Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina amesema “Baada ya kusikiliza kwa kina maelezo ya Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenari Venance Mabeyo aliyoyatoa Machi 16, 2024, nimeshawishika na ninawashawishi Wabunge wenzangu kuruhusu kuunda Tume huru ya kuchunguza utata wa kifo cha Rais wa awamu ya Tano, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli ili kumtendea haki lakini na watu wengu waliotajwa ama kwa wema au kwa ubaya katika suala hili.”
Ameongeza “Pia tume hiyo itabaini hata watu waliokataa kuapishwa kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Tanzania wakati ilikuwa ni takwa la kikatiba.
Kwa mambo yaliyosemwa na Taasisi ambayo sio ya kutiliwa mashaka na mtu ambaye si wa kutiliwa mashakaa kuna haja ya hii tume kuundwa.”