Duh, mbona mada yako hii inachanganya mkuu 'sammonssee'!
Nilipoanza kukusoma, nilidhani unamtia moyo huyo Lukuvi, ili asibweteke, bali ajipime na kutafakari vyema historia ya utumishi wake na nafasi yake katika nchi hii, ili aone kama anafaa kuitumikia zaidi katika ngazi za juu zaidi kuliko alizozifikia kwa uteuzi.
Ajipime, katika utumishi wake, kama waTanzania waliweza kuona juhudi zake katika kuwatumikia, na arudi kwao kwa mipango maalum awaombe wamtazame tena kama anafaa kuendelea kuwatumikia..
Lakini, kwa mafadhaiko kwa wengi, Lukuvi nadhani amekuwa kama viongozi wengine wote walioko huko CCM, ambao inaonyesha wanapoachwa katika nafasi za uteuzi wanakuwa hawana mawazo mengine zaidi. Hii ni ishara kwamba utumishi wao katika nafasi wanazopewa, si kwa wananchi, bali kwa hao wanaowateua kwenye nafasi hizo.
Viongozi waliomo CCM, hawajui kujijenga kwa wananchi moja kwa moja, hata kama wanaonekana kufanya kazi vizuri, badala yake utumishi wao wanaukabidhi kwa hao wanaowateua, na mara wanapoachishwa hizo nafasi, hawajui pa kuanzia ili kuwaended wananchi.
Kwa maoni yangu, hili ndilo tatizo alilopata Lukuvi, na ni kwa bahati mbaya sana, kwani kwa utendaji wake alioonyesha, ingekuwa rahisi kukumbushia tu kwa wananchi wampime zaidi na kumwamini kuwafanyia kazi zaidi endapo wangeridhia. Yeye kaweka kila kitu kwa akina Samia!
Inasikitisha sana.