M-wekeza kutoka Vodacom Riba 13%

Hamna atakayezidi ile 15%+ ya BOT kwa sababu wote hao ni madalali wa BOT.

Mnawapa hela wao wanapeleka BOT wakipewa ile 15%+ yao wao wanawapa 13% wanabakiwa na 2% faida yao.
Hizi bonds za mabenki(nmb,azania, e.t.c) wanasema zinaenda kusaidia wajasiriamali wadogo/vijana/wanawake. Kuna bonds za kimataifa zinauzwa mpaka nchi za nje.


Ila uhalisia
Hizo bonds nahisi zinanaenda BOT lakini pia zinaenda kukopesha watu wengine hasahasa watumishi wa umma ambao ni risk free ni mwendo wa kukata moja kwa moja kwenye mishahara yao. Halafu asilimia ndogo sana wanakopeshwa wafanyabiashara wakubwa wenye assets kubwa na cash flow kubwa sana. Hao wajasiriamali wadogo/vijana/wanawake ndio wanapewa Asilimia ndogo mno kwa ajili ya kuzugia tu.

 
Hio ni passive income mzee sio biashara ya kukupa faida kila siku😆! Badala ya kuweka hela ikakaa bila kuzalisha unaiweka humo. Gawio lako la 13M kama una watoto uhakika wa ada unakuwepo bila kelele kila January.
Mi nawashangaa wanaopigia hesabu hizo faida na kufananisha na tangible business, huko mtu anaweka kujimake tu, yaani uko na ka 1M useme uweke huko udownload pesa, huo ni uongo .
 
Tangu watupige tukio kwenye hisa, hata mpesa siwaamini
 

hii ni product ya Sanlam.. wameamua ku patner na vodacom kutumia Customer database ya vodacom.. wameona wakianza habari za kutengeza app mara kuanza kujitangaza.. watachelewa.. so wao wanakaa nyuma vodacom ambaye tayari ana product za kifedha mfano mpesa, mpawa,mkoba. mgodi ambazo amepatner na tasisi zingine za kifedha itakuwa rahis kuwa convice wateja hil la uwekezaji na watu wakavutika
 
Kuna kuwa na mkataba? Je ikitokea bahati mbaya mtu amepoteza maisha je, kuna utaratibu umeandaliwa kiwango husika kupewa ndugu wa karibu wa huyo atayesepa? Maisha hayana guarantee kwa sasa, japo hatuombeani mabaya lakini ni vizuri kuchukua tahadhari.
Huwa najiuliza hivi watu wanapofariki viakiba vyao vya kwenye mitandao ya simu si huwa inabaki kuwa mali ya wenye mtandao?
Ama kweli, maisha yanahitaji ujanja na umakini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…