Lukuvi: Tukipitisha serikali tatu jeshi litatawala nchi

Lukuvi: Tukipitisha serikali tatu jeshi litatawala nchi

Mkuu ndicho umeona cha maana kuandika hapa sijaona hoja hata moja pengine jipange vizuri utulie na ujenge hoja kwa kutueleza nini unachokitaka kutueleza vema lakini kwa hizi hoja ni nyepesi sana.

Kama hicho kilichosemwa katika uzi huu sio "hoja", basi maana ya neno "hoja" haipo. Nionavyo mimi mleta hoja amejaribu vizuri kutupa angalizo dhidi ya kauli zinazotolewa na watu wenye dhamana ya kuhakikisha usalama wa taifa letu, lakini badala yake kwa makusudi kabisa wameamua kutetea hoja za kubakiza mamlaka yao kwa gharama yoyote ikiwemo kupandikiza hofu na hata kuliandalia jeshi mazingira ya kutwaa utawala wa nchi iwapo hoja yao itashindwa.
 
Uamsho ni CUF,na CUF ni Uamsho.by Lukuvi Mapema leo bungeni.bunge la Intarahamwe!
 
Msameheni bure kwan alikuwa anakwenda milembe ya india.
 
Kwa taarifa tu
1. Cheo chochote jini ya meja ndani ya jeshi anaweza kuandamana na kudai haki ndani ya serikali
2. Cheo chochote zaidi ya meja yaani Lt. Cornell hawezi kuandamana kuidai serikali ila anaweza kuifukuza serikali iliyopo madarakani na sio kuipindua jeshi
3. Mwanajeshi hawezi kujipandisha cheo, ni lazima apandishwe na kamati husika
4. Mimi natamani uasi utokee ili tuifukuze ccm madarakani nchi ipate uhuru, na nitakuwa mtu wa kwanza kuwaunga mkono waasi haraka sana
5. Nchi yetu inaweza kuendelea kuwa masikini miaka mingi ijayo,
 
Tumezisikia kauli nyingi kutoka kwa viongozi wakuu wa CCM akiwa nzima na Jakaya Kikwete ambaye ni Rais wa nchi na mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama , alisema kuwa katiba ikiruhusu kuwa na serikali tatu , basi jeshi ndio ambalo litachukua nchi , hii ni kauli ya kuamsha hisia za Jeshi kujiandaa kumpindua huyu Rais ajaye wa Tanganyika ............

Lukuvi , leo ameendeleza kauli hizo hizo kuwa jeshi litapindua endapo kutakuwa na serikali tatu ,hii ni kuendeleza kuchochea hisia za Mapinduzi kwenye jeshi letu na kuwaandaa kisaikolojia kuwa kumbe wataweza kuipindua serikali wakati Wowote .

Huu ni muendelezo wa mchezo ambao CCM wamekuwa wakifanya tangu baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na walifanya kikao kimoja Kibaha. Na walitoa maelekezo ya hovyo ambayo yalipingwa vikali sana na viongozi wa jeshi waliokuwa wamehudhuria kwenye kongamano hilo la mwaka 2011 na hata 2012 liliitishwa tena , hivyo kauli hizi sio za kupuuzwa hata kidogo , ni lazima zichukuliwe kwa tahadhari kubwa .

Ninategemea kuwa busara za viongozi wa jeshi sasa zitawale naw ajitokeze na waseme hadharani kuwa hawataki kuingizwa kwenye siasa na wawatake wanasiasa kuacha kuwachonganisha na wananchi na jeshi Lao .

Ni vyema sasa Kia mmoja kwa kutumia nafasi yake katika jamii ahakikishe kuwa sasa anatumia kila njia kuwataka viongozi aw CCM na serikali kuacha mara moja kuchochea hisia za Mapinduzi kwa jeshi letu ambalo Lina nidhamu kubwa na ya kuigwa hapa nchini, Afrika na ulimwennguni mwote.
 
cjaona wazir wa ajabu kama lukuvi kwel kavurugwa kwa kuongea ujinga bungeni.
 
Naona leo ndo wanatambulishana bungeni... Kwa mbwembwe zote... Njaa mbaya sana.
 
Interahamwe hawawezi kukubali madhambi yao mpaka wafanye vitu vyao! Ccm wametuchanganya sana kwa kung'ang'ania maoni yao ndio yawe katiba mpya!
 
Hakuna chochote kitachozuia mm kusema,nitasema kweli na nitarudia kusema kweli nikweli cku ,,,tbc wanakataka matangazo jamani kudadedeki tbccc,,,,

kila mmoja wetu angeshangaa kusikia Lukuvi anakubali kuwa yeye ni mnafiki
 
Kaa mkao wa kula nchi iko halijojo na ni matokeo ya kuendekeza wanasiasa na vyama badala ya maslahi ya nchi!!!
Tunasema kila uchao hapa misukule ya vyama wanawapa nguvu sana viongozi wa vyama vyao to an extent hawaoni wala hawasikii nini kizuri au kibaya!!!!!!
Wananchi wangekuwa na umoja wa kukemea viongozi wao wala wasingefikisha nchi hapa!!!!!!

Angalia hizi chache!!!!!
1. Nchi haitatawalika........................
2. Mkiikosa kwenye katiba ya zamani basi mtaikuta kwenye katiba mpya............

Hawa wanawasemea wafuasi wao na walishangiliwa kwani mbegu gani ilikuwa ikipandwa hapo!!!??????

Kama wewe ni mshabiki wa vyama basi ujue wewe ni sehemu ya haya matatizo na kama uko sober basi tuendelee kuelimisha umma kuwa kushiriki siasa sio mbaya ila kuwa msukule na kuburuzwa ndio njia ya kuelekea kaburini!!!!!!!
 
Tumezisikia kauli nyingi kutoka kwa viongozi wakuu wa CCM akiwa nzima na Jakaya Kikwete ambaye ni Rais wa nchi na mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama , alisema kuwa katiba ikiruhusu kuwa na serikali tatu , basi jeshi ndio ambalo litachukua nchi , hii ni kauli ya kuamsha hisia za Jeshi kujiandaa kumpindua huyu Rais ajaye wa Tanganyika ............

Lukuvi , leo ameendeleza kauli hizo hizo kuwa jeshi litapindua endapo kutakuwa na serikali tatu ,hii ni kuendeleza kuchochea hisia za Mapinduzi kwenye jeshi letu na kuwaandaa kisaikolojia kuwa kumbe wataweza kuipindua serikali wakati Wowote .

Huu ni muendelezo wa mchezo ambao CCM wamekuwa wakifanya tangu baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na walifanya kikao kimoja Kibaha. Na walitoa maelekezo ya hovyo ambayo yalipingwa vikali sana na viongozi wa jeshi waliokuwa wamehudhuria kwenye kongamano hilo la mwaka 2011 na hata 2012 liliitishwa tena , hivyo kauli hizi sio za kupuuzwa hata kidogo , ni lazima zichukuliwe kwa tahadhari kubwa .

Ninategemea kuwa busara za viongozi wa jeshi sasa zitawale naw ajitokeze na waseme hadharani kuwa hawataki kuingizwa kwenye siasa na wawatake wanasiasa kuacha kuwachonganisha na wananchi na jeshi Lao .

Ni vyema sasa Kia mmoja kwa kutumia nafasi yake katika jamii ahakikishe kuwa sasa anatumia kila njia kuwataka viongozi aw CCM na serikali kuacha mara moja kuchochea hisia za Mapinduzi kwa jeshi letu ambalo Lina nidhamu kubwa na ya kuigwa hapa nchini, Afrika na ulimwennguni mwote.

sheikh yahaya aliwai kutabiri 2009 kua baada ya uchaguzi kutatokea mapinduzi sasa naanza kupata picha
 
Back
Top Bottom