Ma-expert wa bible msaada kidogo kunifafanulia hili

Yuda ndio Israel sasa, Ukirejea kipindi cha Waajemi baada ya kuwaruhusu Wayahudi walirudi kwao lakini walikuwa chini ya utawala wa Waajemi, waliunganikana hakukuwa na tofauti kati ya watu wa Kaskazini na Kusini kwa maana ya mgawanyiko. Taifa lililojengwa upya liliweza kuitwa Israel au Yuda, kwasababu lilikuwa maendelezi ya kweli ya Israel ya kale...

Ingawa wengi walikuwa watu wa Yuda... Labda nikuulize swali, kina Ezra na Nehemia walijenga Taifa lipi!? Halafu hao Wayuda (Wayahudi) ndio waliweza kusimama katika mstari na misingi, kipindi cha Israel imegawanyika mji mkuu wa Israel ulikuwa Shekemu baadae Tirza halafu tena Samaria mpaka mwisho wa Ufalme wa Israel, Yuda yenyewe mji mkuu wake ulikuwa Yerusalemu
Watu walichukuliwa utumwani ni Wayahudi na sio Waisraeli,hivyo wakina Ezra na Nehemia walijenga taifa la Yuda na sio Israeli na ndio maana wakati Yesu anakuja hakukuta Taifa linaloitwa Israeli bali Yuda

Pamoja na hayo makabila yaliyokuwa yanaunda taifa la Yuda yalikuwa mawili tu ambayo i Yuda na Benjamini hivyo makabila mengine kama Manase,Lawi na mengine hayakuwepo na hayajulikani yalikuwa yamekwenda wapi

Wakati Wayahudi wanachukuliwa utumwani na Wababeli,Waisraeli walikuwa wameshavamiwa na Waashuru kitambi sana
Halafu kipindi Yeroboamu anaongoza Israel dini yake iliunganisha na desturi za kikanaani na za Israel, halafu si walikuwa wamejitenga na Ufalme wa Yuda kwa hiyo hawakuweza kwenda kuabudu Yerusalemu lilipokuwa hekalu... Yeroboamu alijenga madhababhu mjini Dani, kukata stori...

Kama nilivyoeleza hapo mwanzo kina Ezra na Nehemia walipokuja kujenga tena hapakuwa na tofauti za mgawanyiko japokuwa wengi walikuwa Wayahudi, chini ya uongozi wa Zerubabeli na kuhani mkuu Yoshua walianza kujenga taifa lao upya,Taifa lililojengwa upya liliweza kuitwa Israel au Yuda...
Akina Nehemia walijenga nchi ya Yuda na hakukuwa na yale makabila 10 wakati huo hadi Yesu anakuja!
 
Tunapoja jadiri mambo km haya hasa kwa madai mazito kwamba kuna vitu Yesu alibadirisha ni vema tukaambatanisha na ushahidi wa kimaandiko kabisa.

Kuacha kutoa hukumu (adhabu) ya kupigwa mawe hadi kufa...

Yohana 08 : 01 - 11 inasema .......

1 [Walikwenda kila mtu nyumbani kwake; naye Yesu akaenda mpaka mlima wa Mizeituni.
2 Hata asubuhi kulipokucha akaingia tena hekaluni, na watu wote wakamwendea; naye akaketi, akawa akiwafundisha.
3 Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati.
4 Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini.
5 Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje?
6 Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi.
7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.
8 Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi.
9 Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati.
10 Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?
11 Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.]
 
Watu walichukuliwa utumwani ni Wayahudi na sio Waisraeli,hivyo wakina Ezra na Nehemia walijenga taifa la Yuda na sio Israeli na ndio maana wakati Yesu anakuja hakukuta Taifa linaloitwa Israeli bali Yuda

Pamoja na hayo makabila yaliyokuwa yanaunda taifa la Yuda yalikuwa mawili tu ambayo i Yuda na Benjamini hivyo makabila mengine kama Manase,Lawi na mengine hayakuwepo na hayajulikani yalikuwa yamekwenda wapi

Wakati Wayahudi wanachukuliwa utumwani na Wababeli,Waisraeli walikuwa wameshavamiwa na Waashuru kitambi sana

Akina Nehemia walijenga nchi ya Yuda na hakukuwa na yale makabila 10 wakati huo hadi Yesu anakuja!
Mungu aliuangamiza ufalme wa Israel 2 Wafalme 17:7-8

2 Wafalme 17:8 Kwa hiyo Bwana akawaghadhibikia Israeli sana, akawahamisha mbali na uso wake; wala hapana aliyesalia ila kabila ya Yuda peke yake.

Amosi 7:8-11

Amosi 7:11 Kwa maana Amosi asema hivi, Yeroboamu atakufa kwa upanga, na bila shaka Israeli atachukuliwa mbali, hali ya kufungwa, atoke katika nchi yake.

Na hayo yalifanyika baada ya Waashuru walipoteka ufalme wa kaskazini na kuwapeleka wenyeji wake kifungoni Uashuru ( 2 Wafalme 17:5-6)

Baada ya hapo ndio ufalme wa Israel ulipokoma ambapo walikuwa wamekwisha tawala wafalme 19 kati ya hao wote hakuna aliyempendeza Mungu, Waashuru walileta watu wao pale Israel baadae kuchanganyikana na wale wa Israel wachache waliokuwepo pale ndio Wakapatikana Wasamaria (2 Wafalme 17:24-33)

Mkuu nimekuelewa point yako, Ya kuwa hakukuwa na nchi ya Israel ila kulikuwa na nchi ya Yuda kipindi cha Yesu...

Mkuu Yale makabila 10 yalichanganyikana na mataifa mengine...

Mkuu kama hayapo yale makabila 10, iweje kwenye kitabu cha ufunuo yametajwa makabila yote 12!?

Lakini mkuu, Yuda ni subset ya Israel, kwa hiyo sio vibaya kuiita Israel kama mengine hayapo, halafu kwani Yuda walivyotoka utumwani hawakuweza kutawala maeneo yote ya Israel!?
 
Eiyer hebu angalia hizi verse hapa chini...

Matendo ya Mitume 21:28 wakapiga kelele, na kusema, Enyi wanaume wa Israeli, tusaidieni. Huyu ndiye mtu yule afundishaye watu wote kila mahali kinyume cha taifa letu na torati na mahali hapa. Tena, zaidi ya haya, amewaingiza Wayunani katika hekalu, akapatia unajisi mahali hapa patakatifu.

Wafilipi 3:5 Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo,

Hapo kwenye hizo verse wanaposema Taifa la Israel wana refer nini!? kwasababu umesema taifa la Israel halikuwepo kipindi hicho... Hauoni kwamba maelezo yangu ya kusema Yuda=Israel kwa jina jingine hiyo nchi hayana kosa!?
 
Last edited by a moderator:

Mkuu,unabii hausemi kuwa Waisraeli watachanganyika bali watachukuliwa mateka,nani aliwachukua mateka?

Wasamaria sio mchanganyiko wa Waisraeli na Waashuru bali ni wale wale Waashuru tu lakini walibadilika jina kwasababu za kimazingira tu

Ni sawa na Wakikuyu na Wachaga wa Rombo au Waganda na Wahaya,lugha inabadilika kwasababu za kimazingira na eneo lakini watu wanakuwa na asili ile ile

Sikusema kuwa yale makabila hayapo ila kwa binadamu tulioko leo hatujui kwa hakika walipo na hapa ndipo ile hoja ya Wickama inapokuja,kuwepo kwenye Ufunuo ni ushahidi kuwa hawa watu wapo na inawezekana wanajulikana ila tu watu wanaojua hayo hawataki kusema ni akina nani kwasababu zao wenyewe

Huwezi kusema kuwa ni sawa kuiita Yuda Israeli kwasababu kuna tofauti kubwa japokuwa Yuda ilikuwa ni sehemu ya Israeli
 
Last edited by a moderator:
Eiyer hebu angalia hizi verse hapa chini...

Matendo ya Mitume 21:28 wakapiga kelele, na kusema, Enyi wanaume wa Israeli, tusaidieni. Huyu ndiye mtu yule afundishaye watu wote kila mahali kinyume cha taifa letu na torati na mahali hapa. Tena, zaidi ya haya, amewaingiza Wayunani katika hekalu, akapatia unajisi mahali hapa patakatifu.

Wafilipi 3:5 Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo,

Hapo kwenye hizo verse wanaposema Taifa la Israel wana refer nini!? kwasababu umesema taifa la Israel halikuwepo kipindi hicho... Hauoni kwamba maelezo yangu ya kusema Yuda=Israel kwa jina jingine hiyo nchi hayana kosa!?

Kwanza kihistoria ni kweli kuwa taifa hili halikuwepo kabisa,hilo liko wazi

Hapo wanaposema Israeli wanarejea "familia" ya Yakobo na sio nchi!
 
Hebu soma tena hii verse

Wafilipi 3:5 Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo,

Sasa hilo taifa la Israel litakuwa familia kivipi!? Hapo Paulo alikuwa ana refer Taifa lipi!?
 
Mkuu,wakati Waisraeli walipokuwa Misri walikuwa ni taifa lakini hiyo haimaanishi kuwa hawakuwa sio familia ya Yakobo

Kwasababu wakati huo hakukuwa na nchi yenye jina hilo,basi moja kwa moja ni wazi kuwa Paulo aliposema hayo alikuwa anarejea taifa ambalo ni familia ya Yakobo!
 
Sasa kwanini kwa sasa wasiite nchi ya Yuda!?
 
Hilo swali wanapaswa kulijibu waliochagua kuiita nchi hiyo Israeli .....!!

Sasa katika ile mada ya Rabi Leo Baeck, wale jamaa waliopo pale ni kweli wanaweza wakawa ni Wayahudi... wale wa Wickama labda wanaweza wakawa ni yale makabila kumi yaliyopotoea... mkuu unaweza jikuta wewe ni Mlawi hahahahah...
 
Last edited by a moderator:
Sasa katika ile mada ya Rabi Leo Baeck, wale jamaa waliopo pale ni kweli wanaweza wakawa ni Wayahudi... wale wa Wickama labda wanaweza wakawa ni yale makabila kumi yaliyopotoea... mkuu unaweza jikuta wewe ni Mlawi hahahahah...

Inawezekana au isiwezekane wale wakawa sio Wayahudi kwasababu za kihistoria kwasababu kabila la Benjamini linaonekana walikuwa Weusi,rejea namna Paulo walivyomfananisha na Wamisri....

Mkuu,inawezekana na wewe ukawa ni Mreubeni ...hahahahaa!!!!
 
Hebu soma tena hii verse

Wafilipi 3:5 Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo,

Sasa hilo taifa la Israel litakuwa familia kivipi!? Hapo Paulo alikuwa ana refer Taifa lipi!?

Mfano, yaani kama;
Eiyer, ni wa taifa la Tanzania wa kabila la Wasukuma, Mnyantuzu wa Wanyantuzu
 
Last edited by a moderator:
Inawezekana au isiwezekane wale wakawa sio Wayahudi kwasababu za kihistoria kwasababu kabila la Benjamini linaonekana walikuwa Weusi,rejea namna Paulo walivyomfananisha na Wamisri....

Mkuu,inawezekana na wewe ukawa ni Mreubeni ...hahahahaa!!!!
Hahahahahahah, Mkuu nimesoma sehemu eti wale wa Igbo wa Nigeria wana asili ya Waisrael kutoka katika yale makabila kumi yaliyopotea... kuna madai mengi mengi sana mkuu... hebu cheki hizi verse hapa chini

Ezekiel 37:16-17

16 Na wewe mwanadamu, twaa kijiti kimoja; ukaandike juu yake, Kwa Yuda, na kwa wana wa Israeli wenzake; kisha, twaa kijiti cha pili; ukaandike juu yake, Kwa Yusufu, kijiti cha Efraimu, na kwa nyumba yote ya Israeli wenzake;
17 ukaviunge pamoja kwa ajili yako hiki na hiki viwe kijiti kimoja, viwe kimoja katika mkono wako.
 
Mkuu unajua inawezekana kabisa hii kitu japokuwa inaonekana kama ni kituko lakini ndio hivyo!
 
Nataka kujua maana ya hayo maneno katika huo mstari.

Ili kuweza kujua maana ya hayo maneno unatakiwa ujue context nzima ya tukio ambalo lilisababisha akasema hayo,kwa maana hiyo unapaswa kuweka paragraph nzima ili tulitazame tukio hilo

Ukitafsiri kijimstari tu unaweza kutokuelewa context!
 
Mfano, yaani kama;
Eiyer, ni wa taifa la Tanzania wa kabila la Wasukuma, Mnyantuzu wa Wanyantuzu

Halafu mkuu niliwahi kukuuliza kama kuna mahusiano wa yale majina ya Aikaeli,Pendaeli na Anaeli pamoja na akina Michaeli,Raphaeli na Israeli ....!!
 
Ili kuweza kujua maana ya hayo maneno unatakiwa ujue context nzima ya tukio ambalo lilisababisha akasema hayo,kwa maana hiyo unapaswa kuweka paragraph nzima ili tulitazame tukio hilo

Ukitafsiri kijimstari tu unaweza kutokuelewa context!

Mi nachotaka ni kujua maana ya hayo maneno,sasa wewe ndiyo utajua ni jinsi gani ya kunielewesha ili nipate tafsiri sahihi ya hayo maneno.
 
Back
Top Bottom