Luhaga Mpina: Kuundwe Tume ya kuchunguza 'Utata' wa kifo cha Hayati Magufuli

Luhaga Mpina: Kuundwe Tume ya kuchunguza 'Utata' wa kifo cha Hayati Magufuli

Iundwe kamati huru kuchunguza kupotea kwa Ben Saanane na Azory Gwanda .

Kifo cha Leopold Lwajabe.

Shambulio la Tundu Lissu Dodoma.

Kutekwa kwa Roma Mkatoliki na Mohamed Dewji.

Sababu za kuvamiwa Clouds Media Group studio.

Hapa itakuwa tumeutendea haki umma wa watanzania na familia za hao watu.
Mkuu umeneena ukweli, uchunguzi uanze kwanza wa hao watanzania uliowataja hapo juu, ndio ufuate uchunguzi wa kifo cha Mwendazake.

Mpina asijifanye maumivu ya kifo cha msukuma mwenzake yanauma kuliko ya mtanzania mwingine wa jamii nyingine!!

Haki itendeke kwa wote!
 
Mtu alikuwa anatumia mashine ya moyo, bado akaji expose kwenye Corona. Unashangaaje kukata?

Kuhusu watu waliotaka kupindua meza labda wachunguzwe wajulikane kwa ajili ya kupongezwa maana kwa kweli waliona mbali..Samia hawezi
Mkuu swala ni kutoweza au ni katiba kutofatwa baada ya kifo cha Mwendazake???
 
Naunga Mkono hoja.

Watanzania huu ni wakati muafaka ya Kutafuta majibu.

Ukisoma nyuzi nyingi hapa kabla na baada ya Kifo chake, utagundua wapo watu ambao kwa lugha walizozitumia na wanazotumia, ni kwamba Raisi Wetu Aliuwawa??
Mkuu uko sahihi ila haki ianze na waliuawa kabla yake na yeye au utawala wake!

Yeye hakuwa bora kuliko wengine, uhai wake haukuwa wa thamani kuliko wa wengine walio kufa mikononi mwake!

Haki itendeke kwa wote!!!
 
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina amesema “Baada ya kusikiliza kwa kina maelezo ya Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenari Venance Mabeyo aliyoyatoa Machi 16, 2024, nimeshawishika na ninawashawishi Wabunge wenzangu kuruhusu kuunda Tume huru ya kuchunguza utata wa kifo cha Rais wa awamu ya Tano, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli ili kumtendea haki lakini na watu wengu waliotajwa ama kwa wema au kwa ubaya katika suala hili.”

Ameongeza “Pia tume hiyo itabaini hata watu waliokataa kuapishwa kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Tanzania wakati ilikuwa ni takwa la kikatiba. Kwa mambo yaliyosemwa na Taasisi ambayo sio ya kutiliwa mashaka na mtu ambaye si wa kutiliwa mashakaa kuna haja ya hii tume kuundwa.”

🔥🔥🔥
 
Tunaenda mbela hatua moja tunarudi nyuma hatua tatu, Mpaka tutaufikia ukoloni na Uchief mangungo wa enzi za mjerumani.

Hayo tuachane nayo yanatupotezea muda na pesa yashapita na hayana faida tena.
 
Sio ndio ina maana Uchunguzi Ufanyike. Wewe hutaki kujua kwanini Lissu alirindimwa na Risasi? Hutaki kujua labda kawa sababu kama hiyo labda wakatumiwa na mahasimu wa Taifa hili kumfikia Raisi?
Mkuu hakuna sababu yoyote kikatiba inayoruhusu mtanzania yeyote awe Rais au raia kuua mtanzania mwingine.

Rais hana haki wala mamlaka hayo sehemu yoyote kikatiba ya kuua tu! hakuna kitu kama hicho!

Kama ni uchunguzi uanze na waliouwawa chini ya utawala wake yeye Magufuli, halafu ndio uje kwenye kifo chake mwenyewe!

Haki itendeke kwa wote kwa usawa!
 
Unaogopa nini kitafichuliwa? Hutaki kujua Kwanini Tundu Lissu alipigwa Risasi? Je, kupigwa kwa Tundu Lissu Risasi kulikuwa na njama za kujibu shambulizi?
Mkuu usipindishe mambo kwa kudhani watu wamesahau, sababu kubwa ya Tundu Lisu kupigwa Risasi ni kutokana na msimamo wake dhidi ya dhuluma na uongo wa Magufuli kuhusu kodi ya kampuni ya madini ya Acacia.

Mkuu Kitendo kilichopelekea Magufuli kumuita Tundu Lisu msaliti, na kutamka msaliti huuwawa. Usaliti wa Lissu lilikuwa jambo ambalo sio la kweli.

Kwa kauli ya Kabudi mwenyewe anajuta kwa kuwa sehemu ya uongo wa kamati ya Osoro kuhusu malimbikizo ya kubambikiza ya kodi kwa kampuni ya Acacia, yaliyokadiriwa kufikia trilioni 400!

Mwisho wa siku wakaja kuambulia bilioni 300 kishika uchumba kati ya billion 700 ya kwa mkataba mpya wa kugawana manufaa ya uwekezaji sio faida ya uwekezaji!

Na makinikia wakayaachia na mpaka leo yanatoka kwenda nje!!! That means Tindu Lissu was right!

Uchunguzi ufanyike juu ya hilo, na Tundu Lissu apate haki yake!
 
Aisee hii wakiweza kuunda tume hakika taifa litapona. Yule anayejifanya lishe mara moyo anajifanya watanzania ili wasahau wakati ndiye master mind. Ila iko siku Dkt Magufuli atatendewa haki.
Mkuu uchunguzi ufanyike kwa wote waliouwa mikononi mwake na juu ya kifo chake mwenyewe.

Mkuu usifikiri uhai wa watanzania wengine hauna thamani! Wote wapate haki sawa!
 
Dah umenikumbusha hiyo thread, yaani imeanika uhusika wa current ceo na born town yaani hawa watu ni wauji na kibaya kabisa damu ya Dkt Magufuli inawasumbua hawakai kimya lazima wakiongea tu wanajikuta wameropoka viashiria kuwa wao ndiyo walimuua ili wafanya ufisadi etc
Mkuu muosha huoshwa! Imeenda hiyo! Watu wapo masaa ya mbele!
 
Nimewahi kuandika humu na na ninaandika tena, kwa sababu kuna makundi mawili hasimu hayakukubaliana kuhusu mustakabali wa Tanzania baada ya Kifo cha Magufuli na kuvunja utaratibu wa kikatiba, licha ya Samia kuwa next in power succession, kwa sababu ya mapungufu ya kiufundi kwenye hichi kifo, Samia anaweza kuhesabika alifanya uasi, kama watu wakiamua kushikilia bango.

Samia na wafuasi wake wanaweza kuja kupewa kesi kubwa ya Uhaini, Majaliwa kuendelea kuwa Waziri mkuu kwa kujua au kutokujua inampa Samia aina fulani ya Kinga na kumuweka Majaliwa Mateka (Waziri mkuu asiye na nguvu, ila anazuia reaction ya kisiasa na kiutawala).

Hili Jambo watu wenye akili nchini walisuruhishe kabla halijawa armed conflits
Mkuu hilo halitotokea tena, every area of interest is neutralized and under serious surveillance and monitoring.

Every and all threatening moves are all under watch and done away with silently and squarely.

The lesson was noted and learned once and for all. No making mistakes again, not at all, not again!
 
Hiyo ni sawa na kusema, hao mnaowatumia kama ndio kihalalisho cha kifo chake, mfano kina Ben saananee, Tundu Lissu Mdude n.k Kama ilishatokea, ishatokea. Mjadala ufungwe?

Watu wakisema 'kwani Akwilina hakutakiwa kufa' 'Kakufa tu' shida ipo wapi? Ama Tundu Lissu alikipata alichokuwa anakitafuta, shida ipo wapi? Au Ben saanane-Si walijitakia??

Unaona ukinzania wa hoja yako?
Mkuu naona sasa unaona umuhimu wa kufanya uchunguzi kwa watanzania wote kama ifuatavyo; kwanza waliokufa mikononi mwa Magufuli na utawala wake!

Pili uchunguzi juu ya kifo cha hayati Mkapa, then tuje Kwenye kifo cha maalim seifu na mwisho ndio tumalizie kwa Mwendazake mwenyewe!

Bila hivyo tupige kimya, Maisha yasonge mbele!!
 
Mbunge km huyu Kuna wananchi nao walipanga foleni kwenda kumpigia kura penginepo jua likiwachomaa[emoji28][emoji28].

Badala ya kupigania serikali iachee kuiba na kuleta maendeleo ,yupo busy kumuwaza marehemuu..
Shenzi kabsView attachment 2968569
Jaribu kuushughulisha ubongo wako kidogo mkuu. Unakumbuka Mpina alichangia nini kwenye sakata la DP WORLD?..

Kuna hoja nyingi sana na Ngumu mpina kajitoa Muhanga kuziongea mpaka unamuonea huruma kwamba huyu anaotezwa kesho(in Kagera's chairman for UVCCM)
 
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina amesema “Baada ya kusikiliza kwa kina maelezo ya Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenari Venance Mabeyo aliyoyatoa Machi 16, 2024, nimeshawishika na ninawashawishi Wabunge wenzangu kuruhusu kuunda Tume huru ya kuchunguza utata wa kifo cha Rais wa awamu ya Tano, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli ili kumtendea haki lakini na watu wengu waliotajwa ama kwa wema au kwa ubaya katika suala hili.”

Ameongeza “Pia tume hiyo itabaini hata watu waliokataa kuapishwa kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Tanzania wakati ilikuwa ni takwa la kikatiba.

Kwa mambo yaliyosemwa na Taasisi ambayo sio ya kutiliwa mashaka na mtu ambaye si wa kutiliwa mashakaa kuna haja ya hii tume kuundwa.”

Ndiyo mlicho kiteta na kukubaliana na Sirro, Pengo na Bashite?
 
Back
Top Bottom