Lukuvi, mbio za sakafuni huishia ukingoni; jitafakari

Lukuvi, Moja ya Mzee Makini sana na Tunu Kwa Taifa.

Kwa Taifa hili lenye Vijana wajinga waimbao mapambio Kila uchwao.

Mzee anahitajika sana ,tumuombee uzima, 2025 sio mbali.
Ni matumaini yangu kwamba unakielewa unachoandika hapa, nami nafungua masikio nisikilize zaidi kumhusu huyu mTanzania, ambaye ninamchukulia kuwa tofauti kidogo na hawa wengine waliko huko ndani ya chama hicho.

Ni juu yake sasa kusimama ili watu wamwone na kumpima zaidi.
 


CCM haiko hivyo Mkuu, lile pepo la Nyerere kwa bahati mbaya sana lilikuwa linaogopa yeyote anayekubalika kwa wananchi kinyume na wazee wa Chama , na Mzee wa Chama akigundua hilo ujuwe umekwenda na maji ,.

mfano Kambona, Sokoine , Kolimba nk........
 
Niseme tu kwamba sikubaliani na dhana yako ya kipuuzi!
 
ni wapi palifanyika uchaguzi 2020 ?
Waulize kina mbowe na kina sugu watakuambia kichapo walichokula.

Usichokijua ni kuwa kushinda kwa upinzani huwa inategemea mpasuko wa ccm. Kura nyingi za upinzani huwa zinatoka ccm. CCM wakiwa pamoja upinzani mtaimba mashairi yote.

Hata kina msigwa kupata ubunge ni sababu ya kutoswa fredrick mwakalebela kule iringa,
Sugu ilikuwa vita ya makundi ccm mbeya mjini na maeneo mengine mengi tu, jaribu kufuatilia.

Hata 2015 ilichagizwa na kukataliwa ccm hadi na wana ccm wenyewe. 2020 ccm wameungana mmebaki mnaimba tu upinzani ooh kuhujumiwa ooh uchafuzi.

Maneno matatu matukufu ya Magu yalikuwa;
1. Nipeni connection.
2. Msichanganye gunzi na betri tochi haitawaka.
3. Nipeni huyu nammudu naweza kumuwajibisha, mkinipa wa kule sitaweza kumuwajibisha.

Haya maneno yaliwaponda mno upinzani.
 
Mkuu arudi kwa Mzindakaya yupi...marehemu au mwingine
 
Niseme tu kwamba sikubaliani na dhana yako ya kipuuzi!
Una uhuru wa Kukubali na kutokubali lakini ukweli ndio huo. Sokoine alienda , Kambona aliponea chupuchupu kwa kumbilia UK , Kolimba alienda na maji
 
Wadanganye wajinga sana , Huyo Magufuli tulifahamu mwezi mmoja kabla kwamba amejiandalia kura mil 12 , mbona yeye mwenyewe hakushinda kihalali na alikuwa gunzi , angewezaje kuwasaidia wengine ?

Unapaswa kuwa mjinga sana kuamini kwamba Magufuli alishinda kihalali
 
Apambane kupitia wapi ili awe nani ??-- njia iliyokuwepo ni kupitia chama chake, na mkuu wa chama ambaye ndiye Rais hawaivi tena😏.

Labda atoke CCM aende akachukluwe nafasi ya marehemu Mrema 😛 😛
 
Apambane kupitia wapi ili awe nani ??-- njia iliyokuwepo ni kupitia chama chake, na mkuu wa chama ambaye ndiye Rais hawaivi tena😏.
Kupitia humo humo CCM.
Hakuna wakati mzuri, au niseme, haijawahi kuwepo na wakati mzuri kuliko sasa hivi ndani ya chama hicho kujitokeza mbele na kupambana.
Huyo Mwenyekiti sasa hivi usitishike juu yake. Hana nguvu za ushawishi ndani ya hilo lichama.
Unachoona sasa hivi ni unafiki wa kawaida tu unaofanyika kila mara ndani ya chama hicho.

Anachotakiwa kufanya Lukuvi, au hata na wengine wenye misimamo ndani ya chama hicho, wajitoe kufanya kazi ya kujitambulisha kwa wanachama wenzao. Hili linawezekana bila kufanya kelele nyingi, na haihitaji ruhusa ya mtu yeyote kufanya hivyo.
 
Una uhuru wa Kukubali na kutokubali lakini ukweli ndio huo. Sokoine alienda , Kambona aliponea chupuchupu kwa kumbilia UK , Kolimba alienda na maji
Natumia uhuru wangu kukataa upuuzi.
 
Na unatakiwa ujitoe akili kuamini Magu hakushinda kihalali. Nyie si kila siku mnatupa idadi ya watu wanaojiandikisha kupitia ile kampeni maarufu ya chadema kidigitali ambayo kwa sasa hatukusikii tena humu ukiipigia chapuo.? Au lengo la ile kampeni ni nini? Kutafuta watu wa kuandamana barabarani?

Sasa wenzenu wakisema wana mtaji wa kura hizo we unaumia, ila we ukisema ni sawa.

Nakusisitizia tena, upinzani hawashindi bila kupata kura za wanaccm, na ili kupata kura za wanaccm ni lazima kwanza itokee mipasuko ya kimakundi. Ombeeni hilo litokee kila chaguzi, utanishukuru badae.
 
Mkuu kama hutojali tuongee na Wanasheria ili urejeshewe eneo lako
Sagai Ni Tapeli tu huyo kutwa nzima kutukani mimatusi,naomba umpe Darasa awe Kama wewe kutumia lugha za heshima staha na kujifunza kuvumilia kwa wale anaotofautiana nao mitizamo siyo kutukana tu utafikiri amekunywa vimiminika na Moshi upo kichwani mwake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…