Extrovert
JF-Expert Member
- Feb 29, 2016
- 70,785
- 186,690
Hahahaha kijana we ulikuwa ni kama kenge kwenye huo msafara wa mamba!Hahahah me CHUO nilipata Gentlemen
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahahaha kijana we ulikuwa ni kama kenge kwenye huo msafara wa mamba!Hahahah me CHUO nilipata Gentlemen
Mkuu usiforce mkundu kutafuna muwaMm najiona ndio gwiji dunian Hgl division 1-8 bila walimu+ chakula kibaya+shule mbaya. Hapo akina Chegere wenu hawaniwezi. Ninge compete nao kwenye mazingira sawa, Nina uhakika ningewaburuza sana.
Noma sana enzi hizo nilifanikiwa kusalimiana na vipanga hawa kuna mjusi mmoja anaitwa ndege ulaya hivi huyu mdudu unampata...blazaKuna matukio fulani hutokea kwa namna pekee ya kushangaza na mengine huwa ya kufurahisaha zaidi hasa katika jukwaa letu hili pendwa la ELIMU.
Napenda sana kuhudhuria jukwaa hili na ' ITAPENDEZA ' nikiitwa ' MASTER WA JUKWAA LA ELIMU '
Sasa leo nawakumbushia tu historia ya T.O Maarufu zaidi "GWAMAKA NGOBELO" wa MZUMBE SPECIAL SCHOOL na "JAMALI JUMA aka BABU wa FEZA BOYS au AZANIA au ukipenda ITA Azaboys " walipokutana kwa wakati tofauti na KISIKI katika somo la PURE MATHEMATICS aitwaye 'SILVESTER'
Tukubali tukatae ila kuna watu katika ULIMWENGU huu wamebarikiwa sana kuwa na akili,pamoja na hivyo akili za VICHWA hivi viwili kwa nyakati TOFAUTI walijikuta wakimpigia SALUTE Silvester wa KIBAHA kwa kusema 'Kwa Mathematics sikuwezi'.
Bila shaka humu JamiiForums wapo watu waliosoma KIBAHA au waliofanya EZERB form 6 mwaka 2012 na wakasikia JINA Silvester hivyo wanaweza kuthibitisha hiki ninachokisema hapa.
STORY INAANZIA MWAKA 2009
Tuanzie Azania High School mwaka 2009 alitokea mwanafunzi mmoja aliyeteka sana attention kielimu katika Jiji la Dar es Salaam kwa wakati huo akijulikana kama JAMALI JUMA.Wengi tuliosoma DSM miaka hiyo sio rahisi kulikumbuka JINA hilo la JAMALI JUMA ila tutamkumbuka mwanafunzi huyo huyo kwa jina la BABU.Jamaa alifanya maajabu katika mtihani wa TAHOSA Form 4 baada ya kunyuka "A" 7 na kupata div 1.7 na kuwa "BEST STUDENT" wa DSM katika mtihani huo huku akiwaacha mbali VIPANGA wa FEDHA wakibaki wanashangaa kuwa Kijana wa AZANIA anayelipa ADA ya elfu 20 tu akionyesha maajabu mbele ya Mamilioni yaliyojaa Fedha kutokana na ADA za wanafunzi.
Jamali Juma aka BABU alikuwa very talented,na alikuwa very very very talented katika somo la MATHEMATICS.Wanafunzi wote wa AZANIA na DSM kwa ujumla waliamini kuwa sasa ENZI za Azania kutoa T.O tena zimerudi hivyo.Shule ya AZANIA ilikuwa na wakali wengi sana KIPINDI hicho ambao walifichwa ndani ya KIVULI cha JAMAL JUMA aka BABU.
Babu pamoja na kuwa alikuwa na uwezo mkubwa sana darasani ila alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanafunzi wote wa AZANIA olev wanakuwa katika hali nzuri hivyo akaanza kupita darasani kuwafundisha wanafunzi mada ambazo walikuwa hawazielewi kabisa katika masomo yote kuanzia PHYSICS mpaka wale wazee wa kusoma kama wanasoma "GAZETI"(Hahahahah hili bifu nalibeba).Hakika babu alikuwa ni MFANO mzuri wa kuigwa(Wa Azania ni mashahidi).
Maisha yaliendelea mpaka matokeo ya Form 4,2009 yalipotoka ambapo T.O wetu wa DSM ahakuamini macho yake akijikuta ameangukia PUA na kuambulia DIV 1.10 kwa matokeo haya
View attachment 653653
Jamali Juma aka BABU akapangwa MZUMBE akasome PCM class ambalo atakuwemo T.O(hahahahah) anayeitwa GWAMAKA NJOBELO.
Story ya huyu GWAMAKA NJOBELO aliyekuwa wapili kitaifa naisummarize katika mtokeo yake haya
View attachment 653654
STORY YA MWAKA 2009 ikaishia hapo
Baada ya shule za Advance Kufunguliwa hatimaye SHULE YA "FEZA BOYS" ikafanikiwa kumshawishi JAMLI JUMA akajiunga FEZA na maisha ya ADVANCE yakawa na changamoto nyingi sana kwake hasa ALIPOJIKUTA kwenye KIVULI cha jamaa aliyeingia TOP 10 Wakiwa FORM 4 Zawadi Mdoe ambaye yeye hana kitu chochote anachokifiria zaidi ya KUWA T.O
===
TURUDI KIBAHA HIGH SCHOOL
Alilipoti mwanafunzi aliyekuwa na marks za kawaida tu OLEV aliyeitwa SILVESTER.Silvester alikuwa ni mwanafunzi ambaye 'ANAJUA ' mathematics kuliko mwanafunzi yeyote TANZANIA kipindi hiko,hivyo kwa kujiamini kabisa akatangaza kuwa hakuna MTU ALIYENIPITA Additional Math na Basic Math Olevel japo Sikuwa T.O ila Hakuna wa kushindana na mimi katika mtihani wa MATHEMATICS wowote.Silvester alinikuliwa akisema hata mwalimu wa KIBAHA nafahamu kabisa kuwa haniwezi math(Hahahaha).
Wanafunzi waliotoka MZUMBE na AZANIA Olev wakaenda KIBAHA wakmwambia "Sikia Silvester,wote tunajua hapa KIBAH kuwa wewe ndio MCHAWI wa namba ila kuna vichwa VIWILI huwezi shindana navyo kabisa ambao ni Jamal Juma aka BABU wa FEZA na GWAMAKA wa Mzumbe maana jamaa wakiliona tu swali wanaona mpaka mwisho wake".Silvester akawajibu simple tu naomba LIGI nao ya MATH tu niwathibitishie tu kuwa Tz Hii hakuna ZAIDI yangu katika Somo hili...Hahahah jamaa akatania kuwa "haya mambo yana wenyewe na wenyewe ndio sisi"
Haikuchukua mda mrefu hatimaye taarifa zikatua MZUMBE kwa MA-TOs kuwa kuna dharau huko KIBAHA hivyo wanahitajika KWENDA KIBAHA kuwasha MOTO.Hahahah wanafunzi wa MZUMBE hawakuwa na presha na SILVESTER maana walikuwa wanafahamu kuwa MZUMBE na KIBAHA wanafanya mtihani mmoja wa MOCK(ezeb) hivyo mwambieni ajiandae vizuri tunakuja kuwasha MOTO.
=====
Hatimaye taarifa zikatumwa kwa BABU aka MCHAWI wa MATH DSM akitokea FEZA na kuamua kuwa YUPO tayari kufanya MTIHANI na SILVESTER Jangwani Sec kwa Manyirizu kama atakuwa tayari.
Kilia jumamosi BABU akawa anaenda kujipima KWA Manyirizu kumsubili SILVESTER,na wakati huo huo SILVESTER anachati tu kwa simu yake akimsubiri BABU siku itakapo fika akaonyeshe kuwa Tz hii hakuna kama yeye katika math.
Siku ilipofika wanafunzi wa KIBAHA waliosoma na BABU Azania wakampigia simu kumwambia nasi tutakuja kufanya mtihani kwa manyilizu hivyo KIBAHA BOYS itahamia JANGWANI GIRLS.Vijana wa KIBAHA wakatimba KWA MANYIRIZU huku Babu akiwa hayupo na walipomtafuta kwenye simu hakupatikana kabisa.Hii tunaitwa "Jamaa alikimbia "..
Vijana wa KIBAHA BOYS wakafanya mtihani na kuondoka na "A" zao huku vilaza wengine wa DSM wakaambulia C na B..
Kama kawaida,week iliyofuata BABU akaripoti kituo cha mtihani JANGWANI kujipima(Hii tunaita unaangalia kwanza usalama then unaenda) na akawa kama anasukuma WALEVI baada ya SPECIAL SCHOOL NIGGAS kuondoka.
Baada ya weeks 3 babu akatoa sababu mbali mbali za msingi za kutoweza kufika siku ile kujipima hivyo akawaomba waje tena awawashie moto..
VIJANA WA KIBAHA wakwambia SILVESTER ajiaandae kesho(Ijumaa) waondoke watafikia HOSTEL za Azania na watamlipia nauli ya kwenda na kurudi na hela ya kula.Jeshi la watu 19 walitoka KIBAHA wakiongoza na SILVESTER kwenda Azania ila katika kundi hili la watu 19 atakayefanya mtihani ni mmoja tu,yaani wengine ni wapambe tu(Hahahahah wanafunzi bhana).
Baada kufika BABU na SILVESTER wakaingia CHUMBA cha mtihani huku nje vijana wa KIBAHA BOYS wanabadilishana mawazo na JANGWANI Dadaz waliokuwepo hapo(Yani vijana wakapata vitonga)..
Baada ya kutoka CHUMBA cha mtihana wote SILVESTESTER na BABU walikuwa na FURAHA kuonyesha kila mmoja anajiamini kuwa HAKUNA wa kumzuia kuwa wa kwanza.
MATOKEO YALIPOBANDIKWA
Matokeo yalionyesha kama ifuatavyo:
1.SILVESTER aliyepata 100%
2.BABU aliyepata 99% na
3.Said aka MSELEM wa Azania aliyepata 71%
Na huo ndio ukawa mwisho wa UBISHI wa Babu na SILVESTER .Kama ilivyo desturi ya MANYIRIZU ambapo MTU anayekuwa wa KWANZA atafanya mtihani ujao bure hivyo nafasi hii ikaangukia kwa SILVESTER amabaye hatokuwepo DAR hivyo akaamwambia MANYIRIZU kuwa nafasi hiyo ampe BABU na manyirizu akafanya hivyo.
VIJANA WA KIBAHA BOYS WAKAONDOKA NA USHINDI
=====
Habari zikafika MZUMBE ambapo ilikuwa ni weeks mbili kabla ya MOCK aka EZEB.Vijana wa MZUMBE wakaongeza moto zaidi kujiandaa na EZEB wakijua kuwa KUTAKUWA na SILVESTER.
MATOKEO YA EZEB YALIKUWA KAMA IFUATAVYO:
Best Student overall alitoka MZUMBE anayeitwa GWAMAKA NJOBELO akipata 1.3 PCM huku akiwa na A ZOTE PCM
NOTE:Silvester alikuwa na Div 1.5 hivyo hakuingia hata TOP 20
=====
TOUGH TIMES NEVER PAST BUT TOUGH PEOPLE DO
DEADBODY
Umejuaje?Kisha akawa Lipumbavu.
Uyo martin anafuatilia ata Mpira kweli..?manake izo sifa sasa...inaonyesha namba Moja ndo tabia take kuanzia vidudu had I phdmartin chegere kaongoza darasa la 7 taifa wakati anasoma ukonga.Akachaguliwa kibaha hakwenda,akaenda maua seminary akawa t.o o lev,akaenda pugu advance akawa t.o,akaend udsm bachelor akaongoza,masterz udsm akaongoza,akaenda Phd sweden akaongoza.
karudi ud anafundisha.
Ila tofouti na kukamia ila jamaa yuko so talented n humble.... Nadhani muda si mredu ataanza kula mema ya nchi juzi kati alikuwa U.S.A for 3 months kuna meeting fulani alienda na ma prof taratibu fursa zinamfuata jamaa....mkuu tatizo vijaa hukamia sana.....
G hakuwahi kusoma mchikichini wala kwa logman. Kilichokua kinambeba Babu ni sifa sifa tu ambazo watu walikua wanampa, Azania kwenyew paper ya form 2 alipitwa, kuna watu walikua very smart ila hawana kelele, ila huyo Babu alikua anapigiwa kelele nyingi sana.. Paper ya form ya hesbu nakumbuka alipata 99..mm nilipata 97 lakini hzo sifa alzokua anapewa zilikua too much, G was the best jamaa yupo cool.. No wonder ametoka na first class ya civil engineering ya CoeT udsmHahaha
ule ubishi pale Mchikichini kwa Moody Physics kwa hawa jamaa ilikuwa hatari.
Huyo Babu na Gwamaka walikuwa wanasoma namba kwa jamaa mmoja anaitwa Log,
Ilikuwa hatari
na muda mwingi ni mtu wa muv, gem nkUyo martin anafuatilia ata Mpira kweli..?manake izo sifa sasa...inaonyesha namba Moja ndo tabia take kuanzia vidudu had I phd
Umejuaje?
yah vijana wa pale wengi ni unique na pia hawawabanii wenzao fursa ndo maana kama mtu akiwa yuko nje ikatokea nafasi au competition bas huileta pale kibaha straight kwa madogo!!!!!! mfano kuna jamaa alikua yuko oxford univ..sasa kulikua kuna competition ya kuandika idea flani ya ubunifu na winner kuchukua usd 1000( kwa viwango vya enzi zile) basi jamaa akaipeleka kwa madogo th madog wakawin...Ila tofouti na kukamia ila jamaa yuko so talented n humble.... Nadhani muda si mredu ataanza kula mema ya nchi juzi kati alikuwa U.S.A for 3 months kuna meeting fulani alienda na ma prof taratibu fursa zinamfuata jamaa....
OLEV 2009 iMMACULTE ALIKUWA WA KWANZA na FAITH akawa wa 7 .
ALEV FAITH akawa wa kwanza na IMMACULATE akawa wa 5
Mpaka bangi nyeusi walikuwa wanavutaHuu uzi mtaamu saana hivi hao washikaji kweli walikua na mademu? Au wanafuatilia Mpira na misele mingine
Haina madhara hiyo sema daah washikaji walibarikiwa aloo... ss wengine wasindikizajiMpaka bangi nyeusi walikuwa wanavuta
Hongera yaoBabu anasoma MASTERS