Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,891
Watu walichukuliwa utumwani ni Wayahudi na sio Waisraeli,hivyo wakina Ezra na Nehemia walijenga taifa la Yuda na sio Israeli na ndio maana wakati Yesu anakuja hakukuta Taifa linaloitwa Israeli bali YudaYuda ndio Israel sasa, Ukirejea kipindi cha Waajemi baada ya kuwaruhusu Wayahudi walirudi kwao lakini walikuwa chini ya utawala wa Waajemi, waliunganikana hakukuwa na tofauti kati ya watu wa Kaskazini na Kusini kwa maana ya mgawanyiko. Taifa lililojengwa upya liliweza kuitwa Israel au Yuda, kwasababu lilikuwa maendelezi ya kweli ya Israel ya kale...
Ingawa wengi walikuwa watu wa Yuda... Labda nikuulize swali, kina Ezra na Nehemia walijenga Taifa lipi!? Halafu hao Wayuda (Wayahudi) ndio waliweza kusimama katika mstari na misingi, kipindi cha Israel imegawanyika mji mkuu wa Israel ulikuwa Shekemu baadae Tirza halafu tena Samaria mpaka mwisho wa Ufalme wa Israel, Yuda yenyewe mji mkuu wake ulikuwa Yerusalemu
Pamoja na hayo makabila yaliyokuwa yanaunda taifa la Yuda yalikuwa mawili tu ambayo i Yuda na Benjamini hivyo makabila mengine kama Manase,Lawi na mengine hayakuwepo na hayajulikani yalikuwa yamekwenda wapi
Wakati Wayahudi wanachukuliwa utumwani na Wababeli,Waisraeli walikuwa wameshavamiwa na Waashuru kitambi sana
Akina Nehemia walijenga nchi ya Yuda na hakukuwa na yale makabila 10 wakati huo hadi Yesu anakuja!Halafu kipindi Yeroboamu anaongoza Israel dini yake iliunganisha na desturi za kikanaani na za Israel, halafu si walikuwa wamejitenga na Ufalme wa Yuda kwa hiyo hawakuweza kwenda kuabudu Yerusalemu lilipokuwa hekalu... Yeroboamu alijenga madhababhu mjini Dani, kukata stori...
Kama nilivyoeleza hapo mwanzo kina Ezra na Nehemia walipokuja kujenga tena hapakuwa na tofauti za mgawanyiko japokuwa wengi walikuwa Wayahudi, chini ya uongozi wa Zerubabeli na kuhani mkuu Yoshua walianza kujenga taifa lao upya,Taifa lililojengwa upya liliweza kuitwa Israel au Yuda...