Silaha hazinunuliwi kama makontena ya mabakuli kwamba unaagiza tu ukiwa na uhitaji. Niko busy na nina uvivu wa kuandika hapa ila kwa kifupi ni kwamba S-400 wala Su-35 hazijaenda Iran. Wanahitaji si chini ya miaka miwili kuanza kupata Su-35 wakiagiza leo, wanahitaji angalau miaka miwili au mitatu wakisaini S-400. Mpaka mwaka huu hakuna deal lolote kati ya hizo systems mbili ilikuwa imesainiwa.
Russia mwenyewe yuko overwhelmed na matumizi ya hizo silaha frontline kiasi kwamba nchi kadhaa zilizoweka order Urusi zilisitisha kutokana na kuchelewa, kila silaha inaundwa inatumiwa na Urusi vitani. Nyingine sanctions zimechelewesha kutafuta alternatives.
Alafu kampuni za silaha hazifyatui tu kama nguo. Kama hamna order hawaundi, sasa hizo silaha za kwenda Iran wamezipata wapi.