Maadhimisho na Kilele cha Usomaji Quran kufanyika Siku ya Pasaka ni Dharau na Uchokozi kwa Wakristo au ni Utaratibu tu?

Maadhimisho na Kilele cha Usomaji Quran kufanyika Siku ya Pasaka ni Dharau na Uchokozi kwa Wakristo au ni Utaratibu tu?

Na nimeona katika Tangazo lao Kubwa kuwa Mgeni rasmi atakuwa ni Muislamu Mwenzao Rais Samia Suluhu Hassan na litafanyika tarehe 9 April, 2023 ambayo Wakristo wote akina GENTAMYCINE ( Zanaki and Makuwa Think Tank ) ndiyo tutakuwa tunesheherekea Siku Kuu yetu Muhimu na Kubwa ya Pasaka ( Kufufuka kwa Mkombozi Wetu ) Yesu Kristo.

Nimekaa pale sasa tayari kusubiria Majibu yenu na pia Kusoma Maoni yenu kama Great Thinkers hapa JamiiForums.

Endeleeni kutafuta Watu ubaya Oky?
Sioni dharau wala uchokozi wote. Ya waislamu yanamhusu vipi mkristo na kinyume chake? Hawaji kunibughudhi kanisani wala nyumbani kwangu na mimi siwaingilii msikitini au popote wanapofanya shughuli yao.
 
Lakini Umenielewa nilichosema??!!

Labda niseme hivi; huyo mleta mada kimsingi alitaka katika siku hiyo ya Pasaka Waisilamu wangesimamisha na kuahirisha kilele cha usomaji Qur'an kwasababu katika kilele hicho mgeni Rasmi atakuwa ni Mama hivyo attention ya Waisilamu na wasiokuwa waisilamu mainly Christians itakuwepo huko na hivyo "FUNDISHO LA PASAKA" kufifia kwa kiasi kikubwa, fundisho la pasaka ni somo la kiimani na somo hilo linawahusu watu wote kwani kwa imani ya Wakristo Yesu ni mkombozi wa Ulimwengu wote hivyo kama yupo Muisilamu au mpagani ambaye kavutiwa na Ufufuko wa Yesu basi anaweza kujiunga na Ukristo, kwa upande wa pili Usomaji wa Qur'an ni tukio la kiimani na limehimizwa katika Uisilamu na Qur'an ni mafundisho kutoka kwa Mungu kwa mujibu Uisilamu nayo yanawahusu watu wote hivyo mtu akiisikiliza Qur'an anapata rehema kutoka kwa Mungu (this is according to Qur'an), na kama ni mkristo akavutiwa na Uisilamu anaweza kujiunga na Uisilamu hivyo mleta mada alikuwa na "underlying logic" ya aina hiyo isipokuwa tu alishindwa kuiweka katika muundo huo.
Acheni kila mtu aamini kile anacho kiamini, ningewaona mna akili iwapo mnge hamasisha kufungwa kwa mabaa na sehemu za starehe siku hiyo ili watu wasisherekee kwa kulewa na kufanya uzinzi kitu kinacho haribu dhana na maana nzima ya pasaka hiyo ndo maana ya kuiheshimisha pasaka na sio ngonjera zako hizo.
 
Utajipa tabu bure na kujiumiza kichwa,sehemu nyingi Tanzania,hasa sehemu za Pwani,ndani ya familia moja wamechanganyika wakristo na waislamu, na wanashirikiana kwenye furaha na huzuni,usishangae kwenye mashindano ya Qur'an kukuta wa dini zote wapo.

Na mashindano yakimalizika ni saa saba,wakiondoka hapo wote kwa pamoja wanakwenda kutembea kwenye Pasaka.

Kuna wakati kulikuwa na jirani zangu ni waislamu,wakawa wamefiwa na mjukuu wao,kufika mjukuu ni mkristo na maiti imeletwa kwa babu yake muislamu,wakachanganyika waislamu na wakristo,bila kubaguana.
Umejibu vizuri sana kiungwana
 
Elewa post ya mleta mada na comment yangu.

Ni hivi; katika nchi ambayo Kuna watu wa imani tofauti Kuna muda busara inatakiwa itumike na si kushindana. Hii habari ya waislamu kuingilia sikukuu za wakristo na wao kujifanya wako bize kuadhimisha siku zao wakati wangeweza kuwaacha wenzao washerekee sikukuu yao Kisha wao(waislamu) wangesogeza Hadi jumapili nyingine kungekuwa na ubaya gani mkuu?

Mimi ninachosikitika ni hii hali kuifanya karibia kila mwaka. Ikifika pasaka na nyie waislamu mnaomba uwanja mnaganya maadhimisho ya Quran. Tujifunze ustaarabu kwa waislamu wa Senegal. Kule wakristo wachache 10% na waislamu 90% lakini wakristo wanaheshimiwa Sana.


Hiyo "busara" unayoitaka ni religious compromise, na kamwe haitawezekana kuwepo na compromise ya aina hiyo, kila dini inayo mafundisho na taratibu zake na haitakiwi iingiliwe na taratibu za dini nyingine, Wakristo mnayo Pasaka yenu na Waisilamu wanayo siku yao ya kusoma Qur'an na wao wenyewe wataamua ni siku gani Qur'an isomwe na nani awe ni mgeni rasmi, na kwa kufanya hivyo hawajavunja heshima ya kitu chochote.

Sasa hoja yenye mashiko ambayo ni Common kwa dini zote mbili ni swali hili; je Pasaka na Usomaji wa Qur'an unayofaida gani kwa WATU wote??? (Hizi dini ni kwa ajili ya watu wote, haya ni madai ya hizo dini).

Kama usomaji wa Qur'an ni kwa ajili ya watu WOTE basi hapo ndipo hiyo "Busara" ingetumika kupisha kwanza sikukuu ya Pasaka ipite na Waisilamu nao siku hiyo wapate nafasi ya kupata mafundisho ya kiimani kuhusu pasaka ili nao ikibidi siku moja wawe wakristo, hivyo pasaka ni mahubiri.

Ni jambo hilo hilo kwa Waisilamu kuhahirisha siku ya kisomo cha Qur'an ili kuwapa nafasi Wakristo kujumuika kupata Baraka za kisomo na hata ikibidi kama kuna mkristo atakayevutiwa na uisilamu basi anayo hiyari ya kusilimu.

Hiyo ndio logic na busara ya; kwanini Waisilamu Waahirishe siku ya kusoma Qur'an isiingiliane na sikukuu ya Pasaka kinyume na hiyo logic hukutaweza kamwe kuwepo compromise ya aina yoyote kwani dini hizi kimsingi kila moja ipo kivyake.

Cc: GENTAMYCINE
 
Sasa hi hoja yako in Uhusiano gani na thread ya mleta mada mkuu?

Basi Kama ulishindwa kusoma kilichoandikwa si ungesoma tu tittle ungeelewa anakusudia kusema Nini?

Swali ni kwa Nini kilele Cha siku ya Quran iwe siku ya maadhimisho ya pasaka? Kwa nini wasingevuta ikawa jumapili ile nyingine,ili jumapili hii ya pasaka waheshimu wenzao wakristo washerekee sikukuu yao ambayo waliisubiria kwa siku 40(kwaresma)?

Hivyo ndivyo ilipaswa kuwa. Ni swala la ustaharaabu tu,na si kushindana.
Mbona hakuna muingiliano wowote? Waislam watadeal na qur an na wakristo watadeal na pasaka. Mbona kwaresma na Ramadan vimeingiliana na hakuna shida yoyote
 
Sasa hi hoja yako in Uhusiano gani na thread ya mleta mada mkuu?

Basi Kama ulishindwa kusoma kilichoandikwa si ungesoma tu tittle ungeelewa anakusudia kusema Nini?

Swali ni kwa Nini kilele Cha siku ya Quran iwe siku ya maadhimisho ya pasaka? Kwa nini wasingevuta ikawa jumapili ile nyingine,ili jumapili hii ya pasaka waheshimu wenzao wakristo washerekee sikukuu yao ambayo waliisubiria kwa siku 40(kwaresma)?

Hivyo ndivyo ilipaswa kuwa. Ni swala la ustaharaabu tu,na si kushindana.
Exactly.
 
Kwa Mimi naongea nikiwa nimefunga hapa dada yangu kaolewa na mkristo huko Kilimanjaro na anakuja nyumbani ..

Bibi yangu upareni ana ndugu kibao ni wasabato kasoro yeye tunakaa nao wanapikiwa wao tu siku za Ramadhani sisi sote tumefunga..kwa maana hyo sherehe zetu zote lazima utakuta mchanganyiko wa dini zote kwa sababu tu ukaribu na undugu kabisa.
Ndio ukweli, hakuna ubaguzi kabisa. Nakumbuka tumesoma shule ya inaitwa Muslim school, lakini kulikuwa na waalimu wakristo, wengine ni masister, hawa walikuwa hata kuwachapa wanafunzi, hawawachapi, wanakaa na sisi wanafunzi waislamu kiuzuri kabisa.
 
Mbona hakuna muingiliano wowote? Waislam watadeal na qur an na wakristo watadeal na pasaka. Mbona kwaresma na Ramadan vimeingiliana na hakuna shida yoyote
Umemaliza mjadala,hoja zako ni za kisomi.
 
Sherehe za mashindano ya Quran zinafanyika sehemu ndogo tu ya Nchi(kwenye uwanja wa taifa) ambapo pia ni masaa hayazidi saba ndani ya muda huu hata pilau linakuwa halijaiva! Na wahudhuriaji ni waislamu..Sasa hiyo dharau hapo inakujaje ikiwa wanaohusika ni waislamu!? Nyie si muendelee na mambo yenu kwani kuna aliyewaita kuhudhuria sherehe hizo!?..Umekuwa mpumbavu mpaka upumbavu umeshaanza kujuta kukaa na wewe sasa...
Hawa jamaa huwa siwaelewi kabisa, wakitokea hapo wanasema waislam wanapenda kulalamika Sasa sijui wanachokifanya hapa ni nini kama sio malalamiko tena yasiyo na msingi
 
Hayo mashindano siya ya kumualika kiongozi mkuu kama mgeni rasmi. Bila shaka atatuma mwakishi wake ambaye kimsingi atakuwa waziri fulani mwenye imani hiyo. Kwanza ni makosa makubwa kuita usomaji huo eti ni mashindano. Kwa mungu hakuna mashindano. Hiyo ni ibada kama ibada zao zingine. Halafu kuweka siku ambayo taifa litakuwa linaadhimisha sikukuu kwa waumini wa kikristo haileti maana nzuri kwa wakristo wa tanzania. Je kama mgeni rasmi siku hiyo ataalikwa na maaskofu kwenda kuhutubia taifa katika maadhimisho ya pasaka ataenda upande upi? Au atahutubia kotekote bila kuchoka? Hao watu wawe wanaheshimu sikukuu za taifa kama zilivyopangwa, ina maana hawajui siku za matukio ya kitaifa mpaka wapange mashindano yao siku hiyo? Hio ni dharau na si busara na hekima
Acha uchizi wenyewe wanakwambia mashindano wewe unasema ibada
 
Back
Top Bottom