Maafisa uhamiaji Walivyomtesa mtuhumiwa, Je, Sheria inawaruhusu?

Maafisa uhamiaji Walivyomtesa mtuhumiwa, Je, Sheria inawaruhusu?

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Nianze kwa kukiri huyu jamaa kama amedanganya kwa kile kinachosemwa amekosea na ni mtuhumiwa anapaswa aadhibiwe kwa mujibu wa Sheria.

Lakini haya yanayofanywa kwenye hii video ni moja ya majukumu ya hawa maofisa waliomkamata huyu Jamaa? Je, tunafahamu athari zake ikiwa vyombo hivi vitaachwa kijichukulia sheria mkononi?

Nachelea kusema haya mambo yakiachwa raia wengi watakuja athirika nayo. Hizi athabu zikiachwa ziwe zinatolewa na vyombo vya dola ubinadamu wote utaondoka. Tutabakia na Unyani.

Jamaa alipaswa akamatwe na apelekwe sehemu stahiki ili sheria zikafuate mkondo wake.

Zaidi, soma; Askari 3 wa Uhamiaji wasimamishwa kazi kwa kosa la kutumia nguvu dhidi ya Alex Raphael
 
No binafsi nasema sawa why uingile KAZI za WATU ,bora zoezi husika kuliko kwenda jela,bado hao wajifanyao tiss ,hii ni elim tosha kwa umma, ingekua mie alitakiwa fanya zoezi la mgando upside down, jitu limenenepeana kwa pesa za wizi ,na hapo hatujui anavyo wapelekesha WATU wa mtaani kwake kwa kuvaa cheo ambazo hana.
 
Hii imekaa vizuri sana, wapo watu wameanza kudharau mamlaka za serikali kisa tu JPM hayupo. Huyu Kama ameweza kuingia ofisi nyeti hivyo nakudanganya eti anatoka TAKUKURU ameshadhulumu watu wangapi? Yawezekana huyu mtu ni jambaza au muhalifu ni vyema tukapata taarifa rasmi.

Kuingia kwenye vyombo Kama TAKUKURU ukijua siyo mtumishi wa chombo hicho then utegemee kutoka salama hicho chombo kitakuwa kimekufa.

Hawa watu ndiyo wanaotuibia kwa sms za namba zisizofahamika. Na wakikukamata usiku ndo utajua haki za binadamu au la.

Vibaka wamezagaa kila kona imefika wakati Sasa wanajitutumia Hadi kwenye vyombo vya dola, no. Vyombo vyetu vijiimarishe kuwashughulikia Hawa watu la sivyo wakiruhusiwa kutetewa tutawapa kiburi.

Mtu hata bia haishuki kisa vibaka Kama Hawa, juzi wamepiga mtu mbezi mara kituo Cha mafuta wamenyang'anya silaha......kwanini haya yatokee Kama siyo kujaribu nguvu ya utawala mpya
 
Hebu ngoja kwanza kwani imekuaje mpaka huyo jamaa wakamdhalilisha kiasi hicho? Halafu jamaa anasema kabisa mmempima presha?
 
1621258979442.jpg
 
Huyu kijana namjua ni ndugu zake nadhani wanatoka Bukoba, Kuna kipindi alikuwa anaendesha gari ya mkubwa mmoja hapo jijini Dar es salaam. Huyu nadhani ameajiriwa serikalini na hapo kakamatwa may be akiwa anajifanya TAKUKURU.

Na hawa ndio watu waliokuwa wanatutisha kama watu wasiojulikana kujipatia fedha. Kama mzazi lazima uuzunike kuona namna watoto walivyokuwa na ujasiri kujitambulisha kama watendaji wa Umma.

Nadhani pia suala lakutisha watu Mimi Ni Nani liishe. Hivi vyuma vimeumana, hao ni wao kwaoooooo huyu kijana ni wa system au walimlea huko amezoeaaa?
 
haya ndo mambo si ya kuacha hivi hivi yapite. wahusika kama si unyama binafs wanatumia sheria gani? dhana ya utawala bora inatupa shida sana manyani
Wajinga Kama Hawa wameumiza Sana watu mitaani, fikiri wapo hujifanya Tiss, madaktari je wanaumiza watu wangapi
 
Back
Top Bottom