inakaa wapi?.......wakati katika balehe nimepiga bao kibao ndotoni....
Wala tusibishane, naomba kifungu iwe kwenye kitabu chochote kile wala sio bible pekee yake, usijesema nimeku-limit
Mkuu kwani umeisoma biblia ukaimaliza?
Mwanaume anayo bikira, lakini siyo ya kuonekana kwa macho,
ni ya ulimwengu wa Roho...
Kitendo cha Neno la Mungu kusema USIZINI
ina maana unapozini kuna jambo linatokea katika mwili na katika Roho,
ambalo linaleta uharibifu juu ya wanaozini....
Huwa sisi kama wanaume tumekuwa wepesi wa kuwalaumu na kuwanyooshea vidole wanawake kwa sababu bikra zao zinaonekana kwa macho...kwa hiyo akiwa hana anajulikana na kutambulika
Lakini tunasahau kwamba hata Mwanaume anapozini kwa Mara ya kwanza kuna UNAJISI unatokea juu ya mwili wake na Unajisi huo unaharibu mpaka rohoni, yaani Bikra yake (usafi na Utakatifu) ambao chanzo chake ni Ulimwengu wa Roho unakuwa umeondoka, na madhara yake yapo.
Unapozungumzia Bikra ni jambo la Kiroho kwanza kabla halijawa la Kimwili...
Ni kweli kabisa kama ulivyosema Madhara hayo ya kutokuwa na bikra kwa mwanamke ni makubwa na ya Aibu zaidi kuliko ilivyo kwa mwanamume kwa maana Alama pekee ambayo inayobaki kwenye mwili wa mwanamume na ikaonekana kwa macho ni Tohara...
Ila ujue wanaume nao wanayo Bikra na wanaume nao pia wanatiwa unajisi na wanawake na hili limeandikwa katika Biblia kitabu cha;
(Ufunuo 14:4)
Biblia inaeleza wazi.