matonyamswanu
JF-Expert Member
- Dec 7, 2025
- 358
- 433
Wakati mwingine hamueleweki mpaka nashangaa.Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba amesimulia kisa cha mkazi wa Arusha ambaye amelizwa kiasi cha takriban Sh600 milioni na kijana aliyemuamini akamchukulie mkopo.
Kutokana na kisa hicho, Dkt. Mwigulu amemuagiza Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Justine Masejo, kijana huyo apatikanae na ikiwezekana ukoo wake wote ukamatwe.
“Nimemuelekeza RPC amsake huyo kijana amkamate, hata kama wakikamatwa ukoo mzima wakamatwe walipe fedha zile, hawezi mama maskini anakosa pa kukaa wakati yule aliyekula fedha anatembea mkanda nje,” - Mwigulu
MAONI YANGU:
Yaani kwa kuwa mtoto wao ametapeli ndio familia nzima ikamatwe?
Sheria za nchi yetu zikoje? Yaani utapeli ufanywe na mtu mwingine halafu wakamatwe wengine?
Polisi na vyombo vya usalama vimeshindwa kumkamata mhusika hadi ndugu na jamaa nao wakamatwe?
Taarifa kwa ufupi
Pia soma > Mwigulu damu za watanzania mliowaua zinakulilia. Umeanza kuchangamka
Mwigulu anaweza kuwa mbaya kwa mengine ila sio hili.
Unaonaje kama angeacha kumtetea mdhulumiwa na akamkingia kifua tapeli.