Nimekuuliza kwamba umejuaje uliyojua?Mapungufu ya ushahidi niliyokupa ni Yepi? au unadhani Yesu alikuja kudhurula huku duniani bila kuwa na wenyeji?
Mkuu bado huu sio ushahidi kabisa...Mkuu ukisoma katika Biblia inaonyesha ya kwamba Taifa la Israel lilikuwepo kipindi cha Yesu... na Unajua Bwana Yesu alitumwa katika nyumba ya Israel...
Mathayo 21:43 Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake.
Yohana 18:35 Pilato akajibu, Ama! Ni Myahudi mimi! Taifa lako na wakuu wa makuhani ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini?
Nimekuuliza kwamba umejuaje uliyojua?
Umesoma mahali?
Au umeota ndoto?
Hujajibu hayo kabisa!
Mkuu bado huu sio ushahidi kabisa...
Wayahudi kuwepo wakati wa Yesu sio ushahidi wa kuwepo taifa hilo kwani hata baada ya miaka 1000 baada ya Yesu walikuwepo pia
Kuna mahali popote ambapo panaonesha uwepo wa taifa la Israeli kwa maandishi kuwa lilikuwepo wakati wa Yesu?
Mkuu hili jambo inaonekana tunalikubali kinadharia zaidi ya kiuhalisia maana sikumbuki kama hata kwenye agano jipya kuna mahali panainesha hili!
Mkuu bado huu sio ushahidi kabisa...
Wayahudi kuwepo wakati wa Yesu sio ushahidi wa kuwepo taifa hilo kwani hata baada ya miaka 1000 baada ya Yesu walikuwepo pia
Kuna mahali popote ambapo panaonesha uwepo wa taifa la Israeli kwa maandishi kuwa lilikuwepo wakati wa Yesu?
Mkuu hili jambo inaonekana tunalikubali kinadharia zaidi ya kiuhalisia maana sikumbuki kama hata kwenye agano jipya kuna mahali panainesha hili!
Mkuu,mbona hapo kuna nchi ya Yuda?Mkuu umekuwaje tena!? kwa mfano hii mistari inayo sema Bethlehemu uliyo mdogo, kama hakukuwa na Taifa la Israel iweje irejewe katika nchi ya Yuda!?
Hii sio wakati wa Yesu .....Mika 5:2 Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele
Hapo nchi iliyokuwepo ni Yuda na sio IsraeliMathayo 2:6 Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli.
Hii ni sawa,Halafu unajua tena ya kwamba Israel iligawanyika katika Falme mbili, Falme ya Israel na Falme ya Yuda... na Hata jina Wayahudi lilitokana na kabila la Yuda, Wayahudi halikutumiwa katika Agano la kale kabla ya Ufalme kugawanyika, Sehemu ya kaskazini iliitwa Israel na Kusini Ikaitwa Yuda, Lakini wote hao walikuwa Waisrael kwa maana ni wazao wa damu wa Yakobo, waliitwa Wayuda ili kuwatofautisha na Ufalme wa Kaskazini. Baadaye waliitwa Wayahudi
Hapana,Yeremia 34:9 ya kwamba kila mtu amweke huru mtumwa wake, na kila mtu amweke huru mjakazi wake, ikiwa yule mwanamume au yule mwanamke ni Mwebrania; mtu ye yote asiwatumikishe, yaani, asimtumikishe Myahudi, nduguye;
Hizi falme mbili tofauti hazikuangamizwa kwa wakati mmoja na hata waliowasambaratisha ni watu tofautiBaadae hizo falme mbili ziliangamizwa halafu wakapelekwa uhamishoni, Baadae kurudi kutoka uhamishoni uzao wa wengi uliorudi ulikuwa ukitoka katika Ufalme ule wa kusini yaani Wayahudi, baadae hilo jina likaanza kutumika kwa wote
Mkuu kwenye hiyo ramani mbona sioni mahali ambapo inaonesha nchi ya Israeli?
Naona Samaria na Judea tu
Hayo maelezo yaliyoko pembeni hayaendani na hiyo ramani hapo kuanzia hiyo bendera hadi huyo Netanyahu!
Nimesoma kwenye Biblia.
Mbona maeneo yaliyoandikwa ni mengi tu. au computer/simu yako imedelete?
**** kitu kinaitwa "sampling",hiyo inamaana kuwa huna haja ya kuchukua yote unayotaka kuyatolea maelezo bali unaweza kuchukua baadhi tu na kuelezea unachotaka kuelezea
Hapo nimetumia Netanyahu kama "sampling" ya nilichokueleza lakini haina maana hakuna mkanganyiko mwingine,upo tena mwingi tu
Wakati wa hayo mataifa mawili wala hawakuwa wakizungumza Kiarabu kama walivyoandika hapo
Kila taifa lilikuwa na mji wake mkuu na sio kwamba ulikuwa ni Jerusalem tu!
Mataifa mawili yepi tena?
Israel na Judea .....
Eiyer, Israel ni Yakobo... Yuda ni moja ya kabila la Israel, na alikuwa mtoto wa Yakobo... kwani kumuita Myuda ni Muisrael kuna shida gani!? Israel ilikuwa moja kipindi cha Selemani... baadae iligawanyika zigawa mbili, kutofautisha moja ikaitwa Israel nyingine Yuda, na hilo kabila la Yuda ndio lilikuwa kubwa... Baadae wale wengine hawakuwepo ikabaki Yuda... nchi ya Yuda...
Wayahudi ni Waisrael, kwani kuna Ubaya gani Yuda ikiwa ni Israel!?
Unanichanganya sasa, au msimamo wako wa Israel kutokuwa Taifa umebadirika. unapobadirika uwe unatoa taarifa mkuu.
Post zako zinazidi kutia mashaka na utakatifu wa Biblia.Ni vyema uliza wakati mwingine Biblia ni mkusanyiko wa vitabu wajua pana Maandiko na Neno.
Hata shetani pia hutumia hiyo hiyo Biblia kwa maana ya Maandiko ili apotoshe ukweli.
Pia fahamu pana
Sehemu ya Maisha ya Mwili imejitokeza sana Agano la kale na hasa zimetumika Tamaduni za Israel na makabila yake
Na pana Maisha ya kiroho hii utaipata zidi katika Agano jipya
Ndio maana walipo sikia mfalme amezaliwa iliwapashida sana...kumbe si ufalme wa Dunia hii kwa maana ya mwili.
Mtoa maada amepost andiko lijadiliwe, kama lilivyo na si vinginevyo kama alivyotanabaisha mtoa maada.
Tunapoja jadiri mambo km haya hasa kwa madai mazito kwamba kuna vitu Yesu alibadirisha ni vema tukaambatanisha na ushahidi wa kimaandiko kabisa.
Yuda ndio Israel sasa, Ukirejea kipindi cha Waajemi baada ya kuwaruhusu Wayahudi walirudi kwao lakini walikuwa chini ya utawala wa Waajemi, waliunganikana hakukuwa na tofauti kati ya watu wa Kaskazini na Kusini kwa maana ya mgawanyiko. Taifa lililojengwa upya liliweza kuitwa Israel au Yuda, kwasababu lilikuwa maendelezi ya kweli ya Israel ya kale...Sijasema kuna shida kuwaita Wayahudi Waisraeli ila kuna shida kuwaita Walawi Wayahudi,sijui unaiona tofauti hapo?
Yuda ni jina la mtoto wa Israeli lakini pia ni kabila la moja kati ya makabila 12 ya Israeli ambae ni Yakobo,lakini kuna nchi iliyoitwa Yuda ambalo ni jina la kabila lakini pia ni jina la mtu,Ni sawa na kuna nchi iliyokuwa inaitwa Israeli ambalo ni jina la mtu pia
Kuwepo na kabila la Yuda hakufanyi kusiwepo na nchi inayoitwa Yuda au mtu aliyeitwa Yuda!