizi yaliyokua CCM hayakuguswa. Ndio hiki tunapinga double standards.
Kama huelewi ninacho andika juu ya hili, au upende tu kupindisha ili uonekane ku'score' point' hilo halinipi shida hata kidogo.
Napindisha nini? Mpina ni mnafiki tu, ndio maana JPM alimfuta uwaziri kwani hakujua Mpina ni mzalendo kuchoma nyavu? Why alimtumbua? Mtu alipinga uchunguzi wa Lissu ila anashadadia uchunguzi wa JPM kama sio unafiki ni nini? Kipindi CAG analeta hoja ya 1.5 T ni huyu mpina alisema CAG anatumika na mafisadi cha ajabu leo hii anatumia ripoti za CAG kumpinga Samia!!
Ila kwa sasa hivi, anayoyazungumzia Bungeni, na ninayoyajua juu ya utumishi wake tokea huko nyuma, sina sababu ya kunifanya nisiungane naye.
Utumishi gani? Yaani mtu mwenye ndimi mbili ndio unasema utumishi wake uko credible? Mimi naombea tu Mama samia amrudishie uwaziri ili unafiki wake uwe wazi kabisa. Mtashangaa atakavyokana haya yote anayosema leo.
 
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina amesema “Baada ya kusikiliza kwa kina maelezo ya Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenari Venance Mabeyo aliyoyatoa Machi 16, 2024, nimeshawishika na ninawashawishi Wabunge wenzangu kuruhusu kuunda Tume huru ya kuchunguza utata wa kifo cha Rais wa awamu ya Tano, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli ili kumtendea haki lakini na watu wengu waliotajwa ama kwa wema au kwa ubaya katika suala hili.”

Ameongeza “Pia tume hiyo itabaini hata watu waliokataa kuapishwa kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Tanzania wakati ilikuwa ni takwa la kikatiba.

Kwa mambo yaliyosemwa na Taasisi ambayo sio ya kutiliwa mashaka na mtu ambaye si wa kutiliwa mashakaa kuna haja ya hii tume kuundwa.”

View attachment 2968571

==============================​
Kisesa MP, Luhaga Mpina, has stated, "After thoroughly listening to the explanations provided by retired Chief of Defence Forces, General Venance Mabeyo, on March 16, 2024, I am convinced and urge my fellow MPs to allow the formation of an independent commission to investigate the controversy surrounding the death of the Fifth President, Dr. John Joseph Pombe Magufuli. This is to ensure justice is served to both those mentioned positively or negatively in this matter."

He added, "The commission will also identify those who rejected the swearing-in of Dr. Samia Suluhu Hassan as the President of Tanzania when it was a constitutional requirement. Given the gravity of the issues raised by a credible institution and a credible individual, there is a need for this commission to be established."

The narrative surrounding the late President Magufuli's health has been clarified by retired General Venance Mabeyo, who revealed that Magufuli had been battling heart issues since his time at the University of Dar es Salaam. He was initially admitted to Muhimbili Hospital and later transferred to Mzena Hospital, where he unfortunately passed away. There doesn't seem to be any ambiguity in this account. The controversy might have arisen from the lack of transparency in the government's communication after the President's death. However, this doesn't warrant the formation of a commission.

Another area of contention could be the secrecy surrounding Magufuli's illness. Yet, it's known that he conducted his government affairs with a high level of secrecy, propaganda, and denial. Even when he claimed that COVID-19 had been eradicated through prayer, his government remained silent about his health condition. Similarly, when former President Mkapa fell ill, the government didn't disclose any details until his passing. In contrast, during President Samia's administration, updates were provided when President Mwinyi was unwell.

Therefore, Minister Mpina's attempt to insinuate controversy around Magufuli's death doesn't seem to be grounded in his own statements.

However, the public has proposed the formation of an independent committee to investigate key incidents that have stirred concern and controversy in Tanzania. These incidents include the disappearances of Ben Saanane and Azory Gwanda, the death of Leopold Lwajabe, the attack on Tundu Lissu in Dodoma, the kidnappings of Roma Mkatoliki and Mohamed Dewji, and the reasons behind the invasion of the Clouds Media Group studios. Establishing this committee would ensure transparency and justice for the Tanzanian public and the families affected by these events.

Maza na 4Rs zake ..... Haya ndiyo mabo ya kuyafanyia kazi.

Wasukuma mpaka leo inaelekea hawaamini kuwa mpendwa wao aliondoka kwa mapenzi ya Mungu...!!
 
Issue kwani ni kuchoma nyavu haramu au kudai pesa? Waliohonga mboana hawakuchomewa au kukamatwa/kufutiwa leseni? Ni sawa tu na JPM anakamata mafisadi ambao sio CCM ila yale majizi yaliyokua CCM hayakuguswa. Ndio hiki tunapinga double standards.
Hili kama lilitokea sina sababu ya kulitetea. Tatizo pekee ni kuwa binafsi sijui kama ilikuwa hivyo, na sijaona ushahidi nisioutilia mashaka.
Why alimtumbua? Mtu alipinga uchunguzi wa Lissu ila anashadadia uchunguzi wa JPM kama sio unafiki ni nini? Kipindi CAG analeta hoja ya 1.5 T ni huyu mpina alisema CAG anatumika na mafisadi cha ajabu leo hii anatumia ripoti za CAG kumpinga Samia!!
Kwa hiyo swala hapa ni kumpinga Samia? Angetakiwa abaki kimya kwa vile hakupinga wakati wa Magufuli?
Hujaeleza kwa ufasaha kwa nini Magufuli alimtumbua Luhaga Mpina. Ni kwa vile alikula rushwa ya wavuvi, au kuna jambo jingine?

Kama Mpina anatafuta kuteuliwa kwa kupiga kelele za kinafiki kama unavyodai, basi atakuwa na upungufu mkubwa sana kichwani mwake.
Kwa bahati nzuri kwa baadhi yetu, hizi kelele za kinafiki anazofanya ndizo tunazoona angalau zikiwastua baadhi ya wananchi juu ya mwenendo wa serikali iliyopo madarakani. Kazi ambayo tungetegemea ifanywe na wapinzani.
 
Anaitwa mtakatifu Dkt John Joseph Pombe Magufuli. Alikuwa mtu wa watu, mnyenyekevu, na mwenye hekima na uzalendo kwa taifa lake na wananchi wa Tanzania
Najua hata wewe umeandika haya huku ukicheka. Uliza Mtanzania yeyote kuwa Rais mouvu kuwahi kutokea ni nani kama Jiwe hatotajwa
 
Hili kama lilitokea sina sababu ya kulitetea. Tatizo pekee ni kuwa binafsi sijui kama ilikuwa hivyo, na sijaona ushahidi nisioutilia mashaka.
Kwa hiyo swala hapa ni kumpinga Samia? Angetakiwa abaki kimya kwa vile hakupinga wakati wa Magufuli?
Hujaeleza kwa ufasaha kwa nini Magufuli alimtumbua Luhaga Mpina. Ni kwa vile alikula rushwa ya wavuvi, au kuna jambo jingine?

Kama Mpina anatafuta kuteuliwa kwa kupiga kelele za kinafiki kama unavyodai, basi atakuwa na upungufu mkubwa sana kichwani mwake.
Kwa bahati nzuri kwa baadhi yetu, hizi kelele za kinafiki anazofanya ndizo tunazoona angalau zikiwastua baadhi ya wananchi juu ya mwenendo wa serikali iliyopo madarakani. Kazi ambayo tungetegemea ifanywe na wapinzani.
Sidhani kama nafasi za vyama vya upinzani zimeisha. Anzisha chama chako na wewe uwe mpinzani
 
Hivi watanzania mnataka nini kama sio matusi ya nguoni ? Hoja hii ingetolewa na watu wa ufipa ungeunga mkono na miguu
Watu kama nyie ndiyo mlisababisha mpaka Jiwe akawa Rais kwa ujinga wenu
 
Back
Top Bottom