Huu ni mkakati wa kijinga na WA kufikirika TU, hautakaa uwezekane milele.
Wala sidhani kama Kagame anaweza kuwaza jambo la hatari namna hii kwake na watakaomfuata.
Hebu fikiria ugumu huu.
Vita baada ya kujaribu kutaka kukamata mojawapo ya nchi anazotamani kuzikamata kabla ya kuishinda nchi hiyo ili kwenda kuikamata nchi nyingine itapiganwa bila mwisho kwa miaka nenda miaka Rudi.
Sababu Iko hivi,huko congo Rwanda wala kagame haiungwi mkono na watu wote Raia wa congo,hivyo hawatakubali kushindwa.congo kama congo Ina nchi marafiki hawatakuabtayari kuiachia congo iangukie mikononi mwa Rwanda.
Hali Iko hivyo kwa Uganda,Burundi na Tanzania.
Nchi hizi kama ilivyo congo kagame haungwi mkono na raia wa nchi hizi walq Hana kabila linalomuunga mkono zaidi ya jamii wa Warusi wachache TU wasiojitambua wanaopatikana kidogo Burundi na kwa uchache Uganda,Tanzania ndio hakuna kabisa.
Sasa jamii ndogo TU ya wanyarwanda ndio itingishe mbuyu wenye miaka mingi namna hiyo?
Ndugu yangu ,kagame Hana jeshi la namna hiyo,mambo mengine tuanamsingizia TU ama tuanamkuza TU.
Mfano mmoja TU kuishinda Tanzania hiyo ni ndoto.
Lakini hata ikitokea Tanzania ikazidiwa ujue Kuna nchi ndogondogo na kubwa zitaingia upande wa Tanzania kwa sababu za kihistoria.
Sababu za kihistoria ni kwamba nchi kama south Afrika,Angola,msumbiji,Zambia,Botswana haziwezi kuiacha Tanzania ikaanguka.
Hizo nchi ni kama Tanzania aliwekeza.
Rwanda hata akisaidiwa na USA Kaa ukijua kua Urusi,china na Korea kaskazini na baadhi ya nchi kubwa hazitakaa kimya kuiacha nchi rafiki ikianguka.
Huko nimeenda mbali sana kuonesha ugumu wa kagame kwa kile unaita ni mkakati .
Lakini Hali halisi ni kwamba Tanzania peke yetu TU kagame hawezi kufanya lolote.yaani wamuone mwaka wa kwanza kaishinda DRC,mwaka wa pili kaishinda Burundi,mwaka wa Tatu kaishinda Uganda ,halafu Tanzania wamekaa TU.hakuna kitu kama hicho.
Kwanza kabisa Rwanda haiwezi kuishinda DRCpeke yake wala Uganda peke yake,na hata Burundi vita itapiganwa muda mrefu sana.vita ya kuiteka nchi na kuyaweka mikononi mwako majeshi yote ya nchi unayopigana nayo ni ngumu sana.
Vita hubadilika na kua vita vya msituni ama mtaa kwa mtaa baada ya jeshi kuona Sasa limepoteza udhibiti wa maeneo muhimu.hapa hata raia wa kawaida walio wengi huacha shughuli zao na kuingia vitani kwa mtindo wa waasi,wapigania uhuru ama askari wa msituni.kuwatuliza watu Hawa ni miaka na miaka Hadi utakapokubali yaishe.mfano wapalestina, Mujahedeen,Porisalio,umkhonto we swize,MPLA,etc.
Kagame Hana ubavy huo,Hana watu na walq hawezi kujaribu kuonja sumu kwa kuilamba.