Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria

Kassimu majaliwa unapewa ujumbe hapa. Je unapwaya au hawakutaki? kwanini umepewa msaidizi Tena kinyume cha katiba?
Lakini uteuzi huu wa naibu waziri mkuu na huyo mnyeti ni danganya toto kwa wasukuma ambao wameoneka kuwa na mwitikio mkubwa katika oparesheni za Chadema na ni dhahiri hawataki kusikia kuhusu sa100.
 
Rais anao uwanda mpana wa kubadili wizara na kuwaweka Mawaziri kwa kadri atakavyo.

Kwa uzoefu wangu sikuwahi kusikia Kiongozi aliyewahi kuwa Naibu Waziri mkuu.

Hata hivyo kama Rais ana Makamu wake iweje Waziri mkuu asiwe na Naibu?

Nilipochanganyikiwa zaidi ni Kiongozi mmoja kuwa Naibu Waziri na Waziri ktk serikali hiyohiyo. Inawezekanaje?

Kwamba Pale bungeni na huko mitaani hakuna wanachama wa CCM wenye weledi kiasi cha kumtwisha majukumu mazito ndugu Dotto?

Tuombe Mungu uteuzi huu uwe na malengo ya kuimarisha ustawi wa wananchi wote na si kumdhoofisha mtu flani kwa manufaa ya watu wachache.
 
Huyu mama utawala wake itakuja kuwa na makosa mengi sana na skendo kibao. Tujipe muda maana inaonekana kama mama anashauriwa vibaya yaani "Anapigwa saundi" na anakubali.
 
Mwinyi awamu ya pili alimteua mrema kuwa Naibu waziri mkuu sasa awamu ya sita kaja na Naibu waziri mkuu tena.
 
Rais angejiuzuru tuchangue mtu anayejielewa. Huwezi kuteua cheo ambacho hakipo kikatiba
Lakini japo hakipo kikatiba, lakini kilishawahi kulazimishwa kipindi kile cha Rais Mwinyi, akamteua Mrema!! Mrema kuwa naibu waziri mkuu!! Mrema Alipoteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani alikuwa anaingilia kila wizara kama akinusa kuna harufu ya ufisadi. Mawaziri wakawa wanamlalamikia kuwa anaingilia wizara zao!! Mwinyi alipoona hivyo akaamua kumfanya Waziri wa mambo ya ndani na naibu waziri mkuu!! Kwa nafasi hiyo alikuwa na mamlaka ya kuhoji utendaji na ubadhirifu kwenye wizara yoyote!! Mrema alifanya kazi hiyo kwa mafanikio sana!! Hilo ndilo lilikuwa ni lengo. Tujiulize kwa leo lengo ni lipi?
 
Nadhani marehemu Lyatonga Mrema aliwahi kuwa Naibu Waziri Mkuu kama sikosei
 
DP World imembeba Jerry Silaa
Huyo mtoto yupo kwenye Circe yao kitambo, ameshakuwa meya wa Ilala na mjumbe wa Kamati kuu ya Ccm, huwezi kupata hizo nafasi hivihivi.

Ingekuwa upambe tu unalipa hata Pascal Mayalla angepata uteuzi lakini wapi hata ukuu wa wilaya hajawahi kufikiriwa pamoja na kujitowa akili kote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…