Maadhimisho na Kilele cha Usomaji Quran kufanyika Siku ya Pasaka ni Dharau na Uchokozi kwa Wakristo au ni Utaratibu tu?

Matukio wengi sijawahi kuona nimekaa Tanga sana na pale mtaani si mzee wangu wala waarabu wa pale Godown za Simba mtoto walikuwa wakitoa chakula kwa wote siku za Eid enzi hizo.

Nimesoma shule sijawahi kukutana na izo mambo tulikuwa tunaishi vizuri kabisa na kuheshimiani hata kupeana mialiko.

Sisi kipind tunaanza shule fulani headmaster alikuwa ni mkristo hakutaka kabisa tuende kuswali saa Saba na shule yetu ilikuwa na eneo kubwa ..Yupo mwalimu alikuwa anakituadhibu maana kipind chake ni mwisho kuanza name mpaka kutoka 8:30 na ilikuwa ni chuki tu...Pia alikuwa akiongea chuki za wazi kabisa kwa kukashfu dini yetu...


Bahati nzuri ile safu yetu matokeo ndo tulifanya poa wote na kingine alikamatwa na mtoto wa kidogo mdogo wa form 3 alimpa mimba akaozeshwa hapa sijaweka kwamba ukristo ndo umemtuma , bali ni tabia yake binafsi.

Migogor haiwezi kuepukika kwa sababu chokochoko zipo na wala tusiwe too general nimeishi Tanga kama Kuna matukio yalifanyika ya ubaguzi kabla ya mwaka 2012 niambie nimekaa pale sijawahi kuona wala nn na misikiti inayofuturisha ile mda baada ya swala wanajaa wakristo wengi waislamu wanaenda kula makwao hii ni hakika 100% maana jqmaa zangu ndo walikuwa wanaenda..

Baadhi ya madai pale shule palikuwa na kasumba siwezi kukuambia ila ni ukweli kesi moja Kuna mwanafunzi ni mpemba bhana alikuja kugombana na mwenzie bahati mbaya yule mwenzie alimsema sana akamvua hijabu yake kichwani..Siwez kuendelea ila palizuka mgogoro wa kidni mkubwa sana mpaka sisi tulikaa pembeni .
 
Kwa Mimi naongea nikiwa nimefunga hapa dada yangu kaolewa na mkristo huko Kilimanjaro na anakuja nyumbani ..

Bibi yangu upareni ana ndugu kibao ni wasabato kasoro yeye tunakaa nao wanapikiwa wao tu siku za Ramadhani sisi sote tumefunga..kwa maana hyo sherehe zetu zote lazima utakuta mchanganyiko wa dini zote kwa sababu tu ukaribu na undugu kabisa.
 
Hiyo pasaka waislam inawahusu nn mpaka waache kufanya mambo yao kwa ajili yake?
 
Hakuna mtu anayemiliki Siku! Sioni mantiki


Ni matumizi ya siku ndio yanamilikiwa na watu.

Mleta mada alitaka siku ya pasaka Waisilamu wawaachie wakristo watese peke yao huku Waisilamu wakikodoa macho kuangalia Bwana Yesu "akifufuka" na hata kama kuna fundisho la kidini katika siku hiyo waisilamu wapate, halafu siku nyingine ndipo Waisilamu wafanye maadhimisho ya kilele cha Usomaji wa Qur'an huku Wakristo nao wajumuike au washiriki kupitia Luninga nk kusikia sauti tamu za kisomo cha Qur'an tukufu ikizingatiwa kuwa katika hafla hiyo ya kilele cha usomaji Qur'an atakuwepo Mama (Bi mkubwa) kama mgeni rasmi.

Nadhani hoja ya msingi ya huyo mtani wangu ilikuwa ipo hapo ila yeye alishindwa kuijenga ili ilete mantiki kwa wasomaji.😀😀
 
Hakuna undugu wowote wa kiimani kati wa Uislam na Ukristo acheni unafiki.
Sasa waislam wasimamishe shughuli zao kwani pasaka inawahusu nn wao?

Waislam watashuhudiaje kufufuka kwa yesu wakati wao hawaamini kakita ufufuo?
Na wakristo watajumuikaje kusikiliza Qruani wakati hawaiamini?

Wakristo na waislam wana undugu mbali mbali wa damu, kikazi ,kirafiki, lakini linapo kuja suala la kiimani ni mbingu na ardhi hivyo msipende kurazimisha mambo.
 
Hivi unataka kusema Waisilamu kufanya siku hiyo kuwa kilele cha usomaji wa Qur'an ni kuivunjia heshima Sikukuu ya Pasaka?!![emoji57]

Kama maana yako ni hiyo Hebu fafanua inakuaje mambo ya Uisilamu (kusama Qur'an) ivunje heshima ya Pasaka??
Elewa post ya mleta mada na comment yangu.

Ni hivi; katika nchi ambayo Kuna watu wa imani tofauti Kuna muda busara inatakiwa itumike na si kushindana. Hii habari ya waislamu kuingilia sikukuu za wakristo na wao kujifanya wako bize kuadhimisha siku zao wakati wangeweza kuwaacha wenzao washerekee sikukuu yao Kisha wao(waislamu) wangesogeza Hadi jumapili nyingine kungekuwa na ubaya gani mkuu?

Mimi ninachosikitika ni hii hali kuifanya karibia kila mwaka. Ikifika pasaka na nyie waislamu mnaomba uwanja mnaganya maadhimisho ya Quran. Tujifunze ustaarabu kwa waislamu wa Senegal. Kule wakristo wachache 10% na waislamu 90% lakini wakristo wanaheshimiwa Sana.
 
GENTAMYCINE hueleweka na Werevu wachache kama Wewe hapa JamiiForums ila Wapumbavu wengi hushindwa Kunielewa.

Cc: Hance Mtanashati
 
Huwez kuwapangia waislam siku ya kuadhimisha mashindano ya Quran.

Waliopanga hiyo tarehe walikua na sababu zao na wala sio kwa sababu unazozifkiria ww, na wala sio ushindani.

Unavosema wangevuta mbele unajua ingewagarimu kias gani? Pengine siku hyo mgeni rasmi ndo Ana nafasi, au pengine siku hyo ndo kuna nafasi ya uwanja wa kufanyia maadhimisho, au pengine kuna sababu kibao ambayo imewafanya waweke siku hiyo,

Unapozungumza jambo litafakari kwanza, usikurupuke, kuna wakati machafuko tunayatengeneza sisi wenyewe kuongea vitu vya kichochezi, ukikaa kimya jambo litapita vzr bila shida, waislam watafanya yao, na wakristo watafnya yao, kila mmoja atafurahi kwa nafasi yake. Wala waislam hawatawazuia wakristo kutosherehekea.
 
Hayo mashindano siya ya kumualika kiongozi mkuu kama mgeni rasmi. Bila shaka atatuma mwakishi wake ambaye kimsingi atakuwa waziri fulani mwenye imani hiyo. Kwanza ni makosa makubwa kuita usomaji huo eti ni mashindano.

Kwa mungu hakuna mashindano. Hiyo ni ibada kama ibada zao zingine. Halafu kuweka siku ambayo taifa litakuwa linaadhimisha sikukuu kwa waumini wa kikristo haileti maana nzuri kwa wakristo wa tanzania.

Je, kama mgeni rasmi siku hiyo ataalikwa na maaskofu kwenda kuhutubia taifa katika maadhimisho ya pasaka ataenda upande upi? Au atahutubia kotekote bila kuchoka? Hao watu wawe wanaheshimu sikukuu za taifa kama zilivyopangwa, ina maana hawajui siku za matukio ya kitaifa mpaka wapange mashindano yao siku hiyo?

Hio ni dharau na si busara na hekima.
 


Lakini Umenielewa nilichosema??!!

Labda niseme hivi; huyo mleta mada kimsingi alitaka katika siku hiyo ya Pasaka Waisilamu wangesimamisha na kuahirisha kilele cha usomaji Qur'an kwasababu katika kilele hicho mgeni Rasmi atakuwa ni Mama hivyo attention ya Waisilamu na wasiokuwa waisilamu mainly Christians itakuwepo huko na hivyo "FUNDISHO LA PASAKA" kufifia kwa kiasi kikubwa, fundisho la pasaka ni somo la kiimani na somo hilo linawahusu watu wote kwani kwa imani ya Wakristo Yesu ni mkombozi wa Ulimwengu wote hivyo kama yupo Muisilamu au mpagani ambaye kavutiwa na Ufufuko wa Yesu basi anaweza kujiunga na Ukristo, kwa upande wa pili Usomaji wa Qur'an ni tukio la kiimani na limehimizwa katika Uisilamu na Qur'an ni mafundisho kutoka kwa Mungu kwa mujibu Uisilamu nayo yanawahusu watu wote hivyo mtu akiisikiliza Qur'an anapata rehema kutoka kwa Mungu (this is according to Qur'an), na kama ni mkristo akavutiwa na Uisilamu anaweza kujiunga na Uisilamu hivyo mleta mada alikuwa na "underlying logic" ya aina hiyo isipokuwa tu alishindwa kuiweka katika muundo huo.
 
Utashangaa kwa Akili Kubwa yako hii Uliyoandika hapa bado kuna Mijuha ( Nuts ) itakubishia tu.

Cc: Mokaze na Hance Mtanashati
 
Angalia tarehe vizuri
Mpaka Jana Usiku Mabango yote ya Barabarani juu ya hilo Tukio tarehe iliyokuwepo ni 9 April, 2023 na sasa baada ya kuona GENTAMYCINE nimewashikeni pabaya mmeamua kubadili tarehe na Venue. Hovyoooooooo....!!!!!!!

Mimi ndiyo GENTAMYCINE The King!!!!
 
Binafsi sioni kama Kuna tatizo..
 
Stupid,yaaan umeandika utumbo .pumbavu zako
 
Binafsi sioni kama Kuna tatizo..
Hopeless kungekuwa hakuna tatizo wangebadili tarehe ya hilo Tukio lao kutoka tarehe 9 April ( Pasaka ) na sasa kuwa tarehe 2 April?
 
Ukiongelea Israel hao ni dini ya Jewish.
Pasaka ni ya Wakristo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…