Tumezisikia kauli nyingi kutoka kwa viongozi wakuu wa CCM akiwa nzima na Jakaya Kikwete ambaye ni Rais wa nchi na mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama , alisema kuwa katiba ikiruhusu kuwa na serikali tatu , basi jeshi ndio ambalo litachukua nchi , hii ni kauli ya kuamsha hisia za Jeshi kujiandaa kumpindua huyu Rais ajaye wa Tanganyika ............
Lukuvi , leo ameendeleza kauli hizo hizo kuwa jeshi litapindua endapo kutakuwa na serikali tatu ,hii ni kuendeleza kuchochea hisia za Mapinduzi kwenye jeshi letu na kuwaandaa kisaikolojia kuwa kumbe wataweza kuipindua serikali wakati Wowote .
Huu ni muendelezo wa mchezo ambao CCM wamekuwa wakifanya tangu baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na walifanya kikao kimoja Kibaha. Na walitoa maelekezo ya hovyo ambayo yalipingwa vikali sana na viongozi wa jeshi waliokuwa wamehudhuria kwenye kongamano hilo la mwaka 2011 na hata 2012 liliitishwa tena , hivyo kauli hizi sio za kupuuzwa hata kidogo , ni lazima zichukuliwe kwa tahadhari kubwa .
Ninategemea kuwa busara za viongozi wa jeshi sasa zitawale naw ajitokeze na waseme hadharani kuwa hawataki kuingizwa kwenye siasa na wawatake wanasiasa kuacha kuwachonganisha na wananchi na jeshi Lao .
Ni vyema sasa Kia mmoja kwa kutumia nafasi yake katika jamii ahakikishe kuwa sasa anatumia kila njia kuwataka viongozi aw CCM na serikali kuacha mara moja kuchochea hisia za Mapinduzi kwa jeshi letu ambalo Lina nidhamu kubwa na ya kuigwa hapa nchini, Afrika na ulimwennguni mwote.