Luhaga Mpina: Kuundwe Tume ya kuchunguza 'Utata' wa kifo cha Hayati Magufuli

Luhaga Mpina: Kuundwe Tume ya kuchunguza 'Utata' wa kifo cha Hayati Magufuli

Iundwe kamati huru kuchunguza kupotea kwa Ben Saanane na Azory Gwanda .

Kifo cha Leopold Lwajabe.

Shambulio la Tundu Lissu Dodoma.

Kutekwa kwa Roma Mkatoliki na Mohamed Dewji.

Sababu za kuvamiwa Clouds Media Group studio.

Hapa itakuwa tumeutendea haki umma wa watanzania na familia za hao watu.
Hilo ni jukumu la CHADOMO
 
Jiwe naye alipoteza pia watu wengi wasio na hatia kipindi cha utawala wake. Auwaye kwa upanga hufa kwa upanga 🤔
Hizo ni propaganda, Dkt Magufuli hahusiki. Mbona Dkt JK kipindi chake watu wengi walikufa au umesahau? Utasema Dkt JK anahusika? Mambo mengine tusipende kuyasema bila ushahidi. Kwa ufupi huku mitaani wanasema Dkt Magufuli aliuawa na hao waliomuua lengo la ni kurejesha mifumo ya ufisadi ambayo leo wananchi wanashuhudia. Rejea kipindi kile CAG report baada ya kufa Dkt Magufuli ilifumuliwa na kurekebishwa ili ionekane kuna wizi kipindi chake ili hii awamu ikianza kuiba iwe ilianzia kwa Dkt Magufuli. Kwa ufupi kama nchi tunahitaji kupona maana hali ni mbaya sana mitaani, alianza vizuri ila tu baada ya kuanza vijembe vya kifo cha Magufuli wananchi wakasema kumbe huyu inawezekana ndiye muuaji wa rais wetu na alimuua akijua kwa sababu yeye ndiye anayefiatia basi atakuwa rais na ndiyo maana wanasiasa wanasema kwa katiba iliyopo makamu anaweza kumuua rais ili awe rais na unaweza kuta kumbe wanamaanisha kwa kilichotokea 2021 maana siyo vijembe hivyo etc. Ni Makonda pekee alianza kufuta hiyo dhana.
 
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina amesema “Baada ya kusikiliza kwa kina maelezo ya Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenari Venance Mabeyo aliyoyatoa Machi 16, 2024, nimeshawishika na ninawashawishi Wabunge wenzangu kuruhusu kuunda Tume huru ya kuchunguza utata wa kifo cha Rais wa awamu ya Tano, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli ili kumtendea haki lakini na watu wengu waliotajwa ama kwa wema au kwa ubaya katika suala hili.”

Ameongeza “Pia tume hiyo itabaini hata watu waliokataa kuapishwa kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Tanzania wakati ilikuwa ni takwa la kikatiba.

Kwa mambo yaliyosemwa na Taasisi ambayo sio ya kutiliwa mashaka na mtu ambaye si wa kutiliwa mashakaa kuna haja ya hii tume kuundwa.”

Mtu alikuwa mgonjwa,akauguzwa Hadi akafa inahitaji Tume?

Basi iundwe na Mwenyekiti awe Mpina
 
Hizo ni propaganda, Dkt Magufuli hahusiki. Mbona Dkt JK kipindi chake watu wengi walikufa au umesahau? Utasema Dkt JK anahusika? Mambo mengine tusipende kuyasema bila ushahidi. Kwa ufupi huku mitaani wanasema Dkt Magufuli aliuawa na hao waliomuua lengo la ni kurejesha mifumo ya ufisadi ambayo leo wananchi wanashuhudia. Rejea kipindi kile CAG report baada ya kufa Dkt Magufuli ilifumuliwa na kurekebishwa ili ionekane kuna wizi kipindi chake ili hii awamu ikianza kuiba iwe ilianzia kwa Dkt Magufuli. Kwa ufupi kama nchi tunahitaji kupona maana hali ni mbaya sana mitaani, alianza vizuri ila tu baada ya kuanza vijembe vya kifo cha Magufuli wananchi wakasema kumbe huyu inawezekana ndiye muuaji wa rais wetu na alimuua akijua kwa sababu yeye ndiye anayefiatia basi atakuwa rais na ndiyo maana wanasiasa wanasema kwa katiba iliyopo makamu anaweza kumuua rais ili awe rais na unaweza kuta kumbe wanamaanisha kwa kilichotokea 2021 maana siyo vijembe hivyo etc. Ni Makonda pekee alianza kufuta hiyo dhana.
Naona umeandika waraka mrefu kumtetea Jiwe. Labda nikukumbushe tu raisi ni Amiri Jeshi Mkuu. Yupo juu ya vyombo vyote vya ulinzi na usalama. Ikitokea raia kuumizwa, kuuwawa au kupotea, na bila hatua stahiki kuchukuliwa, yeye ndiye wa kwanza anapaswa kulaumiwa🤔
 
Hili swala nilishawahi sema ipo siku itakuja kufanyika uchunguzi. Kidaktari kifo cha Rais Magufuli hakikuwa cha kawaida. Kifo cha Rais Magufuli kilikuwa na hujuma.

Naunga mkono hoja ya Luhaga Mpina. Tusipofanya leo itakuwa ni kawaida kufanya assassination kwa Marais wetu. Na hii itapelekea kuyumba kwa Taifa. Kifo cha Rais Magufuli dots za kidaktari zinagoma kabisa kabisa kuwa alikufa kifo cha ugonjwa wa Moyo.

Kifo cha Rais Magufuli Clinical analysis inagoma kabisa kama kweli alikufa kwa corona.

Ukitaka ujue kifo cha Rais kulikuwa na hujuma angalia walikufa watu wote waliokuwa Ikulu. Wote aliowaamini, waliomzunguka. Kama ni corona inawezaje iue watu wa eneo moja tu tena kwa kufuatana. Afu watu ambao walikuwa hawakutani na watu wengi to that extent. Watu wa mtaani huku tulikuwa tunakaa hovyo hatuna Any precautions Lakini hatukufa. Sayansi inagoma kabisa kuwa Magufuli alikufa kifo cha kawaida.

Naunga mkono hoja ili tujenge misingi imara ya ulinzi wa Marais wetu. Hata kama siyo leo hata kesho au awamu yeyote nashauri wafanye uchunguzi wa kina. Magufuli for me with my own reasoning hakufa kifo cha kawaida
 
Naona umeandika waraka mrefu kumtetea Jiwe. Labda nikukumbushe tu raisi ni Amiri Jeshi Mkuu. Yupo juu ya vyombo vyote vya ulinzi na usalama. Ikitokea raia kuumizwa, kuuwawa au kupotea, na bila hatua stahiki kuchukuliwa, yeye ndiye wa kwanza anapaswa kulaumiwa🤔
Nakubaliana 💯 percent. Ndiyo maana tunahitaji katiba ili rais asiendelee kubebeshwa kila baya. Mfano kwa sasa Dkt Samia anabebeshwa vitu vingi vibaya wakati kuna baadhi ya watendaji ndiyo wenye shida
 
Mbunge km huyu Kuna wananchi nao walipanga foleni kwenda kumpigia kura penginepo jua likiwachomaa😅😅.

Badala ya kupigania serikali iachee kuiba na kuleta maendeleo ,yupo busy kumuwaza marehemuu..
Shenzi kabsView attachment 2968569
KIFO Kila nafsi itapatwa na kufikiwa na KIFO,Tulio hai hatupendi kusikia mpendwa wetu amefariki,tunafikia hata hatukubali kuwa umri wa miaka 50na kuendelea ni umri wa kufariki,na walio hai wenye umri wa miaka 80 ni wachache mno,na wenye miaka 100ni. kama hamna,hamna kabisa kwa walio hai Kila KIFO kinasababishwa na aliyefariki mwenyewe,marafiki au maadui zake.Mwl Nyerere alipofariki,minong'ono ilikuwa mingi hata kwa kina Kighoma,Balali,Sokoine,Kolimba,Wangwe,Mkapa,Omari,Membe,Lowasa&Sefu.....Tulio hai ni vigumu kukubali utadhani MUNGU hakusema Kila nafsi ni lazima ionje mauti😭
 
Ndugu mpina ,Samia anasema kijitabu kijitabu,Kwanza ilitakiwa mabeyo akamatwe Kwa kuvunja katiba ,Nani alimwambia awe msemaje wa familia?

Yaani katiba inauzwa shs 10000 pale kariakoo alishindwa kwenda kusoma utaratibu wa Rais akifa Nani anafuata?Mabeyo akaisaidie polisi!Joni amekufa 2021 Kwa nini hiyo hadithi asimulie Sasa?
CDF unafikiri ni mtu wa mchezo mchezo eti?!
 
Iundwe kamati huru kuchunguza kupotea kwa Ben Saanane na Azory Gwanda .

Kifo cha Leopold Lwajabe.

Shambulio la Tundu Lissu Dodoma.

Kutekwa kwa Roma Mkatoliki na Mohamed Dewji.

Sababu za kuvamiwa Clouds Media Group studio.

Hapa itakuwa tumeutendea haki umma wa watanzania na familia za hao watu.
Sawa kabisa, maana huyo Luhaga anataka kutuaminisha Magufuli alikuwa mtu msafi, hivyo kifo chake pekee ndio Cha kuundiwa kamati. Ikiundwa kamati kuchunguza vifo vyote vyote wakati wa Magufuli, Nina hakika Kinga dhidi ya Marais itaondolewa kwenye katiba.
 
Kwa hao wote mbowe anahusika na genge lake la mabeberu walitaka kutengeneza taharuki. Akamatwe gaidi mbowe kwanza maana kesi alifutiwa na Dkt Samia
Hivi watu wasiyojulikana+ Bashite waliletwa na nani vile?
 
Aisee hii wakiweza kuunda tume hakika taifa litapona. Yule anayejifanya lishe mara moyo anajifanya watanzania ili wasahau wakati ndiye master mind. Ila iko siku Dkt Magufuli atatendewa haki.
Huyo Jiwe wako alitendewa aliyokuwa anawatendea Watanzania. Bila Mungu kuingilia kati sijui Taifa hili lingekuwa wapi
 
Back
Top Bottom