Ma-expert wa bible msaada kidogo kunifafanulia hili

Ma-expert wa bible msaada kidogo kunifafanulia hili

Mapungufu ya ushahidi niliyokupa ni Yepi? au unadhani Yesu alikuja kudhurula huku duniani bila kuwa na wenyeji?
Nimekuuliza kwamba umejuaje uliyojua?

Umesoma mahali?

Au umeota ndoto?

Hujajibu hayo kabisa!
 
Mkuu ukisoma katika Biblia inaonyesha ya kwamba Taifa la Israel lilikuwepo kipindi cha Yesu... na Unajua Bwana Yesu alitumwa katika nyumba ya Israel...

Mathayo 21:43 Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake.

Yohana 18:35 Pilato akajibu, Ama! Ni Myahudi mimi! Taifa lako na wakuu wa makuhani ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini?
Mkuu bado huu sio ushahidi kabisa...

Wayahudi kuwepo wakati wa Yesu sio ushahidi wa kuwepo taifa hilo kwani hata baada ya miaka 1000 baada ya Yesu walikuwepo pia

Kuna mahali popote ambapo panaonesha uwepo wa taifa la Israeli kwa maandishi kuwa lilikuwepo wakati wa Yesu?

Mkuu hili jambo inaonekana tunalikubali kinadharia zaidi ya kiuhalisia maana sikumbuki kama hata kwenye agano jipya kuna mahali panainesha hili!
 
map_of_an_alternate_israel_by_ieph-d7gcj4z.png
 
Mkuu bado huu sio ushahidi kabisa...

Wayahudi kuwepo wakati wa Yesu sio ushahidi wa kuwepo taifa hilo kwani hata baada ya miaka 1000 baada ya Yesu walikuwepo pia

Kuna mahali popote ambapo panaonesha uwepo wa taifa la Israeli kwa maandishi kuwa lilikuwepo wakati wa Yesu?

Mkuu hili jambo inaonekana tunalikubali kinadharia zaidi ya kiuhalisia maana sikumbuki kama hata kwenye agano jipya kuna mahali panainesha hili!

Mkuu umekuwaje tena!? kwa mfano hii mistari inayo sema Bethlehemu uliyo mdogo, kama hakukuwa na Taifa la Israel iweje irejewe katika nchi ya Yuda!?

Mika 5:2 Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele

Mathayo 2:6 Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli.

Halafu unajua tena ya kwamba Israel iligawanyika katika Falme mbili, Falme ya Israel na Falme ya Yuda... na Hata jina Wayahudi lilitokana na kabila la Yuda, Wayahudi halikutumiwa katika Agano la kale kabla ya Ufalme kugawanyika, Sehemu ya kaskazini iliitwa Israel na Kusini Ikaitwa Yuda, Lakini wote hao walikuwa Waisrael kwa maana ni wazao wa damu wa Yakobo, waliitwa Wayuda ili kuwatofautisha na Ufalme wa Kaskazini. Baadaye waliitwa Wayahudi

Yeremia 34:9 ya kwamba kila mtu amweke huru mtumwa wake, na kila mtu amweke huru mjakazi wake, ikiwa yule mwanamume au yule mwanamke ni Mwebrania; mtu ye yote asiwatumikishe, yaani, asimtumikishe Myahudi, nduguye;

Baadae hizo falme mbili ziliangamizwa halafu wakapelekwa uhamishoni, Baadae kurudi kutoka uhamishoni uzao wa wengi uliorudi ulikuwa ukitoka katika Ufalme ule wa kusini yaani Wayahudi, baadae hilo jina likaanza kutumika kwa wote
 
Mkuu kwenye hiyo ramani mbona sioni mahali ambapo inaonesha nchi ya Israeli?

Naona Samaria na Judea tu

Hayo maelezo yaliyoko pembeni hayaendani na hiyo ramani hapo kuanzia hiyo bendera hadi huyo Netanyahu!
 
Mkuu umekuwaje tena!? kwa mfano hii mistari inayo sema Bethlehemu uliyo mdogo, kama hakukuwa na Taifa la Israel iweje irejewe katika nchi ya Yuda!?
Mkuu,mbona hapo kuna nchi ya Yuda?

Israeli inatoka wapi?
Mika 5:2 Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele
Hii sio wakati wa Yesu .....
Mathayo 2:6 Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli.
Hapo nchi iliyokuwepo ni Yuda na sio Israeli

Israeli inayotajwa hapo sio nchi bali ni "familia" ya Yakobo....
Halafu unajua tena ya kwamba Israel iligawanyika katika Falme mbili, Falme ya Israel na Falme ya Yuda... na Hata jina Wayahudi lilitokana na kabila la Yuda, Wayahudi halikutumiwa katika Agano la kale kabla ya Ufalme kugawanyika, Sehemu ya kaskazini iliitwa Israel na Kusini Ikaitwa Yuda, Lakini wote hao walikuwa Waisrael kwa maana ni wazao wa damu wa Yakobo, waliitwa Wayuda ili kuwatofautisha na Ufalme wa Kaskazini. Baadaye waliitwa Wayahudi
Hii ni sawa,

Baada ya mgawanyo kulikuwepo na nchi iliyoitwa Israeli na nchi ya Yuda,lakini wakati Yesu anakuja hapa duniani nchi ya Israeli haikuwepo kabisa nchi iliyokuwepo ni Yuda tu
Yeremia 34:9 ya kwamba kila mtu amweke huru mtumwa wake, na kila mtu amweke huru mjakazi wake, ikiwa yule mwanamume au yule mwanamke ni Mwebrania; mtu ye yote asiwatumikishe, yaani, asimtumikishe Myahudi, nduguye;
Hapana,

Wayahudi sio watoto wote wa Yakobo au kwa jina lingine Israeli bali ni watu wa kabila la Yuda tu

Wayahudi ni Waebrania lakini Wabenjamini au Walawi sio Wayahudi ...
Baadae hizo falme mbili ziliangamizwa halafu wakapelekwa uhamishoni, Baadae kurudi kutoka uhamishoni uzao wa wengi uliorudi ulikuwa ukitoka katika Ufalme ule wa kusini yaani Wayahudi, baadae hilo jina likaanza kutumika kwa wote
Hizi falme mbili tofauti hazikuangamizwa kwa wakati mmoja na hata waliowasambaratisha ni watu tofauti

Nchi ya Israeli ilivamiwa na Waashuru mwaka 722 B.C na ilikoma miaka kama 500 baadae,yaani baada ya muda huo hakukuwa tena na nchi ya Israeli

Nchi ya Yuda yenyewe ilikuja kusambaratishwa na utawala wa Rumi mwaka 70 A.D

Kwahiyo hayo mataifa yana historia tofauti kabisa na wakati wa Yesu hakukuwa na nchi iliyoitwa Israeli!
 
Mkuu kwenye hiyo ramani mbona sioni mahali ambapo inaonesha nchi ya Israeli?

Naona Samaria na Judea tu

Hayo maelezo yaliyoko pembeni hayaendani na hiyo ramani hapo kuanzia hiyo bendera hadi huyo Netanyahu!

Mbona maeneo yaliyoandikwa ni mengi tu. au computer/simu yako imedelete?
 
Mbona maeneo yaliyoandikwa ni mengi tu. au computer/simu yako imedelete?

**** kitu kinaitwa "sampling",hiyo inamaana kuwa huna haja ya kuchukua yote unayotaka kuyatolea maelezo bali unaweza kuchukua baadhi tu na kuelezea unachotaka kuelezea

Hapo nimetumia Netanyahu kama "sampling" ya nilichokueleza lakini haina maana hakuna mkanganyiko mwingine,upo tena mwingi tu

Wakati wa hayo mataifa mawili wala hawakuwa wakizungumza Kiarabu kama walivyoandika hapo
Kila taifa lilikuwa na mji wake mkuu na sio kwamba ulikuwa ni Jerusalem tu!
 
Mataifa mawili yepi tena?
 
Eiyer, Israel ni Yakobo... Yuda ni moja ya kabila la Israel, na alikuwa mtoto wa Yakobo... kwani kumuita Myuda ni Muisrael kuna shida gani!? Israel ilikuwa moja kipindi cha Selemani... baadae iligawanyika zigawa mbili, kutofautisha moja ikaitwa Israel nyingine Yuda, na hilo kabila la Yuda ndio lilikuwa kubwa... Baadae wale wengine hawakuwepo ikabaki Yuda... nchi ya Yuda...

Wayahudi ni Waisrael, kwani kuna Ubaya gani Yuda ikiwa ni Israel!?
 
Last edited by a moderator:

Sijasema kuna shida kuwaita Wayahudi Waisraeli ila kuna shida kuwaita Walawi Wayahudi,sijui unaiona tofauti hapo?

Yuda ni jina la mtoto wa Israeli lakini pia ni kabila la moja kati ya makabila 12 ya Israeli ambae ni Yakobo,lakini kuna nchi iliyoitwa Yuda ambalo ni jina la kabila lakini pia ni jina la mtu,Ni sawa na kuna nchi iliyokuwa inaitwa Israeli ambalo ni jina la mtu pia

Kuwepo na kabila la Yuda hakufanyi kusiwepo na nchi inayoitwa Yuda au mtu aliyeitwa Yuda!
 
Unanichanganya sasa, au msimamo wako wa Israel kutokuwa Taifa umebadirika. unapobadirika uwe unatoa taarifa mkuu.

Sijakataa popote kuwepo kwa nchi inayoitwa Israeli,ila nimekataa kuwepo kwa nchi iliyoitwa Israeli wakati wa Yesu kuwepo duniani

Tuliza kichwa uelewe hayo...

Sikuchanganyi bali unajichanganya mwenyewe!
 
Ni vyema uliza wakati mwingine Biblia ni mkusanyiko wa vitabu wajua pana Maandiko na Neno.

Hata shetani pia hutumia hiyo hiyo Biblia kwa maana ya Maandiko ili apotoshe ukweli.

Pia fahamu pana
Sehemu ya Maisha ya Mwili imejitokeza sana Agano la kale na hasa zimetumika Tamaduni za Israel na makabila yake

Na pana Maisha ya kiroho hii utaipata zidi katika Agano jipya

Ndio maana walipo sikia mfalme amezaliwa iliwapashida sana...kumbe si ufalme wa Dunia hii kwa maana ya mwili.

Mtoa maada amepost andiko lijadiliwe, kama lilivyo na si vinginevyo kama alivyotanabaisha mtoa maada.
Post zako zinazidi kutia mashaka na utakatifu wa Biblia.
Hiki kitabu ili uamini yaliomo inabidi unapokisoma akili yako uweke pembeni.
 
Tunapoja jadiri mambo km haya hasa kwa madai mazito kwamba kuna vitu Yesu alibadirisha ni vema tukaambatanisha na ushahidi wa kimaandiko kabisa.

Kutoshika Sabato.

Yohana 05 : 01 - 19 inasema......

1 Baada ya hayo palikuwa na sikukuu ya Wayahudi; naye Yesu akakwea kwenda Yerusalemu.
2 Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania Bethzatha, nayo ina matao matano.
3 Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza, [wakingoja maji yachemke.
4 Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka, akaingia katika ile birika, akayatibua maji. Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona ugonjwa wote uliokuwa umempata.]
5 Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane.
6 Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima?
7 Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu.
8 Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende.
9 Mara yule mtu akawa mzima, akajitwika godoro lake, akaenda. Nayo ilikuwa ni sabato siku hiyo.
10 Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwambia yule aliyeponywa, Leo ni sabato, wala si halali kwako kujitwika godoro.
11 Akawajibu, Yeye aliyenifanya kuwa mzima ndiye aliyeniambia, Jitwike godoro lako, uende.
12 Basi wakamwuliza, Yule aliyekuambia, Jitwike, uende, ni nani?
13 Lakini yule mtu aliyeponywa hakumjua ni nani; maana Yesu alikuwa amejitenga, kwa sababu palikuwa na watu wengi mahali pale.
14 Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.
15 Yule mtu akaenda zake, akawapasha habari Wayahudi ya kwamba ni Yesu aliyemfanya kuwa mzima.
16 Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwudhi Yesu, kwa kuwa alitenda hayo siku ya sabato.
17 Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi.
18 Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu. Basi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambia,
19 Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile.
 
Sijasema kuna shida kuwaita Wayahudi Waisraeli ila kuna shida kuwaita Walawi Wayahudi,sijui unaiona tofauti hapo?

Yuda ni jina la mtoto wa Israeli lakini pia ni kabila la moja kati ya makabila 12 ya Israeli ambae ni Yakobo,lakini kuna nchi iliyoitwa Yuda ambalo ni jina la kabila lakini pia ni jina la mtu,Ni sawa na kuna nchi iliyokuwa inaitwa Israeli ambalo ni jina la mtu pia

Kuwepo na kabila la Yuda hakufanyi kusiwepo na nchi inayoitwa Yuda au mtu aliyeitwa Yuda!
Yuda ndio Israel sasa, Ukirejea kipindi cha Waajemi baada ya kuwaruhusu Wayahudi walirudi kwao lakini walikuwa chini ya utawala wa Waajemi, waliunganikana hakukuwa na tofauti kati ya watu wa Kaskazini na Kusini kwa maana ya mgawanyiko. Taifa lililojengwa upya liliweza kuitwa Israel au Yuda, kwasababu lilikuwa maendelezi ya kweli ya Israel ya kale...

Ingawa wengi walikuwa watu wa Yuda... Labda nikuulize swali, kina Ezra na Nehemia walijenga Taifa lipi!? Halafu hao Wayuda (Wayahudi) ndio waliweza kusimama katika mstari na misingi, kipindi cha Israel imegawanyika mji mkuu wa Israel ulikuwa Shekemu baadae Tirza halafu tena Samaria mpaka mwisho wa Ufalme wa Israel, Yuda yenyewe mji mkuu wake ulikuwa Yerusalemu

Halafu kipindi Yeroboamu anaongoza Israel dini yake iliunganisha na desturi za kikanaani na za Israel, halafu si walikuwa wamejitenga na Ufalme wa Yuda kwa hiyo hawakuweza kwenda kuabudu Yerusalemu lilipokuwa hekalu... Yeroboamu alijenga madhababhu mjini Dani, kukata stori...

Kama nilivyoeleza hapo mwanzo kina Ezra na Nehemia walipokuja kujenga tena hapakuwa na tofauti za mgawanyiko japokuwa wengi walikuwa Wayahudi, chini ya uongozi wa Zerubabeli na kuhani mkuu Yoshua walianza kujenga taifa lao upya,Taifa lililojengwa upya liliweza kuitwa Israel au Yuda...
 
Back
Top Bottom