Mabachela: Ni chakula gani kigumu kupika geto?

Mabachela: Ni chakula gani kigumu kupika geto?

Kuna wakati naangalia movie nacheki msela anaingia jikoni anakaangiza anachukua anaweka dining anagonga. Kama raisi vile. Niige sasa niingie mlimani city ndo balaa linaanza. Vitu vitakaa kwa friji hadi nagawa.
 
Mi naweza vifuatavyo

Ugali
Wali
Maharagwe
Nyama
Kuku
Viazi
Ndizi
Mchicha
Spinach
Chinese
Mayai
 
Kupika najua karibia vyakula vyote na hata nisivyojua nikijifunza nafahamu fasta,tatizo uvivu,kupika chakula cha mtu mmoja au wawili kwangu ni changamoto,naona natumia muda mwingi kupika alafu nakula dakika tano tu,bora kununua mgahawani
 
Mimi mgahawani napapenda sana sema kuna wakati unataka ucheze draft kama la home ndo shida inapoanzia. Lazima kuna kete itakuwa shida kusukuma.
 
Daaaah wali wa kupika kwenye jiko la gesi unazingua sana ukibugi kidogo tu ukajaza maji ni shida kitu kinatoka bokoboko na jiko la mkaa kuanza purukushani za kutafuta mkaa miyeyusho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wakati namkumbuka sana mama. Na wale wadogo zangu wadogo!!! Kale kawimbo kananiingia kuwa " sadikii sasaa ashibaa chakula kingi nyumbani" dah
 
Back
Top Bottom