Luhaga Mpina: Kuundwe Tume ya kuchunguza 'Utata' wa kifo cha Hayati Magufuli

Luhaga Mpina: Kuundwe Tume ya kuchunguza 'Utata' wa kifo cha Hayati Magufuli

Zama za Mpina zimekwisha,.anajaribu kufosi kiki zimtoe lakini bado zinagoma. Kapiga mdomo sana lakini sasa mwaka wa nne, hamna kitu, too much arrogance japo kichwani kajaza mapumba tu.

Baada ya uchaguzi alimdhulumu mganga wake, na mganga kampiga chombo cha kienyeji nyota zote chini, na aliyekuwa mgombea tishio kwa Mpina pale jimboni ndio anatumia mganga wa Mpina, 2025 asisingizie kukatwa na CCM, CCM hawamtaki, wavuvi wanasubiri sherehe kubwa sana siku Mpina anaangushwa
 
Akipewa Uwaziri anageuka kusifia mm ndio huwa siwaelewi hawa watu.Magufuli angesaidia hiyo nchi tungekua mbali sana.yeye alimanisha
 
Uko nje ya Maada, yeye anazungumzia Uchunguzi na sio teuzi
Huyu mpina huyu sasa amekuwa bundi kwenye kundi la njiwa. Kama yeye ni mwana-ccm anashindwa kumwamini mwenyekiti wake aliyetangaza kuwa magufuli alikufa kwa tatizo la mfumo wa umeme kwenye moyo. Au anataka kuwaamini wazushi waliosema alikufa kwa corona?
 
Huyu jamaa ushamba unamsumbua madktari wameshasema sababu zilizomuua yeye ni nani mpaka alete masharti mengine ya uchunguzi?
 
Jiwe naye alipoteza pia watu wengi wasio na hatia kipindi cha utawala wake. Auwaye kwa upanga hufa kwa upanga 🤔
 
Yaani iko hivi, ukali wa kukemea ufisadi wa Dkt Magufuli waliutumia mabeberu
Ufisadi upi huo? Kuzuia mikutano ya kisiasa iliyopo kikatiba halafu yeye anafanya ndio kukemea ufisadi...

Je nini kilimuondoa CAG Musa Assad ofisini?
kupitia mbowe na kundi lake kutekeleza mauaji ili kusema Dkt Magufuli ni Dikiteta na muuaji, hivyo inasemekana
Mbowe alimuua Azory wapi hivi unajua hata Azory haijawa confirmed kama alikufa zaidi ya kupotea tu baada ya kuchukuliwa na maofisa wa usalama ? acha kuota
Mbowe alimuua azory, kamuua ben, alimkosa kosa tundu lisu etc.
Hilo kundi la kina Mbowe linaitwaje na kwanini Mbowe hakukamatwa baada ya Dewji kupatikana?
Hata Mo alitekwa na kundi la akina mbowe na msoga ili kuleta taharuki kuwa serikali inateka watu. Kwa ufupi Dkt Magufuli was very humble and kind sana, ila baadhi ya watanzania walimzidi kete kwa kufanya matukio na kuwahi haraka haraka kuripoti kwenye vyombo vya habari. Kwa ufupi wakisema wachunguze kwa kutumia tume wengi watafungwa
Mbona unajishtukia sana wewe diehard fan wa Jiwe kwaninu unakuja na majibu ya inasemekana wakati mimi nimeona wakianzisha uchunguzi wa kifo chake basi pia tuwatendekee haki waliopotea , kuuwawa, na kutekwa kwenye utawala wake basi ufanyike uchunguzi mbona unaweweseka kusema alikuwa na roho nzuri kwani unafikiri hatujui alikuwa mtu wa namna gani hadi utuambie alikua na roho nzuri au tafsiri ya roho nzuri ni ipi?
 
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina amesema “Baada ya kusikiliza kwa kina maelezo ya Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenari Venance Mabeyo aliyoyatoa Machi 16, 2024, nimeshawishika na ninawashawishi Wabunge wenzangu kuruhusu kuunda Tume huru ya kuchunguza utata wa kifo cha Rais wa awamu ya Tano, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli ili kumtendea haki lakini na watu wengu waliotajwa ama kwa wema au kwa ubaya katika suala hili.”

Ameongeza “Pia tume hiyo itabaini hata watu waliokataa kuapishwa kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Tanzania wakati ilikuwa ni takwa la kikatiba.

Kwa mambo yaliyosemwa na Taasisi ambayo sio ya kutiliwa mashaka na mtu ambaye si wa kutiliwa mashakaa kuna haja ya hii tume kuundwa.”

Nilitamani Sana kupata mtu jasiri atakaye toa kauli hii na sasa amepatikana. Kwa kuwa kauli imesemwa basi moyo umetulia. Pumzika Magufuli lakini naamini aliyeua kwa upanga atakufa kwa upanga
 
Nilitamani Sana kupata mtu jasiri atakaye toa kauli hii na sasa amepatikana. Kwa kuwa kauli imesemwa basi moyo umetulia. Pumzika Magufuli lakini naamini aliyeua kwa upanga atakufa kwa upanga
Acha ujinga, kipindi tunamuulizia JPM ulikua unatuzodoa kuwa tunazusha!! Baada ya kifo ndio mnajifanya mko concerned naye!!
 
Mpina anayo rekodi inayozungumza yenyewe.
Rekodi gani? Anachopigania ni uwaziri, nimeshasema humu nasubiri siku atakayoteuliwa ndio mtaona atakavyokana kauli zake zote!!

Ni mnafiki tu huyo Mpina hana tofauti na majizi mengine yaliyojazana CCM.
 
Pia cha Ben Saanane na Azory Gwanda - pamoja na waliotaka kumuua Tundu Antipas Lissu.
 
Iundwe kamati huru kuchunguza kupotea kwa Ben Saanane na Azory Gwanda .

Kifo cha Leopold Lwajabe.

Shambulio la Tundu Lissu Dodoma.

Kutekwa kwa Roma Mkatoliki na Mohamed Dewji.

Sababu za kuvamiwa Clouds Media Group studio.

Hapa itakuwa tumeutendea haki umma wa watanzania na familia za hao watu.
Ongezea na kutekwa na kuteswa kwa Wakili Madeleka, Dr Steven Ulimboka, kuuwawa kwa Dr Mvungi na kumwagiwa tindikali kwa Saed Kubenea
 
Aisee hii wakiweza kuunda tume hakika taifa litapona. Yule anayejifanya lishe mara moyo anajifanya watanzania ili wasahau wakati ndiye master mind. Ila iko siku Dkt Magufuli atatendewa haki.
Hivi bado analindwa kama mwanzo?
Nadhan, hizi drama za Lishe ni ni mpango kabambe wa kusahaulisha Umma ombwd lake. Lkn Mungu yupo
 
Back
Top Bottom