Maagizo ya Waziri Mkuu kutaka UKOO MZIMA kukamatwa kwa makosa ya ndugu yao si sahihi kisheria!

Maagizo ya Waziri Mkuu kutaka UKOO MZIMA kukamatwa kwa makosa ya ndugu yao si sahihi kisheria!

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
7,748
Reaction score
10,288
Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba amesimulia kisa cha mkazi wa Arusha ambaye amelizwa kiasi cha takriban Sh600 milioni na kijana aliyemuamini akamchukulie mkopo.

Kutokana na kisa hicho, Dkt. Mwigulu amemuagiza Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Justine Masejo, kijana huyo apatikanae na ikiwezekana ukoo wake wote ukamatwe.

“Nimemuelekeza RPC amsake huyo kijana amkamate, hata kama wakikamatwa ukoo mzima wakamatwe walipe fedha zile, hawezi mama maskini anakosa pa kukaa wakati yule aliyekula fedha anatembea mkanda nje,” - Mwigulu

MAONI YANGU:
Yaani kwa kuwa mtoto wao ametapeli ndio familia nzima ikamatwe?

Sheria za nchi yetu zikoje? Yaani utapeli ufanywe na mtu mwingine halafu wakamatwe wengine?

Polisi na vyombo vya usalama vimeshindwa kumkamata mhusika hadi ndugu na jamaa nao wakamatwe?

Taarifa kwa ufupi

Pia soma > Mwigulu damu za watanzania mliowaua zinakulilia. Umeanza kuchangamka
 
Yaani kwa kuwa mtoto wao ametapeli ndio familia nzima ikamatwe?

Sheria za nchi yetu zikoje? Yaani utapeli ufanywe na mtu mwingine alafu wakamatwe wengine?

Polisi na vyombo vya usalama vimeshindwa kumkamata mhusika hadi ndungu na jamaa nao wakamatwe?

Ongeza nyama au weka crip. Story haijitoshelezi.
 
Kwanza nikurekebishe kidogo hakusema familia nzima ikamatwe usimsingizie waziri wetu alichosema yeye ni ukoo mzima yaani ukifanana nae lile Jina la mwisho tu umekwenda na maji😂😂

Mtaenda kueleza vizuri Kwa Nini hamkumfundisha kijana wenu tabia njema kama alivyosema boss wake kwamba mngetaka vijana wenu wasiuwawe mngewakataza wasiingie barabarani
 
Hadi mtu atolewe vitu ndani ya nyumba maana yake si kesi ya jana hiyo.
Ni kesi ya muda mrefu, maana yake imepita Polisi, Mahakamani hadi Mahakama ya Rufaa

Swali ni je Huyo mwenye nyumba iweje Hati yake itumike?
Iweje Bank wakubali kama yeye si mkopaji?
Aweke mkataba wa makubaliano kati yake na Bank, Mkopaji
 
Ni kama nimedandia mtumbwi wa vibwengo. Sijui wanaenda wapi wala wanajadili nini,ngoje niruke tu.
Kwa ufupi
Kuna Kijana alikubaliana na Familia moja huko Arusha kuwa akope pesa, kisha wagawane, sasa mkopo haujarudi, nyumba ya familia inapigwa mnada, Familia imeenda kwa mwigulu, Mwigulu kaagiza Ukoo wa huyo kijana ukamatwe na wasiachiwe hadi pesa ilipwe
 
Kama full stori ipo humu tag me.
 
Hii mbinu huwa inatumika ili kumkamata muhusika kama atakua hapatikani kuna Jambazi mmoja alivyosikia mama mzazi kakamatwa alienda kujisalimisha polisi mwenyewe. Wakamdaka wakamuachia mama so hizi techniques huwa zinatumika.​
 
Kisheria imekaaje au ni ya kujiongeza tu!! Mfano mimi namdai mtu naweza omba polisi wamkamate mzazi wake?
 
Acha wafanye kila mbinu mhusika apatikane! Haiwezekan familia fulan inalia halaf mpigaj anakula goodtime kitaa!
 
Yaani kwa kuwa mtoto wao ametapeli ndio familia nzima ikamatwe?

Sheria za nchi yetu zikoje? Yaani utapeli ufanywe na mtu mwingine halafu wakamatwe wengine?

Polisi na vyombo vya usalama vimeshindwa kumkamata mhusika hadi ndugu na jamaa nao wakamatwe?

Taarifa kwa ufupi

Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba amesimulia kisa cha mkazi wa Arusha ambaye amelizwa kiasi cha takriban Sh600 milioni na kijana aliyemuamini akamchukulie mkopo.

Kutokana na kisa hicho, Dkt. Mwigulu amemuagiza Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Justine Masejo, kijana huyo apatikanae na ikiwezekana ukoo wake wote ukamatwe.

“Nimemuelekeza RPC amsake huyo kijana akamatwe hata wakikamatwa ukoo mzima wakamatwe walipe fedha zile, hawezi mama maskini anakosa pa kukaa wakati yule aliyekula fedha anatembea mkanda nje,”amesema.

Pia soma > Mwigulu damu za watanzania mliowaua zinakulilia. Umeanza kuchangamka
Hii sheria itafaa sana kuwakamata wanaukoo wote wa Msoga gang na Kizimkazi gang
 
Hivi,hao polisi wanapopelekwa CCP huwa wanafundishwa nini kama hawajui hata hatua za upelelezi hadi kuubaini ukweli/uhalifu?Wanapewa maelekezo ya kukamata wasiohusika na uhalifu?Sheria ya makosa ya jinai (Criminal Procedure Act na vifungu vyake)inasemaje kuhusu mtu mmoja kuwajibika kwa makosa aliyoyafanya mtu mwingine?
 
Back
Top Bottom