Maadhimisho na Kilele cha Usomaji Quran kufanyika Siku ya Pasaka ni Dharau na Uchokozi kwa Wakristo au ni Utaratibu tu?

Maadhimisho na Kilele cha Usomaji Quran kufanyika Siku ya Pasaka ni Dharau na Uchokozi kwa Wakristo au ni Utaratibu tu?

Labda uwe specific unaongelea pwani gani mkuu. Ila Kama ni pwani ya Tanga, Dar, Zanzibar,Lindi na Mtwara kwa maoni yangu ni vile tu wakristo wameamua kuwa wapole ilakama wangekuwa Wanapenda kushindana,mambo yasingekuwa Kama ulivyosema.

Nakumbuka miaka mitatu iliyopita mkuu. Wa mkoa wa Lindi na shehe wa mkoa walienda shule Mahiwa (mahiwa high school) kushluhisha mgogoro wanafunzi wa kiislamu walikuwa hawataki kuchangia vitu vyao na watoto wa kikristo,na shule ilikuwa wanalazimisha I we na ratiba Kama shule ya kiislamu. Serikali ilimaliza mgogoro kwa kuwajengea msikiti mkubwa nje kidogo ya shule na Kuna ambao walifukuzwa kwa kuleta misimamo mikali. Hapo hatujaongelea matukio ya Zanzibar,Kilwa na sehemu zingine zenye waislamu wengi Kama newala na tandahimba jinsi wasio waislamu wanavyopata shida ila wanaamua kukubalinana na matokeo. Masasi ndiyo Hakuna maswala ya udini kwa kule kusini.
Matukio wengi sijawahi kuona nimekaa Tanga sana na pale mtaani si mzee wangu wala waarabu wa pale Godown za Simba mtoto walikuwa wakitoa chakula kwa wote siku za Eid enzi hizo.

Nimesoma shule sijawahi kukutana na izo mambo tulikuwa tunaishi vizuri kabisa na kuheshimiani hata kupeana mialiko.

Sisi kipind tunaanza shule fulani headmaster alikuwa ni mkristo hakutaka kabisa tuende kuswali saa Saba na shule yetu ilikuwa na eneo kubwa ..Yupo mwalimu alikuwa anakituadhibu maana kipind chake ni mwisho kuanza name mpaka kutoka 8:30 na ilikuwa ni chuki tu...Pia alikuwa akiongea chuki za wazi kabisa kwa kukashfu dini yetu...


Bahati nzuri ile safu yetu matokeo ndo tulifanya poa wote na kingine alikamatwa na mtoto wa kidogo mdogo wa form 3 alimpa mimba akaozeshwa hapa sijaweka kwamba ukristo ndo umemtuma , bali ni tabia yake binafsi.

Migogor haiwezi kuepukika kwa sababu chokochoko zipo na wala tusiwe too general nimeishi Tanga kama Kuna matukio yalifanyika ya ubaguzi kabla ya mwaka 2012 niambie nimekaa pale sijawahi kuona wala nn na misikiti inayofuturisha ile mda baada ya swala wanajaa wakristo wengi waislamu wanaenda kula makwao hii ni hakika 100% maana jqmaa zangu ndo walikuwa wanaenda..

Baadhi ya madai pale shule palikuwa na kasumba siwezi kukuambia ila ni ukweli kesi moja Kuna mwanafunzi ni mpemba bhana alikuja kugombana na mwenzie bahati mbaya yule mwenzie alimsema sana akamvua hijabu yake kichwani..Siwez kuendelea ila palizuka mgogoro wa kidni mkubwa sana mpaka sisi tulikaa pembeni .
 
Labda uwe specific unaongelea pwani gani mkuu. Ila Kama ni pwani ya Tanga, Dar, Zanzibar,Lindi na Mtwara kwa maoni yangu ni vile tu wakristo wameamua kuwa wapole ilakama wangekuwa Wanapenda kushindana,mambo yasingekuwa Kama ulivyosema.

Nakumbuka miaka mitatu iliyopita mkuu. Wa mkoa wa Lindi na shehe wa mkoa walienda shule Mahiwa (mahiwa high school) kushluhisha mgogoro wanafunzi wa kiislamu walikuwa hawataki kuchangia vitu vyao na watoto wa kikristo,na shule ilikuwa wanalazimisha I we na ratiba Kama shule ya kiislamu. Serikali ilimaliza mgogoro kwa kuwajengea msikiti mkubwa nje kidogo ya shule na Kuna ambao walifukuzwa kwa kuleta misimamo mikali. Hapo hatujaongelea matukio ya Zanzibar,Kilwa na sehemu zingine zenye waislamu wengi Kama newala na tandahimba jinsi wasio waislamu wanavyopata shida ila wanaamua kukubalinana na matokeo. Masasi ndiyo Hakuna maswala ya udini kwa kule kusini.
Kwa Mimi naongea nikiwa nimefunga hapa dada yangu kaolewa na mkristo huko Kilimanjaro na anakuja nyumbani ..

Bibi yangu upareni ana ndugu kibao ni wasabato kasoro yeye tunakaa nao wanapikiwa wao tu siku za Ramadhani sisi sote tumefunga..kwa maana hyo sherehe zetu zote lazima utakuta mchanganyiko wa dini zote kwa sababu tu ukaribu na undugu kabisa.
 
Sasa hi hoja yako in Uhusiano gani na thread ya mleta mada mkuu?

Basi Kama ulishindwa kusoma kilichoandikwa si ungesoma tu tittle ungeelewa anakusudia kusema Nini?

Swali ni kwa Nini kilele Cha siku ya Quran iwe siku ya maadhimisho ya pasaka? Kwa nini wasingevuta ikawa jumapili ile nyingine,ili jumapili hii ya pasaka waheshimu wenzao wakristo washerekee sikukuu yao ambayo waliisubiria kwa siku 40(kwaresma)?

Hivyo ndivyo ilipaswa kuwa. Ni swala la ustaharaabu tu,na si kushindana.
Hiyo pasaka waislam inawahusu nn mpaka waache kufanya mambo yao kwa ajili yake?
 
Hakuna mtu anayemiliki Siku! Sioni mantiki


Ni matumizi ya siku ndio yanamilikiwa na watu.

Mleta mada alitaka siku ya pasaka Waisilamu wawaachie wakristo watese peke yao huku Waisilamu wakikodoa macho kuangalia Bwana Yesu "akifufuka" na hata kama kuna fundisho la kidini katika siku hiyo waisilamu wapate, halafu siku nyingine ndipo Waisilamu wafanye maadhimisho ya kilele cha Usomaji wa Qur'an huku Wakristo nao wajumuike au washiriki kupitia Luninga nk kusikia sauti tamu za kisomo cha Qur'an tukufu ikizingatiwa kuwa katika hafla hiyo ya kilele cha usomaji Qur'an atakuwepo Mama (Bi mkubwa) kama mgeni rasmi.

Nadhani hoja ya msingi ya huyo mtani wangu ilikuwa ipo hapo ila yeye alishindwa kuijenga ili ilete mantiki kwa wasomaji.😀😀
 
Ni matumizi ya siku ndio yanamilikiwa na watu.

Mleta mada alitaka siku ya pasaka Waisilamu wawaachie wakristo watese peke yao huku Waisilamu wakikodoa macho kuangalia Bwana Yesu "akifufuka" na hata kama kuna fundisho la kidini katika siku hiyo waisilamu wapate, halafu siku nyingine ndipo Waisilamu wafanye maadhimisho ya kilele cha Usomaji wa Qur'an huku Wakristo nao wajumuike au washiriki kupitia Luninga nk kusikia sauti tamu za kisomo cha Qur'an tukufu ikizingatiwa kuwa katika hafla hiyo ya kilele cha usomaji Qur'an atakuwepo Mama (Bi mkubwa) kama mgeni rasmi.

Nadhani hoja ya msingi ya huyo mtani wangu ilikuwa ipo hapo ila yeye alishindwa kuijenga ili ilete mantiki kwa wasomaji, si unajua watu wa kutoka Mara tena!!, [emoji3][emoji3]
Hakuna undugu wowote wa kiimani kati wa Uislam na Ukristo acheni unafiki.
Sasa waislam wasimamishe shughuli zao kwani pasaka inawahusu nn wao?

Waislam watashuhudiaje kufufuka kwa yesu wakati wao hawaamini kakita ufufuo?
Na wakristo watajumuikaje kusikiliza Qruani wakati hawaiamini?

Wakristo na waislam wana undugu mbali mbali wa damu, kikazi ,kirafiki, lakini linapo kuja suala la kiimani ni mbingu na ardhi hivyo msipende kurazimisha mambo.
 
Hivi unataka kusema Waisilamu kufanya siku hiyo kuwa kilele cha usomaji wa Qur'an ni kuivunjia heshima Sikukuu ya Pasaka?!![emoji57]

Kama maana yako ni hiyo Hebu fafanua inakuaje mambo ya Uisilamu (kusama Qur'an) ivunje heshima ya Pasaka??
Elewa post ya mleta mada na comment yangu.

Ni hivi; katika nchi ambayo Kuna watu wa imani tofauti Kuna muda busara inatakiwa itumike na si kushindana. Hii habari ya waislamu kuingilia sikukuu za wakristo na wao kujifanya wako bize kuadhimisha siku zao wakati wangeweza kuwaacha wenzao washerekee sikukuu yao Kisha wao(waislamu) wangesogeza Hadi jumapili nyingine kungekuwa na ubaya gani mkuu?

Mimi ninachosikitika ni hii hali kuifanya karibia kila mwaka. Ikifika pasaka na nyie waislamu mnaomba uwanja mnaganya maadhimisho ya Quran. Tujifunze ustaarabu kwa waislamu wa Senegal. Kule wakristo wachache 10% na waislamu 90% lakini wakristo wanaheshimiwa Sana.
 
Hii hoja yako imepitwa na wakati mkuu.

Watu dhaifu Kama wewe ndiyo mmefanya ukristo kuonekana laini laini wakati kiuhalisia ukristo hauko hivyo.

Hili swala ni la kuhoji Kama alivyofanya mleta mada,maana limekuwa sugu. Maana ingekuwa Ni Mara Moja tu ungesema aah wacha tu lipite. Unadhani ingekuwa wakristo ndiyo wanafanya sherehe zao siku ya sikukuu za kiislamu wao wangekaa kimya na kusema tunamwachia Mungu Kama alivyofanya wewe mkuu?
GENTAMYCINE hueleweka na Werevu wachache kama Wewe hapa JamiiForums ila Wapumbavu wengi hushindwa Kunielewa.

Cc: Hance Mtanashati
 
Sasa hi hoja yako in Uhusiano gani na thread ya mleta mada mkuu?

Basi Kama ulishindwa kusoma kilichoandikwa si ungesoma tu tittle ungeelewa anakusudia kusema Nini?

Swali ni kwa Nini kilele Cha siku ya Quran iwe siku ya maadhimisho ya pasaka? Kwa nini wasingevuta ikawa jumapili ile nyingine,ili jumapili hii ya pasaka waheshimu wenzao wakristo washerekee sikukuu yao ambayo waliisubiria kwa siku 40(kwaresma)?

Hivyo ndivyo ilipaswa kuwa. Ni swala la ustaharaabu tu,na si kushindana.
Huwez kuwapangia waislam siku ya kuadhimisha mashindano ya Quran.

Waliopanga hiyo tarehe walikua na sababu zao na wala sio kwa sababu unazozifkiria ww, na wala sio ushindani.

Unavosema wangevuta mbele unajua ingewagarimu kias gani? Pengine siku hyo mgeni rasmi ndo Ana nafasi, au pengine siku hyo ndo kuna nafasi ya uwanja wa kufanyia maadhimisho, au pengine kuna sababu kibao ambayo imewafanya waweke siku hiyo,

Unapozungumza jambo litafakari kwanza, usikurupuke, kuna wakati machafuko tunayatengeneza sisi wenyewe kuongea vitu vya kichochezi, ukikaa kimya jambo litapita vzr bila shida, waislam watafanya yao, na wakristo watafnya yao, kila mmoja atafurahi kwa nafasi yake. Wala waislam hawatawazuia wakristo kutosherehekea.
 
Hayo mashindano siya ya kumualika kiongozi mkuu kama mgeni rasmi. Bila shaka atatuma mwakishi wake ambaye kimsingi atakuwa waziri fulani mwenye imani hiyo. Kwanza ni makosa makubwa kuita usomaji huo eti ni mashindano.

Kwa mungu hakuna mashindano. Hiyo ni ibada kama ibada zao zingine. Halafu kuweka siku ambayo taifa litakuwa linaadhimisha sikukuu kwa waumini wa kikristo haileti maana nzuri kwa wakristo wa tanzania.

Je, kama mgeni rasmi siku hiyo ataalikwa na maaskofu kwenda kuhutubia taifa katika maadhimisho ya pasaka ataenda upande upi? Au atahutubia kotekote bila kuchoka? Hao watu wawe wanaheshimu sikukuu za taifa kama zilivyopangwa, ina maana hawajui siku za matukio ya kitaifa mpaka wapange mashindano yao siku hiyo?

Hio ni dharau na si busara na hekima.
 
Hakuna undugu wowote wa kiimani kati wa Uislam na Ukristo acheni unafiki.
Sasa waislam wasimamishe shughuli zao kwani pasaka inawahusu nn wao?

Waislam watashuhudiaje kufufuka kwa yesu wakati wao hawaamini kakita ufufuo?
Na wakristo watajumuikaje kusikiliza Qruani wakati hawaiamini?

Wakristo na waislam wana undugu mbali mbali wa damu, kikazi ,kirafiki, lakini linapo kuja suala la kiimani ni mbingu na ardhi hivyo msipende kurazimisha mambo.


Lakini Umenielewa nilichosema??!!

Labda niseme hivi; huyo mleta mada kimsingi alitaka katika siku hiyo ya Pasaka Waisilamu wangesimamisha na kuahirisha kilele cha usomaji Qur'an kwasababu katika kilele hicho mgeni Rasmi atakuwa ni Mama hivyo attention ya Waisilamu na wasiokuwa waisilamu mainly Christians itakuwepo huko na hivyo "FUNDISHO LA PASAKA" kufifia kwa kiasi kikubwa, fundisho la pasaka ni somo la kiimani na somo hilo linawahusu watu wote kwani kwa imani ya Wakristo Yesu ni mkombozi wa Ulimwengu wote hivyo kama yupo Muisilamu au mpagani ambaye kavutiwa na Ufufuko wa Yesu basi anaweza kujiunga na Ukristo, kwa upande wa pili Usomaji wa Qur'an ni tukio la kiimani na limehimizwa katika Uisilamu na Qur'an ni mafundisho kutoka kwa Mungu kwa mujibu Uisilamu nayo yanawahusu watu wote hivyo mtu akiisikiliza Qur'an anapata rehema kutoka kwa Mungu (this is according to Qur'an), na kama ni mkristo akavutiwa na Uisilamu anaweza kujiunga na Uisilamu hivyo mleta mada alikuwa na "underlying logic" ya aina hiyo isipokuwa tu alishindwa kuiweka katika muundo huo.
 
nazani huo ni utaratibu ulioshindwa heshimu imani zingine , waandaaji walipaswa kuheshimu siku husika kwa imani nyingine haswa inapotokea kiongozi mkuu wa nchi kuwa mgeni rasmi hiyo itapelekea vyombo vingi vya habari kutupia macho alipo Mh Raisi. Ingawa mh Raisi utomuona akiwa kwa kanisa siku ya pasaka kutokana na misingi ya imani yake lakini makamu wake lazima ataoneshwa kama nembo ya serikali katika kuwakilisha sikukuu hiyo ingawa itakuwa kwa uchache kwa kigezo cha habari kuelekea sana alipo Mh Raisi . Wakati ujao mambo haya yasije tokea tena tuishi kwa kuheshimiana nchi yetu sote hii.
Utashangaa kwa Akili Kubwa yako hii Uliyoandika hapa bado kuna Mijuha ( Nuts ) itakubishia tu.

Cc: Mokaze na Hance Mtanashati
 
Angalia tarehe vizuri
Mpaka Jana Usiku Mabango yote ya Barabarani juu ya hilo Tukio tarehe iliyokuwepo ni 9 April, 2023 na sasa baada ya kuona GENTAMYCINE nimewashikeni pabaya mmeamua kubadili tarehe na Venue. Hovyoooooooo....!!!!!!!

Mimi ndiyo GENTAMYCINE The King!!!!
 
Na nimeona katika Tangazo lao Kubwa kuwa Mgeni rasmi atakuwa ni Muislamu Mwenzao Rais Samia Suluhu Hassan na litafanyika tarehe 9 April, 2023 ambayo Wakristo wote akina GENTAMYCINE ( Zanaki and Makuwa Think Tank ) ndiyo tutakuwa tunesheherekea Siku Kuu yetu Muhimu na Kubwa ya Pasaka ( Kufufuka kwa Mkombozi Wetu ) Yesu Kristo.

Nimekaa pale sasa tayari kusubiria Majibu yenu na pia Kusoma Maoni yenu kama Great Thinkers hapa JamiiForums.

Endeleeni kutafuta Watu ubaya Oky?
Binafsi sioni kama Kuna tatizo..
 
Utajipa tabu bure na kujiumiza kichwa,sehemu nyingi Tanzania,hasa sehemu za Pwani,ndani ya familia moja wamechanganyika wakristo na waislamu, na wanashirikiana kwenye furaha na huzuni,usishangae kwenye mashindano ya Qur'an kukuta wa dini zote wapo.

Na mashindano yakimalizika ni saa saba,wakiondoka hapo wote kwa pamoja wanakwenda kutembea kwenye Pasaka.

Kuna wakati kulikuwa na jirani zangu ni waislamu,wakawa wamefiwa na mjukuu wao,kufika mjukuu ni mkristo na maiti imeletwa kwa babu yake muislamu,wakachanganyika waislamu na wakristo,bila kubaguana.
Stupid,yaaan umeandika utumbo .pumbavu zako
 
Binafsi sioni kama Kuna tatizo..
Hopeless kungekuwa hakuna tatizo wangebadili tarehe ya hilo Tukio lao kutoka tarehe 9 April ( Pasaka ) na sasa kuwa tarehe 2 April?
 
pasaka ni kufufuka kwa Yesu?
Mi ninavyojua pasaka ni maadhimisho ya Waisrael kutoka misri utumwani

Kutoka12:12 Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi Bwana.
13 Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri.
14 Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa Bwana; mtaifanya iwe sikukuu katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele
15 Mtakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba; siku hiyo ya kwanza mtaondoa chachu yote isiwe katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu ye yote atakayekula mkate uliochachwa tangu siku hiyo ya kwanza hata siku ya saba, nafsi hiyo atakatiliwa mbali na Israeli.
16 Siku ya kwanza kutakuwa kwenu na kusanyiko takatifu, na siku ya saba kutakuwa kusanyiko takatifu; haitafanywa kazi yo yote katika siku hizo, isipokuwa kwa hiyo ambayo kila mtu hana budi kula, hiyo tu ifanyike kwenu.
17 Nanyi mtaitunza ile sikukuu ya mikate isiyochachwa; kwa kuwa katika siku iyo hiyo mimi nimeyatoa majeshi yenu katika nchi ya Misri; kwa hiyo mtaitunza siku hiyo katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele.
18 Mwezi wa kwanza, siku ya mwezi kumi na nne, wakati wa jioni, mtakula mikate isiyochachwa, hata siku ya mwezi ishirini na moja jioni.
19 Muda wa siku saba isionekane chachu katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu ye yote atakayekula hiyo iliyotiwa chachu, nafsi hiyo atakatiliwa mbali na mkutano wa Israeli, akiwa mwenye kukaa hali ya ugeni, au akiwa mtu aliyezaliwa katika nchi.
20 Msile kitu chochote kilichochachwa; mtakula mikate isiyochachwa katika makao yenu yote.
21 Hapo ndipo Musa akawaita wazee wa Israeli, na kuwaambia, Nendeni, mkajitwalie wana-kondoo kama jamaa zenu zilivyo mkamchinje pasaka.
22 Nanyi twaeni tawi la hisopu, mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu ye yote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi.
23 Kwa kuwa Bwana atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, Bwana atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi.
24 Nanyi mtalitunza jambo hili kuwa ni amri kwako na kwa wanao milele.
25 Itakuwa hapo mtakapoifikilia hiyo nchi, Bwana atakayowapa, kama alivyoahidi, ndipo mtakapoushika utumishi huu.
26 Kisha itakuwa, hapo watoto wenu watakapowauliza, N'nini maana yake utumishi huu kwenu?
27 Ndipo mtawaambia, Ni dhabihu ya pasaka ya Bwana, kwa kuwa alipita juu ya nyumba za wana wa Israeli huko Misri, hapo alipowapiga Wamisri, akaziokoa nyumba zetu. Hao watu wakainama vichwa na kusujudia.
28 Basi wana wa Israeli wakaenda na kufanya mambo hayo; vile vile kama Bwana alivyowaamuru Musa na Haruni, ndivyo walivyofanya.
29 Hata ikawa, usiku wa manane Bwana akawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, tangu mzaliwa wa kwanza wa Farao aliyeketi katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa mtu aliyefungwa katika nyumba ya wafungwa; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama.
30 Farao akaondoka usiku, yeye na watumishi wake wote, na Wamisri wote; pakawa na kilio kikuu katika Misri; maana hapakuwa na nyumba hata moja asimokufa mtu.
Ukiongelea Israel hao ni dini ya Jewish.
Pasaka ni ya Wakristo.
 
Back
Top Bottom