Mpo poah wakuu!
Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu..
Tumerudi nyumbani, Moshi kama ilivyo ada, kwa wakazi wa moshi mjini, Nipo hapa Kibosho Road. Mimi ndio nilikuwa wakwanza kuja moshi kabla ya dogo ambaye amekuja jumapili ya wiki hii.
Sasa juzi jumanne Dogo katuweka kikao, akatuambia amepata mchumba na anafikiri kuwa huyo ndiye mke wake. Tukafurahi, Dingi akaagiza kreti ya bia ili kikao kikamilike.
Mama na Baba waliuliza maswali yote ya msingi kumhusu huyo mchumba wake, Dogo akayajibu vizuri sana, Wazazi walifurahi mno.
Kikao kilikuwa na watu kumi. Baba, Mama, ndugu zangu wanne, yaani mimi, kaka yangu, dada, na huyo dogo wetu wa mwisho mwenye mchumba, Baba mdogo na mke wake na watoto wadogo wawili wa baba mdogo.
Kwa vile ndugu zangu wakubwa wako bize, nikateuliwa mimi ndio siku yakwenda kutoa mahari basi mimi niwe bega kwa bega na dogo. Dogo alifurahi ukizingatia mimi naye tumenyang'anyana ziwa na tunapenda kichizi.
Katika hali isiyotarajiwa, hali ikavurugika, kutokana na swali langu nililouliza, Niliuliza hivi; Huyo mchumba wako ni bikra? Kama ni bikra nitaenda na wewe kutoa mahari, kama sio tafuta mwingine wakuenda naye.
Kauli hiyo ilileta ukimya kisha,kilichiofuata ni kelele kutoka kwa Dogo, kikao kikagawanyika katikati, wapo walioniunga mkono akiwepo Baba, Mama yangu, na Dada yangu, lakini Kaka Mkubwa, Baba mdogo na mama Mdogo wakaungana na Dogo.
Siku ikaisha, dogo akaondoka nyumbani akaenda kwa Baba Mdogo Anakaa Majengo.
Jana jioni karudi, amenuna mno, hataki kuongea na mtu. Nikamuita, tukazungumza kwa kirefu kama lisaa na nusu. Mbaya zaidi ananiambia huyo mrembo anamtoto mmoja. Hapo ndio nikawambia kabisa sio kwenye mahari tuu sitaenda,, hata kwenye harusi yako sitakuja, na wala sitakuja kwako kabisa, na wala usinihusishe na mambo ya nyumba yako.
Aliponiuliza kwa nini, nilimuelezea sababu nyingi sana, tuliongea mpaka saa sita za usiku
Leo asubuhi wakati tunapara kifungua kinywa, alizungumza maneno mafupi sana.
" Naombeni mnisamehe. Nimewaelewa"
Sikukuu ndio kesho, familia imeamua hakuna wakupinga.
Jokajeusi