Maadhimisho na Kilele cha Usomaji Quran kufanyika Siku ya Pasaka ni Dharau na Uchokozi kwa Wakristo au ni Utaratibu tu?

Maadhimisho na Kilele cha Usomaji Quran kufanyika Siku ya Pasaka ni Dharau na Uchokozi kwa Wakristo au ni Utaratibu tu?

Mimi nimekaa na waislamu miaka mingi Sana, ninachoweza kusema Ni kwamba waislamu Wanapenda kushindana na wakristo ilhali wakristo hawana time ya kushindana na waislamu.

Sehemu niliyokaa, siku za sikukuu za kikristo lazima hiyo siku waislamu wafunge barabara kufanya maadhimisho ya siku zao. Utakuta mtaa mzima wamefunga taa usiku na vitambaa vinapepea barabara zote. Lakini unakuta baada ya ile jumapili kupita, Jumapili inayofuata wanakuwa hawana kabisa utaratibu wa kufanya shughuli kama ile hadi unabaki kujiuliza sasa waislamu kwa nini ile Jumapili wasingewaacha wenzao wakasherekea sikukuu yao vizuri kisha wao (waislamu) wakaadhimisha hiyo siku yao Jumapili ya leo?

Miaka ya mwanzo kuishi nao nilidhani ni coincidence wanapofanya hili swala la kufunga mitaa siku za sikukuu za kikristo ili nao washerekee siku zao. Ila baadae nikaja kugundua lengo lao ni kuzima sikukuu za Kikristo zisisikike kabisa. Sijui kwa nini wale jamaa walikuwa washari kiasi kile!
 
Na nimeona katika Tangazo lao Kubwa kuwa Mgeni rasmi atakuwa ni Muislamu Mwenzao Rais Samia Suluhu Hassan na litafanyika tarehe 9 April, 2023 ambayo Wakristo wote akina GENTAMYCINE ( Zanaki and Makuwa Think Tank ) ndiyo tutakuwa tunesheherekea Siku Kuu yetu Muhimu na Kubwa ya Pasaka ( Kufufuka kwa Mkombozi Wetu ) Yesu Kristo.

Nimekaa pale sasa tayari kusubiria Majibu yenu na pia Kusoma Maoni yenu kama Great Thinkers hapa JamiiForums.

Endeleeni kutafuta Watu ubaya Oky?
Huu ni ukorofi aiseee Sasa taifa pale sisi tutaenda kupiga show mchana ya kumsifu Yesukristo
 
Wakristo huwa hatuna shida maana Mungu wetu ni Mkubwa.
Hao wengine ni wadhaifu sana

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Hii hoja yako imepitwa na wakati mkuu.

Watu dhaifu Kama wewe ndiyo mmefanya ukristo kuonekana laini laini wakati kiuhalisia ukristo hauko hivyo.

Hili swala ni la kuhoji Kama alivyofanya mleta mada, maana limekuwa sugu. Maana ingekuwa ni mara moja tu ungesema aah wacha tu lipite. Unadhani ingekuwa wakristo ndiyo wanafanya sherehe zao siku ya sikukuu za kiislamu wao wangekaa kimya na kusema tunamwachia Mungu kama alivyofanya wewe mkuu?
 
Na nimeona katika Tangazo lao Kubwa kuwa Mgeni rasmi atakuwa ni Muislamu Mwenzao Rais Samia Suluhu Hassan na litafanyika tarehe 9 April, 2023 ambayo Wakristo wote akina GENTAMYCINE ( Zanaki and Makuwa Think Tank ) ndiyo tutakuwa tunesheherekea Siku Kuu yetu Muhimu na Kubwa ya Pasaka ( Kufufuka kwa Mkombozi Wetu ) Yesu Kristo.

Nimekaa pale sasa tayari kusubiria Majibu yenu na pia Kusoma Maoni yenu kama Great Thinkers hapa JamiiForums.

Endeleeni kutafuta Watu ubaya Oky?
Aiseee!!!...ingekuwaje sikukuu ya Eid el Fitr iangukie JUMAPILI au Siku ambayo wakristo wamepanga kutekeleza tukio lao,Inamaana mambo mengine yangepaswa kusimama au kutofanyika kabisa kisa tu kuna dini nyingine imeandaa tukio lao?...nadhani unapaswa kutafakari vyema kabla ya kuleta hiki unachoona kama "ushindani"usio namaana wala mustakabali mzuri kwa Watanzania na Nchi kwa ujumla.
 
Uko sahihi pwani na wakristi tunaishi nao vizuri kabisa
Labda uwe specific unaongelea pwani gani mkuu. Ila Kama ni pwani ya Tanga, Dar, Zanzibar, Lindi na Mtwara kwa maoni yangu ni vile tu wakristo wameamua kuwa wapole ilakama wangekuwa wanapenda kushindana, mambo yasingekuwa kama ulivyosema.

Nakumbuka miaka mitatu iliyopita Mkuu wa mkoa wa Lindi na shehe wa mkoa walienda shule Mahiwa (mahiwa high school) kusuluhisha mgogoro wanafunzi wa kiislamu walikuwa hawataki kuchangia vitu vyao na watoto wa kikristo, na shule ilikuwa wanalazimisha iwe na ratiba kama shule ya kiislamu.

Serikali ilimaliza mgogoro kwa kuwajengea msikiti mkubwa nje kidogo ya shule na kuna ambao walifukuzwa kwa kuleta misimamo mikali. Hapo hatujaongelea matukio ya Zanzibar, Kilwa na sehemu zingine zenye waislamu wengi kama Newala na Tandahimba jinsi wasio waislamu wanavyopata shida ila wanaamua kukubalinana na matokeo.

Masasi ndiyo hakuna maswala ya udini kwa kule Kusini.
 
,ili jumapili hii ya pasaka waheshimu wenzao wakristo washerekee sikukuu yao ambayo waliisubiria kwa siku 40(kwaresma


Hivi unataka kusema Waisilamu kufanya siku hiyo kuwa kilele cha usomaji wa Qur'an ni kuivunjia heshima Sikukuu ya Pasaka?!!😏

Kama maana yako ni hiyo Hebu fafanua inakuaje mambo ya Uisilamu (kusama Qur'an) ivunje heshima ya Pasaka??
 
Huu ndio ukweli, hakuna familia Tanzania, hasa sehemu za Pwani, zisizochanganyika katika uislamu na ulristo. Nimewahi pia kukuta waarabu waislamu wana undugu na wakristo.
 
Nadhani huo ni utaratibu ulioshindwa heshimu imani zingine, waandaaji walipaswa kuheshimu siku husika kwa imani nyingine haswa inapotokea kiongozi mkuu wa nchi kuwa mgeni rasmi hiyo itapelekea vyombo vingi vya habari kutupia macho alipo Mh. Rais.

Ingawa Mh. Rais utomuona akiwa kwa kanisa siku ya pasaka kutokana na misingi ya imani yake lakini Makamu wake lazima ataoneshwa kama nembo ya serikali katika kuwakilisha sikukuu hiyo ingawa itakuwa kwa uchache kwa kigezo cha habari kuelekea sana alipo Mh. Rais. Wakati ujao mambo haya yasije tokea tena tuishi kwa kuheshimiana nchi yetu sote hii.
 
Sherehe za mashindano ya Quran zinafanyika sehemu ndogo tu ya Nchi (kwenye uwanja wa taifa) ambapo pia ni masaa hayazidi saba ndani ya muda huu hata pilau linakuwa halijaiva! Na wahudhuriaji ni waislamu.

Sasa hiyo dharau hapo inakujaje ikiwa wanaohusika ni waislamu? Nyie si muendelee na mambo yenu, kwani kuna aliyewaita kuhudhuria sherehe hizo?
 
Uko sahihi pwani na wakristi tunaishi nao vizuri kabisa
Ni ndugu kabisa, wapo wakristo ndugu zao waislamu, mama wakubwa, mama wadogo, wajomba, Shangazi, baba wakubwa, baba wadogo, zipo nyumba familia moja, utakuta kuna majina ya kikristo na ya kiislamu.

Wapo mpaka waarabu kabisa, waislamu wana undugu na wakristo, na wanaishi pamoja na kutembeleana. Hiyo kwa miji ya Pwani ni kawaida kabisa.
 
Sasa hi hoja yako in Uhusiano gani na thread ya mleta mada mkuu?

Basi Kama ulishindwa kusoma kilichoandikwa si ungesoma tu tittle ungeelewa anakusudia kusema Nini?

Swali ni kwa Nini kilele Cha siku ya Quran iwe siku ya maadhimisho ya pasaka? Kwa nini wasingevuta ikawa jumapili ile nyingine, ili jumapili hii ya pasaka waheshimu wenzao wakristo washerekee sikukuu yao ambayo waliisubiria kwa siku 40(kwaresma)?

Hivyo ndivyo ilipaswa kuwa. Ni swala la ustaharaabu tu,na si kushindana.
Ndio nikamwambia atapata tabu bure, si ajabu hata wapo wakristo wamefadhili hayo mashindano, na wapo watakao hudhuria, na wengine ni viongozi wa kikristo.

Wakristo na waislamu kwa mikoa ya Pwani, hao ni ndugu, wanaishi pamoja, na kusaidiana.
 
Angalia tarehe vizuri
 

Attachments

  • IMG-20230314-WA0009.jpg
    IMG-20230314-WA0009.jpg
    82.4 KB · Views: 3
Na nimeona katika Tangazo lao Kubwa kuwa Mgeni rasmi atakuwa ni Muislamu Mwenzao Rais Samia Suluhu Hassan na litafanyika tarehe 9 April, 2023 ambayo Wakristo wote akina GENTAMYCINE ( Zanaki and Makuwa Think Tank ) ndiyo tutakuwa tunesheherekea Siku Kuu yetu Muhimu na Kubwa ya Pasaka ( Kufufuka kwa Mkombozi Wetu ) Yesu Kristo.

Nimekaa pale sasa tayari kusubiria Majibu yenu na pia Kusoma Maoni yenu kama Great Thinkers hapa JamiiForums.

Endeleeni kutafuta Watu ubaya Oky?
Hakuna mtu anayemiliki Siku! Sioni mantiki
 
Back
Top Bottom