Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji120]Alamsiki
Acha ujinga ww. Kama alikuwa na mapenzi na wewe angekutafuta mkawa wote. Tupo busy na maandalizi ya kampeni. Huyo dadani muhuni nadhani hauwajui wanawake wapore .NI MAAMUZI MAGUMU LAKINI YAMETOKA MOYONI
Wapendwa wana jukwa hili la mahusiano, mapenzi na urafiki ninawasalimu nyote.
Kama habari ya awali inavyosemaka kuwa nimechukua uamuzi mgumu wa kuwa baba mtarajiwa wa mtoto mtarajiwa wa rafiki yangu kwa hiyari na kwa kupenda mwenyewe kwa sababu nitakazo zieleza hapa chini, lakini kabla ya hizo sababu naomba nitoe ufafanuzi wa urafiki wetu.
Kuna dada mmoja tulikutana ofisi flani ya serikali, ni dada flani mpole kiasi na mcheshi kiaina. Kwa muda mfupi sana nilivutiwa naye na ikafikia hatua ya kubadilishana naye namba za simu.
Zoezi la huduma lilienda vyema kwa yeye kufanya koneksheni na mtumishi flani na tukafanikiwa kupata hiyo huduma (pass ya kusafiria kwa haraka).
Baada ya hapo hatukuwasiliana haraka japo nilipanga lazima nimtafute. Ulifika wakati tukaanza kuwasiliana hapa na pale. Na ukafika wakati nikawa nachomekea viutani kuwa ninamhitaji awe rafiki yangu.
Baada ya muda mrefu tulifanikiwa kuwa marafiki hatimaye tukaanza kushirikiana....hapa wakubwa mmeelewa. Jambo nililompenda zaidi ni mwelewa na mwenye misimamo yake mizuri. Tuliwekana wazi kuhusu mahusiano yetu, kwake yeye mpenzi wake alikuwa ni raia wa kigeni na anaishi huko kwao huja mara chache hivyo alikuwa anajiandaa kwenda kumtembelea na walikuwa wamepanga kuoana.
Nini kilitokea kati yao?
Uliwadia wakati wa kusafiri alinijulisha nami nilimpa nafasi ya kuwa mbali naye kimawasiliano ili ajiweke sawa na akili yake iwaze juu ya mpenzi wake. Alifanikiwa kwenda na kurudi. Baada ya kurudi mawasiliano yetu yalikuwa hafifu kwani nilikuwa tight sana na kazi.
Baada ya miezi kama mitatu na nusu, tuliwasiliana na kupiga stori nyingi na mwishowe akanijulisha ni mjamzito. Nikampa hongera zake. Lakini mawasiliano yakazidi kuwa hafifu zaidi. Ukafika wakati nikamuuliza maendeleo na mipango ya ndoa na kama wamepanga lini wataanza kuishi pamoja?
JIBU LAKE NDILO HASA LILINIGUSA NA KUAMUA HAYA
Rafiki yangu huyu alinishtua aliponieleza kuwa walitengana na yule mchumba kwani walipokutana ughaibuni alimfanyia visa vingi vibaya mno..sitavitaja
Na alipotua nchini alimtumia ujumbe kuwa asimtafute tena. Akiwa katika hali ya kutafakari yaliyompata na jinsi gani atasonga mbele...ndipo alianza mahusiano na jamaa flani aliyeanza kumnyemelea kitambo na muda mfupi akapata ujauzito.
Baada ya kupata ujauzito alimjulisha mhusika lakini hakuwa tayari kuukubali bali alimwambia autoe kwani yeye ana familia lakini aligoma kuutoa na akajiapiza ataulea na kwa vile jamaa ameukataa hata jina litakuwa la upande wa familia yake yaani ubini wa baba.
Habari hii iliniumiza sana na niliwaza haya yafuatayo;
1. Kuwa huyu dada ataishi kwa sonono kubwa wakati wa ujauzito na atamwathiri mtoto akiwa tumboni wazazi wanajua hili.
2. Huyu atakayezaliwa hatakuwa na upendo katika jamii na anaweza kuja kuwa na tabia ya ajabu.
MAAMUZI YANGU
1. Nikamwomba kama naweza kuwa baba wa wa hiyari na apewe ubini wa jina langu kama baba alikubali hili kwa mshangao mkubwa sana (Haya[emoji116]sijamshirikisha)
2. Nitamhudumia kipindi chote cha ujauzito
3. Nitamfanya mwenye furaha ili kulinda afya mama na ya mtoto atakaye zaliwa
4. Baada ya mtoto kukua yeye yuko huru kuwa na maisha yake bila mimi kumwingilia uhuru wake.
5. Nitampa mtoto kiwanja na kumjengea kadri Mungu atakaponiweka hai na kunibariki, ili apate malazi na malezi bora.
Uamuzi huu nimeufanya mwenyewe japo sipangi kuishi na mtoto isipokuwa kumsapoti kimalezi tu.
Baada ya kukubaliana naye hasa kuhusu mtoto kuitwa kwa jina langu kama baba, alifurahi sana kiasi cha kulia machozi na nikamwahidi kuwa siku chache zijazo atakuja mkoa nilipo apate mapumziko ya muda mfupi sio nyumbani kwangu lakini. Amemweleza mama yake mzazi na hajaamini kuwa kuna mtu anaweza kufanya maamuzi magumu kiasi hiki.
Pamoja na hayo sijamweleza kwa undani namna nilivyojipanga kumsapoti mtoto hasa kumpa eneo na kumjengea, hili nimebaki nalo nikiomba Mungu aniwezeshe kulitimiza.
Wapendwa wana jf, inaweza kuonekana kuwa uamuzi wangu ni wa kijinga sana lakini kwangu mimi nitaona fahari kubwa kama hili litafaniniwa kwani;
Sisi wanaume tunapaswa kuwa chemichemi ya furaha ya wake zetu, mama, watoto na dada zetu lakini kinyume chake tumekuwa ni chanzo cha machozi.
Tujitahidi sana kuwafanya watu kuwa na furaha badala ya machozi. Muwe na wakati mwema wote.
(KATIKA HILI SITEGEMEI ANY RETURN)
Nimekusoma mkuumkuu Mswati nimepitia kisa chako kwa makini, kwanza nikupongeze kwa ujasiri uliochukua. Ni maamuzi magumu, lakini ndiyo uanaume. watu wengi wana moyo dhaifu, ndo maana wanakupinga na hawaelewi. lakini mimi ninaweza kuelewa,
Fanya kitu kwa amani ya moyo wako. usirudi nyuma.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna shida...niwe tu Baba yao!!Njoo tulee wakwangu . Nina wanne sijui utaweza . 😂😂😂😂😂😂
Mimi mwenyewe nahisi jamaa ana shida sehemuWazazi wako unawasaidia kweli? Una matatizo sio bure.
Mkuu vipi, naona umeguswa na wewe, unataka kunisaidia ama?Vipi majukumu yameanza?
Sawa mkuu, Acha nikusanye thawabu peke yangu!Hiyo toto 4 hapana pambana kivyako mkuu[emoji38][emoji38][emoji38]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Mkuu una siasa kaliii!! Mwanao yupo level gani ya elimu???? Kuna kitu unaficha kuhusu hilii
Huyupo serious kijana huyu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Mzee wa kula kimasihara, unaanza kuhisi kwamba bro hatungishi?
Hahaaa Riki bwana!
Karibu baba wanne .. Karibu sana 😂😂😂😂Hakuna shida...niwe tu Baba yao!!
Hapana utakuwa unazawadi ya kiroho mkiwa serious na mungu mnakuwaga manabii.ngoja nimalizie konyagi kwanzaYa kijinga eee
ahsante mama foo!!!Karibu baba wanne .. Karibu sana 😂😂😂😂
Njoo basi tutazaa wetu mmoja tupate 🖐🏼 eeh baba ila mashart sitaki maana hawa 4 wote wakiume usije sema unataka wa kike 😂😂😂😂ahsante mama foo!!!