Luhaga Mpina: Kuundwe Tume ya kuchunguza 'Utata' wa kifo cha Hayati Magufuli

Luhaga Mpina: Kuundwe Tume ya kuchunguza 'Utata' wa kifo cha Hayati Magufuli

Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina amesema “Baada ya kusikiliza kwa kina maelezo ya Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenari Venance Mabeyo aliyoyatoa Machi 16, 2024, nimeshawishika na ninawashawishi Wabunge wenzangu kuruhusu kuunda Tume huru ya kuchunguza utata wa kifo cha Rais wa awamu ya Tano, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli ili kumtendea haki lakini na watu wengu waliotajwa ama kwa wema au kwa ubaya katika suala hili.”

Ameongeza “Pia tume hiyo itabaini hata watu waliokataa kuapishwa kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Tanzania wakati ilikuwa ni takwa la kikatiba.

Kwa mambo yaliyosemwa na Taasisi ambayo sio ya kutiliwa mashaka na mtu ambaye si wa kutiliwa mashakaa kuna haja ya hii tume kuundwa.”

Tuanze na utata wa kifo cha Sokoine, kupotea Ben Sa8
 
Wawahoji akina kasimu majaliwa, bashiru,pole pole na Dr abas. Hawa ndo hawakutaka Samia aapishwe.
 
Waziri ovyo kabisa! Chunguza DP World, uuzaji mbuga zetu kwa waarabu, unyanyasaji wa wamasai kwa kuwaondoa kwenye ardhi yao ya asili kupisha waarabu, wizi unaoendelea kila siku, ufisadi uliojaa ndani ya serikali kwa mujibu wa ripoti ya CAG, na mengine mengi ya kutia kinyaa, ambayo yakirekebishwa, nchi itarudi kwenye hadhi yake!

Magufuli alikuwa mgonjwa wa moyo, HIV na mwisho korona; ulitegemea aponeje, haya kwa kudharau tahadhari ya korona?
 
Iundwe kamati huru kuchunguza kupotea kwa Ben Saanane na Azory Gwanda .

Kifo cha Leopold Lwajabe.

Shambulio la Tundu Lissu Dodoma.

Kutekwa kwa Roma Mkatoliki na Mohamed Dewji.

Sababu za kuvamiwa Clouds Media Group studio.

Hapa itakuwa tumeutendea haki umma wa watanzania na familia za hao watu.
100%
 
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina ameshauri Bunge liunde Tume Huru itakayochunguza Kifo alichodai kina utata cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania, Hayati John Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021.

“Baada ya kusikiliza maelezo ya Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Venance Mabeyo, ninawashawishi Wabunge wenzangu kuruhusu kuunda Tume Huru ya kuchunguza utata wa kifo cha Dkt. John Magufuli ili kumtendea haki.” — amesema Mpina.

“Pia tume hiyo itabaini hata watu waliokataa kuapishwa kwa Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Tanzania wakati ilikuwa ni takwa la Kikatiba.” — Mpina

#KitengeUpdates
 
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina ameshauri Bunge liunde Tume Huru itakayochunguza Kifo alichodai kina utata cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania, Hayati John Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021.

“Baada ya kusikiliza maelezo ya Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Venance Mabeyo, ninawashawishi Wabunge wenzangu kuruhusu kuunda Tume Huru ya kuchunguza utata wa kifo cha Dkt. John Magufuli ili kumtendea haki.” — amesema Mpina.

“Pia tume hiyo itabaini hata watu waliokataa kuapishwa kwa Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Tanzania wakati ilikuwa ni takwa la Kikatiba.” — Mpina

#KitengeUpdates
 
Tunaunga mkono hoja wtz wazalendo.hiyo tume ikimaliza ichunguze pia matumizi mabaya ya pesa za umma Kwa yule anayesafiri mara Kwa mara na kupewa vyeti fake.
 
The fact that he's dead and rotting brings us relief, as we are no longer under a dictatorship.
 
Hilo ni jukumu la CHADOMO
Mbona unaweweseka mtekaji?

Lile genge lenu mkae mkifahamu jinai haifi .

Daniel Moi alitesa watu sana Nyayo house na wengine Kamiti maximum prison kwa miaka 24 na aliamini angekuwa rais wa maisha.

Ila baada ya Kibaki kuingia madarakani 2003 ,Nyayo house torture chambers zilifunguliwa na wahanga kujitokeza rasmi japo wengine walikuwa wamekimbilia uhamishoni miaka mingi sana, eneo hilo kuwekwa wazi ilikuwa ni mkakati wa kuonyesha madhila ya utawala wake tena akiwa bado hai.

Na wahanga wa mateso hayo walilipwa japo wengine tayari walikuwa wamepoteza maisha huku na wengine kupata vilema vya kudumu.

Ujumbe wangu tu ni mmoja japo CCM mnatamba na kuonea watu vilivyo ila mjue ipo siku mtapotea kama ilivyopotea KANU maana nakumbuka nikiishi Nairobi miaka hiyo kuna hadi nyimbo alitungiwa kabisa wakiimba "KANU juu nyayo juu juu kabisa " ila leo hii KANU haijulikani hata ipo wapi.

Ni suala la muda jinai haifi ipo siku wahanga nao wa Tanzania watajitokeza na haki itatendeka hata kama muhusika atakuwa hayupo hiyo siku ipo .

 
Ka
Mkuu muosha huoshwa! Imeenda hiyo! Watu wapo masaa ya mbele!
Kauli kama hizo ndo zinazoongeza utata.
Huyo Jiwe wako alitendewa aliyokuwa anawatendea Watanzania. Bila Mungu kuingilia kati sijui Taifa hili lingekuwa wapi
Uchunguzi uanzie hapa..
KAMATI HIYO HIYO PIA ISIACHE KUCHUNGUZA KIFO CHA MPENDWA WETU MWANASIASA NGULI JASIRI LATE, BENJAMINI WILIAM MKAPA, IT WAS SO SUDDEENLY!, KUTOKA AFYA NZURI MNO, MPAKA KUFIKIA PALE!
°Alifariki wakati ambao kiongozi fulani akijaribu kujiongezea muda! Inatia shaka sana.
Kabisa,
Tutachunguza Kwa makini.
Jjiwe kajiua mwenyewe
Kauli nyengine tata.
 
Naunga mkono hoja, nimefikiri sana bila ya jibu, huo mkono wa mtu utafutwe kwa gharama yoyote ile.
 
Ni kama vile jamaa amepita na huu uzi


Screenshot_20240420-163054_1.jpg
Screenshot_20240420-162725_1.jpg
 
Back
Top Bottom