Maandalizi ya mkutano wa UKAWA/CHADEMA uwanja wa Jangwani

Maandalizi ya mkutano wa UKAWA/CHADEMA uwanja wa Jangwani

Status
Not open for further replies.
Kuna watu wanasema watalala jangwani hasa wa kutokea mikoani wanaoletwa na CHADEMA ambao CHADEMA haina pa kuwalaza kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni kesho.

Sina tatizo la wao kulala viwanjani hofu yangu umati mkubwa kulala pale kipindi hiki cha kipindupindu si sahihi kabisa.Pale hakuna huduma za kiafya za kueleweka.Hebu fikiria hayo mafuriko yatakayolala yaanze kuharisha kwa kipindupindu usiku halafu yaambukize kipindupindu kwa mafuriko yatakayokuwemo kesho ikiwa ni pamoja na mgombea uraisi na mgombea mwenza si itakuwa hatari jamani.

Nashauri serikali ipige marufuku umati kulala Jangwani leo.

unahitaji ukombozi wa fikra nadhan hata kwenye baraza lenu la umoja wa wanawake wakutoe tu maana unadhalilisha wanawake wenzako kwa kuwa na fikra fupi.
 
Timu ya maandalizi ya uzinduzi wa kampeni za urais kupitia CHADEMA(UKAWA) imepanga kuteka anga la Fikra za watanzania kwa masaa matatu mfululizo kuanzia saa 9 mchana, Jumamosi(29/8/2015) wakati mgombea urais wao Edward Lowassa atakapofanya mkutano mkubwa wa kwanza wa kampeni za kuelekea Ikulu katika viwanja vya Jangwani.
Hapa chini ni baadhi ya mipango yao.

*MALENGO
-Idadi ya watu zaidi ya Laki tano wanakusudiwa kuhudhuria mkutano huo pale Jangwani.

-Zaidi ya watanzania milioni 20 wamekusudiwa kufuatilia tukio hilo kupitia Luninga, Redio, Mitandao nk.

-Mwelekeo mzima wa Sera, Ahadi na kampeni za UKAWA mwaka huu kuwekwa wazi.

-Watanzania wote kujua Agenda na mikakati ya UKAWA watakapo ingia madarakani.

*MIKAKATI
1/Kutumia uwanja mkubwa wa Jangwani ili uweze kutosha Idadi kubwa ya watu, Maegesho ya Magari na Usalama wa kutosha.

2/Kufunga vipaza sauti sehemu zote za uwanja
ili kila mtu apate kusikia, pia kufunga Kamera kadhaa kuzunguka uwanja wote ili kufuatilia mwenendo mzima wa watu, usalama na matukio.

3/Kurusha matangazo ya moja kwa moja(Live) kupitia Vituo vikubwa 4 vya Luninga, Redio kadhaa, Mitandao (Live streaming, Update details nk)

4/Kuhamasisha watu wengi zaidi wasiokuwepo majumbani kufuatilia tukio hilo popote walipo kupitia Redioni kwenye Magari, bodaboda, Simu za mikononi na pia kwenye mabaa, hotel, migahawa, maeneo ya kazi nk kupitia Television.

*CHANGAMOTO.
(A)KUKATIKA UMEME.
Inategemewa maeneo mengi ya Dar na mikoa kadhaa huenda umeme wa Tanesco ukakatwa kuanzia saa tisa mchana, hivyo watu wanahamasishwa kuweka mipango yote ya Dharula ya nishati.

(B)MAKUNDI YA WAHUNI
Zipo tetesi za uhakika zinasema kuna makundi fulani ya vijana waliopangwa na Chama fulani ili kuja kuvuruga mkutano kwa kuleta taharuki, taarifa hizo zinafanyiwa kazi.

(C)VYOMBO VYA DOLA
Zipo taarifa kuwa Polisi pia wamepangwa kuja kuleta vitisho na Taharuki kabla ya mkutano na wakati wa mkutano. Moja ya tetesi inasema Daladala zote zitazuiwa na jeshi la Polisi kushusha watu kituo cha Jangwani au kuingia maeneo ya uwanjani kushusha abiria na watu hawataruhusiwa kutembea kwa makundi makundi kufika uwanjani, lengo ni kuwakatisha tamaa watu wanaokwenda mkutanoni.

(D)KUKATISHWA MATANGAZO
Zipo habari zinasema huenda matangazo ya Television yakakatishwa ghafla wakati mkutano ukiwa unaendelea(Tetesi zinasema NEC wamepanga kuwaeleza wamiliki wa Vyombo vya utangazaji kukatisha matangazo yote mara tu inapofika saa 12 jioni, kwa kuwa muda wa kampeni utakuwa umekwisha kisheria)

SOURCE:Team Lowassa.
 
Hakuna mwana siasa alie na dini,kwa waislamu wezangu heri mtawala awe
Najash muadilifu
kuliko Abusufiani au

au HAJJAJI BIN YUSUF .Kikwete kawatia ndani mashekh ambao wanamswalisha
Na walimpa kura wakati wa uchaguzi dhidi ya Slaa wa CDM.Wakaziita kura maslahi,
Leo fadhila ya punda kawatia mdani na kuwafanyia uovu wa kuwanajisi.
Mzee Mwinyi nae hivyo hivyo waislamu hatukuwa raha ,mashekh walipigwa na kuburuzwa jela na wengine kuuwawa
Bora nyie waislam mfunguke sababu ccm wamewatumia sana na wakati huu hawana hoja ya udini wala ukabila sababu UKAWA ni Muungano wa vyama vingi na wanaushwawishi katika makundi yote juu ya hapo Lowassa anakubalika na kila imani.
 
😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃
 
wao wameona hiyo ndio mbinu...

CCM na viongozi wake walitakiwa kukaa chini na kujiuliza kweli tatizo ni LOWASSA??Au tatizo ni watu wamechoka hali halisi ya namna ambavyo nchi inaongozwa??

Kama ni Lowassa,basi kwanini bado wengi wanaprefer Lowassa kuliko Magufuli pamoja na record yake mbaya lakini wako tayari kumpa uongozi??

Badala ya kupiga watu wangekaa chini wajiulize.Badala ya kuendelea kuwatukana UKAWA wangekaa chini wajiulize nini kimewasibu hawa WADANGANYIKA aka WAPUMBAVU na MALOFA...
 
yan magamba mnaweweseka, kwann unateseka hvyo amia UKAWA il uishi kwa aman
 
Nitashangaa mleta mada km sio Mtt wa MAGUFULI basi utakuwa wa JK kwa jinsi unavyoipenda CCM kwa wema gani ulionao hadi uwaonee huruma jamaa wa UKAWA
 
Ben mkapa angalau aliwakumbuka waislamu kwa kuwa chuo kikuu cha morogoro.
Huyu kikwete yeye na Mwinyi ndio walioidhinisha memorandam of understanding kati ya
serikali na ka nisa.Sasa anaedhani kuwa viongozi waislamu
Watasaidi kutatua madai yetu,si kweli.
Mimi nadhani MKIRISTO anayejiamini mwadilifu
ni bora kuliko muislamu moga,asyejiamini
tena mbadhirifu anayeogopa watu fulani
 
Kwa kuwa muda unaweza kuwabana ukawa kesho na mambo ni mengi bora shamra2 zianze saa 4 asbh ukizingatia kuna wageni wanatambulishwa na kuwapa wajumbe nafasi ya kutoa salaam na burdani. Isiwe kama Ccm walivyoshindwa manage time wakapitilza na kukiuka sheria ya Nec
 
Naiweka kama nilivyotumiwa na Classmate wangu.


Wana 4U movement mkoa wa kilimanjaro kma ambavyotumekubaliana kwenye kikao chetu juu ya kwenda dar kwenye uzinduzi wa kampeni za lowassa tutaondoka moshi mjini saa 12 jioni
Tutaondokea Mekuz na viongozi wa msafara watakuwa makamanda wetu fredi mushi na Paul matemu tuwah jamani
Tumeamua kuondoka mda huo ilitupite usiku kwa usiku wasione kma lowassa ametoa watu mikoani lkn pia tulishakubaliana tutampa kila mtu nauli yake ya daladala ilituingie jangwani kwa daladala kuwaaminisha watu kuwa tumekwenda kwa mapenzi yetu. Msisahau majina ya hoter zenu mtakazofikia ukisahau wasiliana na mratibu wako.
Maelekezo mengine mtapewa na viongozi wenu


By Dr Juma Mwininga
Mratibu Mpya Wa 4U movement na Team lowasa Kitaifa

Nipo Moshi nitaenda kuthibitisha hyo saa 12,km ni kweli nitaandika hapa na km sio kweli aisee utajuta.
 



Lowassa 🌀🌀 Mabadilikoooo.. x 2

Mabadiliko 🌀🌀 Lowassaaa x 2

👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇

FOUNDER, & the MOST GENIUS HUMAN BEING currently in Tz politics....!!!!


Kamanda wa Anga, Field Marshal Mboweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee...!!!
 
Nipo Moshi nitaenda kuthibitisha hyo saa 12,km ni kweli nitaandika hapa na km sio kweli aisee utajuta.

Watakuwa wameshaambiana kuwa tayari limebuma tukutane sehemu ingine!
 
pole wewe unayeishi kwa hofu
LOWASA NI KIONGOZI. MKWELI WA DHAMIRA,
Alipoona ofisiyake imeshutumowa kwa kosa la
ufisadi kajiuzulu ili sheria ifuate mkondo wake
huu ndio aina ya uongozi tuohitaji.WATANZANI
LOWASA NIWADILIFU NA MKWELI.
Hana sifa za ulaji rushwa wala ufisadi.Alibambikiziwa
zengwe na wakubwa zake wa kazi ikabidi awe kondoo wa kafara
KIKWETE ANALO JAMBO DHIDI YA LOWASA.
Masikini Makufuli,anabebeshwa zigo la uovu wa ccm afe nalo shingoni
 
KUKATA UMEME KWA MASAA 3 KWA ENEO KUBWA LA NCHI BILA SABABU ZA KIMSINGI NI HASARA KIASI GANI? KWA SHIRIKA!NA KWA TAIFA LETU?

FIGISU FIGISU ZA CCM!

why kidish like that!
""UTOTO""
 
Kuna watu wanasema watalala jangwani hasa wa kutokea mikoani wanaoletwa na CHADEMA ambao CHADEMA haina pa kuwalaza kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni kesho.

Sina tatizo la wao kulala viwanjani hofu yangu umati mkubwa kulala pale kipindi hiki cha kipindupindu si sahihi kabisa.Pale hakuna huduma za kiafya za kueleweka.Hebu fikiria hayo mafuriko yatakayolala yaanze kuharisha kwa kipindupindu usiku halafu yaambukize kipindupindu kwa mafuriko yatakayokuwemo kesho ikiwa ni pamoja na mgombea uraisi na mgombea mwenza si itakuwa hatari jamani.

Nashauri serikali ipige marufuku umati kulala Jangwani leo.

Politically DEAD!! HUJISTUKII HATA
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom