Mabachela wenzangu, mnapika vyakula gani vya haraka haraka?

Mabachela wenzangu, mnapika vyakula gani vya haraka haraka?

Tuko wengi,labda nieke kikiwa kibichi na kisikae mda mrefi 3_4days.Utakuta watu wanasema unachemsha maharage mengi yaweke kwenye fridge inabaki kuunga Tu lakini sioni kama yanakuwaga mazuri.Mi kila nnapotaka kupika maharage napika naunga tunakula yanaisha,nkihitaji ntachemsha tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
Haswaa! Yani maharage uyale siku uliyoyachemsha na kuyaunga bana. Sasa mie ili kuepuka kero naendaga chukua kwa mama muuza. Yeye anayapika fresh kila siku.
 
Weka wali kweny ricecooker weka chai yako pemben wali ukiiva pakua weka kweny feni upoe fasta ukishapoa chukua chai piga fasta au unaweza nunua ndondo kwa mamantilie ukija unamwagia juu unapiga

Ukichoka wali chai nunua kiungo cha pilau cha 100 na mshikaki wa jero changanya kwenye ricecooker vizur vikiiva ni pilau tayar halina mbwembee chukua nyanya moja kata kata piga shushia na maji

Mm nilijenga urafiki na wale wamama wanaouza mboga za majan so nikitaka nampigia simu ananikatia katia kabisa nikichukua nikuosha weka kwenye jungu chukua nyanya moja kitunguu changany vyote na mafuta wela vyote zungusha dk 6 had 8 tayar



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila ukitembelea supermarkets kuna zile frozen foods...

Wewe unakuja kukangaa tu au kuja kumalizia kupika kidogo jaribu hivyo...



Cc: mahondaw
 
Weka wali kweny ricecooker weka chai yako pemben wali ukiiva pakua weka kweny feni upoe fasta ukishapoa chukua chai piga fasta au unaweza nunua ndondo kwa mamantilie ukija unamwagia juu unapiga

Ukichoka wali chai nunua kiungo cha pilau cha 100 na mshikaki wa jero changanya kwenye ricecooker vizur vikiiva ni pilau tayar halina mbwembee chukua nyanya moja kata kata piga shushia na maji

Mm nilijenga urafiki na wale wamama wanaouza mboga za majan so nikitaka nampigia simu ananikatia katia kabisa nikichukua nikuosha weka kwenye jungu chukua nyanya moja kitunguu changany vyote na mafuta wela vyote zungusha dk 6 had 8 tayar



Sent using Jamii Forums mobile app
Umetisha sana mkuu, hiyo wali chai unamaanisha wali mkavu na chai??, dah hilo pilau sasa 😀😀😀
 
Nimekula mboga ya bachelor leo aiseeee imejaaa pilipili kama tuko Bombay

mama wawili
 
Ugali na mayai..
Unapiga ugali, unapika mayai. Ugali unalia kwenye sufulia na mayai unachanganya umo umo.. Flampeni kwa mwezi inaoshwa mara moja sababu huwa haichafuki.
Unakuwa na kazi ya kuosha sufulia tu
Hii ya ugali mayai huwa naipiga sana

Ugali sembe ukubwa wa ngumi

Mayai manne au matatu nayachanganya na nyanya kitunguu karoti hoho nakoroga

Naweka we frying pan au sufuria fasta sana

Nakataa ugali wangu imetoka hio[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vyakula visivyo na mlolongo mrefu wa kuandaa na vyombo vichache sana vitumike. Nimechoka ubwabwa (wa rice kuka)/tambi/ugali na nyama au mainiau mchemsho. Vitu gani vingine huwa mnapika?

Asanteni
Nyanya moja +yai moja = mboga. Songa kaugali. Jibu ni mlo
 
hili suala linatesa nimejaribu kwa muda naona sasa limeshafika ukingoni aisee
vyakula naweka kwenye friji kesho yake namwaga nlikua siwezi kuvirudia
narudi usiku nataka kupika mara kiberiti nimesau kununua nazungusha zungusha cha kuwashia gesi labda itajisau itawaka holaaa naamua kuchukua beer 2 nakunywa nalala.

Kuna sehemu nilikua nakulaga kuna mdada alikua yupo vizuri ikatokea tukawa marafiki nikamjaribu kama anaweza kuwa anakuja kunipikia mtoto akakubali mi nikumpa tu menu ya jioni na asubuhi/chai.

Ila sasa naona ntanasa kwa kupika na kupakua huku mabachelor wenzangu maana mtoto siku nyingine anadondosha kabisa hapa duuh.
 
Ugali na yai la kukaanga,huu n msosi ambao HUWA nauandaa nikiwa nimechoka afu Nina njaa
 
Vyakula visivyo na mlolongo mrefu wa kuandaa na vyombo vichache sana vitumike. Nimechoka ubwabwa (wa rice kuka)/tambi/ugali na nyama au mainiau mchemsho. Vitu gani vingine huwa mnapika?

Asanteni
Mchemsho wa ng'ombe - j3
Mchemsho wa kuku - j4
Mchemsho wa mbuzi - j5
Nyama choma ng'ombe alhamis
Nyama choma mbuzi - ijumaa
Nyama choma kuku - j.mosi
J.pili unaweza choma kitimoto au ukapika mtori wa ng'ombe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kupika kipaji bna mi geto kwangu hakuna Sahani wala kijiko kuna glass tu ya kunywea Pombe, Mambo hayo siwezi aisee kuanza kuhangaika na Kuosha vyombo msosi wenyewe unapika hauna radha tabu ya nini sasa, Wakati nipo chuo kuna demu alikuja na calculation zake za saving nkaona isiwe tabu nkampa hela akaenda kaleta mavitu kibao geto hafu sasa yeye alikuwa anaishi hostel za chuo ivo geto anakuja mara chache chache alichokuwa anakikuta na analalamika vitu vinaharibika mana sikuwa ata na friji labda masela wakija ndio wavipike ivo vitu, mimi ilikuwa jumamosi au jumapili tu asubuhi ile naamka naliamsha Dongo (Ugali) mkubwa nanua na nyama buchani nachemsha chukuchuku bila nyanya wala nini Napiga foundation ya kutosha hapo sasa Nikwenda kutafuta Ugimbi mana tumbo liko full.
Mpaka sasa mimi najua kupika ugali mzuri sana kuliko chakùla chochote.
Sema kuna comments nimesoma yani mtu uishi kwa kula matambi tu sijui soseji mara chips mara sijui viazi tu mwingine anasema nunua mikate uweke ndani aiseee mimi siku mbili bila ugali sielewi kabisa, najua ugali hauna faida sana mwilini ila ndio na mix sasa na matunda hayo kama chipsi, Wali, Mboga za majani kwa mbali ili ni pate virutubisho muhimu ila wanga still ni muhimu kwa energy
 
Mm pia kupika ina nichosha hasa nikiwa alone nikipika chakula hakina radha kabisa nahic mateso nabaki tu kununua msosi kwa Mama ntilie simple tu,nikiwa nataka kula chakula nikipendacho naweka order kwa mazaa wa chakula mapema tu nampa ela yake ya msosi ,siku inapita fresh hakuna kupoteza mda,
 
mseto wa karanga
mahitaji: karanga mbichi1/4 kilo
mchele 1/2 kilo
osha karanga zako vizuri, pima maji wastani kwenye sufuria , weka karanga hizo, chumvi na mafuta, funika vichemke kama dk 10, kisha weka mchele wako huko , hakikisha tuu wali wako haukauki saana, huu msoc unaezapiga na chai au maziwa na ni fasta tuu
 
Mi.nakushauri mboga ya fasta. Dagaa zilizokaangwa, kachumbari yenye matango na caroti ukiweza mix na parachichi ndani yake, haina haj yakupik jikoni jipe dakik kdha tu wakati maji ya ugali yanachemka we fanya kuuchanganya mchanganyiko wa mboga zako... utanishkuru maana hadi mchuzi ni humo humo. NB ugali kula ukiw wamoto maan mboga zitakua za baridi!

Kwa haraka utakua umepika ugali only. Hiyo ni mchana.

Usiku tafuta chombo cha plastiki chenye mfuniko. weka mchele wako uliouosha changnya chumvi na mafuta humohumo then funik chombo chako katika sufuria la maji yanayochemka, baada ya hapo unawwza kurudi JF ukaendelea kuchati mpaka km nusu saa au lisaa hivi unaweza kuutoa mchele wako ukiwa wali tayari Na maji ukayatumia kwa mishe nyingine, hapo najua mboga hauwezi kosa, unanunua maharage ya shng 500 tuu kama upo Dar!

NB: jribu kwanza ukiwa umeshiba!!
 
Back
Top Bottom