balibabambonahi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 15,771
- 14,294
Mkuu acha uongo,Jamaa alikufa katika mazingira ya ugomvi uliomuhusisha Lulu na Lulu ndo anajua na ndo maana ni lone suspect.Seth ni shahid tuu,ushahidi wake unatakiwa uendane na material facts ya kesi husika,Seth akisema mambo ambayo hayana kushabihiana na kesi au kuonesha Lulu si muhusika inawezekana Lulu akachomoka lakini Seth hawez kuwa hatiani labda upande wa mashtaka ushtaki upya na Seth awe suspect.Kumbuka Lulu alisha plead manslaugthter,kama hii ni kweli kitakachofanyika mitigating process ya kumpunguzia ukali wa adhabu.Ila huyu Seth Ana mengi ya kuiambia mahakama....Hata siku ile ya msiba anahojiwa na vyombo vya habari hakuwa anaonekana na huzuni wala mawazo alikuwa anatiririka tu.
Na hata maelezo yake ya Leo mahakamani kama Lulu akipata wakili mzuri basi kesi yote itahamia kwa Seth maana inaonyesha kuna mengi anayojua Ila hataki kuyasema pengine kwa Makusudi au kwa kuamua kufanya siri.
Humu Lulu anachomoka bila kufungwa....Kama Kanumba mwili wake ungekutwa na sumu,majeraha au angekufa kwa silaha Lulu angekuwa kwenye matatizo.
Ila kwa kesi jinsi ilivyo Lulu anachomoka na Seth asipopanga vzuri utetezi wake ataishia pabaya.