Tetesi: M23 wamepewa kichapo na wamerudishwa nyuma baada na za Vikosi Maalum vya DRC kuingia Goma

Tetesi: M23 wamepewa kichapo na wamerudishwa nyuma baada na za Vikosi Maalum vya DRC kuingia Goma

M23 hawataki kuwasikia JWTZ wanakwambia "hawa JW NI hatari wanapiga usiku, mchana, jua mvua wao wanapiga tu hujui hata wanakula na kulala saa ngapi? NI wao ndio walituondoa" kile kipindi walichopigwa wakakimbilia Uganda [emoji3][emoji3]

hahahaha tuache kuishi kwa historia, mfumo wa vita umebadirika sana sasa hivi.
Na tuwe makini sana kujiingiza kwenye hizi vita, kuna watu wana hamu sana na sisi.
 
Msituni sio kazi kufika Kinshasa, mkishavunjwa defensive line yenu tu watu wanaserereka kama ilivyomkuta Mobutu offguard.

Vijana wakiCongo wanapaswa sasa kuifia nchi yao ili wasichezewechezewe Kila siku.
Hii kazi wasiiachie jeshi peke yake, hii kazi iwe ni kwa waCongoman wote kuanzia Kasumbalesa, Kolwezi, Lubumbashi na Katanga yote, kurudi Kinshasa, Kisangani, Bukavu, nk

Ni wakati sasa waCongo watangaze Fatwa, Kila Mcongo popote alipo duniani aje aipiganie nchi yake, uzalendo ndio iwe nyimbo kwenye maredio nk.
Wanasiasa waache kunywa chai Kinshasa, Paris, Belgium wajitolee nao na familia zao kuilinda nchi, Kila kijana above 18 ajiunge na jeshi kwa lazima, muziki upige marufuku kwa muda iwe nyimbo zakuhamasisha tu..nk.
Hahahaha,khaa umesikika Mkuu
 
Inaripotiwa kuwa, mpaka majira ya saa 5 usiku, waasi wa M23 wameshindwa kuushika mji wa Goma na wameanza kuzidiwa.

Hii ni baada ya askari wa ranks za captain na Lieutenants kuoongoza vikosi vya jeshi la Kongo baada ya majenerali na wengine wa vyeo vya juu kukimbia.

Screenshot_20250128-143534.jpg
Screenshot_20250128-143452.jpg
Screenshot_20250128-143444.jpg
 
Siyo kweli kwamba WaCongoman siyo wazalendo kwa nchi yao, la hasha. Kabla ya kuwalaumu hao raia/Wananchi tunapaswa tujiulize: Je, ni kwa nini hasa huko DR Congo Vita na uasi havikomi miaka nenda rudi? Nini hasa kiini au chanzo cha kuwepo kwa huo Mgogoro na vurugu zisizoisha huko DR Congo?

Kimsingi, DR Congo kuna matatizo mengi Sana ambayo yanasababisha hali hiyo ya kuwepo kwa migogoro na Vita isiyokwisha.

Kwa kifupi, DR Congo is a failed State! Hakuna Utawala ulio madhubuti nchini DR Congo, Utawala wake unaundwa na Magenge ya Watu wachache Sana ambao umejikita kwenye ufisadi na uporaji wa rasilimali za nchi hiyo ili kujinufaisha wao wenyewe pamoja na Vibaraka wao (wafuasi wao wachache) ambao wamejikita huko Kinsasha huku kundi kubwa zaidi la Wananchi wengi zaidi wa nchi hiyo wamebaki kuwa mafukara wa kupindukia.

Mbaya zaidi Sana, Utawala wa nchi hiyo unafanya Siasa za Propaganda hatari za Kuwagawa Watu kwa misingi ya Ukabila, Ukanda, Itikadi za Siasa, n.k. Siasa za kuwagawa watu ni jambo baya na la hatari kubwa sana, matokeo yake ndiyo hayo unayoyaona ya Wanajeshi kuasi na kujiunga na Wapiganaji Waasi.

Hata baadhi ya Wananchi wengi waishio kwenye hayo maeneo yenye vurugu na Vita wamekuwa wakiwaunga mkono Waasi wa M23.
Watu wa mashariki mwa DRC hawathamiwi hata kidogo na wale wa kuanzia Mbuji-Mayi kuelekea mashariki up to Kinshasa ndiyo maana unakuta loyalty kwa M-23 upande wa Eastern DRC inakuwepo kwani vinginevyo wangekuwa wameshamalizwa kitambo.
 
Congo ni nchi yenye mfumo wa jeshi mbovu sana sasa afisa mwenye rank ya major General anaendaje front line kuongoza mapigano. Hao junior officers wanakazi gani mpaka senior officers kama brig general na major general waokaongoze vita ndiyo maana yule Gavana major general kauawa
Mkuu,
Kwenye falme za zamani watawala wa falme ndio waliongoza battle field mfano kina mfalme daudi pia hata kule Korea kina JUMONG.

Ni kawaida kwa kamanda alie iva vizuri kutamani kuongoza askari wake kuwapa molari mstari wa mbele vitani..
 
Jana jioni breaking news Goma imeangushwa sasa unakuja habari nyengine, chanzo chako ni mashaka mashaka ueandika na kujithibitishia mwenyewe
Niwekee thread hiyo unayodai niliweka jana kuwa Goma imeangushwa
 
Fuatilia historia ya nchi hiyo hususani kuhusiana na masuala haya ya Majeshi ya Ulinzi kwenye nchi hiyo.

Dikteta Mobutu Sese Seko aliwavuruga hasa, kwanza Jeshi la Ulinzi la Taifa hilo aliligawa katika makundi kama mawili hivi:- Jeshi/Kikosi Maalumu Cha Kumlinda yeye Rais wa nchi hiyo, pamoja na Kikosi kingine Cha Ulinzi wa nchi.
Vikosi hivi vilikuwa na Wakuu wake, ambapo Kikosi Maalumu Cha Kumlinda Rais kilikuwa kinapewa upendeleo zaidi, Mkuu wa Kikosi hiki alikuwa hapokei Amri kutoka kwa Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo (CDF), Bali yeye alikuwa kama CDF Daraja la Kwanza ambaye alikuwa anawezeshwa kwa kila kitu kuanzia Fedha, Vifaa vya Kijeshi, n.k, Kikosi hiki Wanajeshi wake walikuwa wapo karibu zaidi na Rais wa nchi huku kile Kikosi kingine Cha Jeshi la Ulinzi wa nchi kikiwa dhaifu Sana kupita kiasi kwani walikuwa hawana Fedha za kutosha za kuendesha shughuli za kijeshi, Vifaa vichache na duni, Dis-organozation ya Mfumo wa Utawala wa Jeshi lenyewe wakati walikuwa na Hukumu kubwa zaidi la kulinda Nchi hiyo yote kabisa.
Ndio maana unaona hata Waasi walipoanzisha Vita ya Mapinduzi ya Utawala wa Rais Mobutu Sese Seko Mwaka 1997 hawakuwahi kukumbana na upinzani mkali Sana kutoka kwa. Jeshi la Ulinzi la nchi hiyo. Hali iliyosababisha hata Rais Mobutu Sese Seko kuhisi kwamba Mkuu wa Majeshi General Mahele alikuwa anafanya usaliti dhidi yake yeye. Rais. Mwisho wake Mobutu Sese Seko aliamua kumteka huyo Mkuu wa Majeshi General Mahele na kumuua kikatili Sana.
Udhaifu wa Jeshi la Ulinzi la nchi hiyo ni tatizo la kihistoria, lilianzia tangu zamani
I was waiting for this comment, at least wewe unaifahamu historia ya jeshi la DRC and the then Zaire. Wengi humu hawaelewi historia wala kinachoendelea muda huu, wanahisi wanabishana mambo ya CCM vs CHADEMA yaani ushabiki zaidi ya uhalisia.
 
Hivi ikija timbwili kama hili,mtaweza kuhimili? Mapambano ya miaka yote yaani ukiamka ,ukilala ni bunduki tu
Mkuu nadhani hiki ulichosema ndicho kinawafanya watu waseme DRC ina jeshi dhaifu miaka yote wameshindwa kuwaeliminate m23, maana nchi yoyote inayojielewa na ina jeshi imara haiwezi kulea timbwili linalohatarisha usalama wa nchi yake.
 
Msituni sio kazi kufika Kinshasa, mkishavunjwa defensive line yenu tu watu wanaserereka kama ilivyomkuta Mobutu offguard.

Vijana wakiCongo wanapaswa sasa kuifia nchi yao ili wasichezewechezewe Kila siku.
Hii kazi wasiiachie jeshi peke yake, hii kazi iwe ni kwa waCongoman wote kuanzia Kasumbalesa, Kolwezi, Lubumbashi na Katanga yote, kurudi Kinshasa, Kisangani, Bukavu, nk

Ni wakati sasa waCongo watangaze Fatwa, Kila Mcongo popote alipo duniani aje aipiganie nchi yake, uzalendo ndio iwe nyimbo kwenye maredio nk.
Wanasiasa waache kunywa chai Kinshasa, Paris, Belgium wajitolee nao na familia zao kuilinda nchi, Kila kijana above 18 ajiunge na jeshi kwa lazima, muziki upige marufuku kwa muda iwe nyimbo zakuhamasisha tu..nk.
Kwanza wenyewe kwa wenyewe hawapendani na wala hawaaminiani, watu wa Eastern hawawakubali kabisa hawa wanaoitwa Waswahili and vice versa. Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa za Banga alishawagawanya(divide and rule system) wakajengewa kuchukiana na kutokuaminiana na hiyo kuja kuifuta it's an uphill task, itachukua muda mrefu na waanze na watoto wadogo sumu walizopandikizwa hawa wa zamani gradually zitafifia na hatimaye kutoweka kabisa otherwise wagawane nchi yaani wa huku wa huku na wa kule wa kule.
 
Back
Top Bottom