Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria

Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria

Hivi kwa nchi zetu hizi za Afrika ambazo zina lundo la nafasi za uongozi na bado ni masikini ambapo wengine wanasema umasikini wetu umesababishwa na laana, wengine ni utamaduni wa kutopenda kazi na mifumo mibovu ya kubana mafisadina kuleta uwajibikaji;

Kuna ulazima gani kuwa na nafasi ya Naibu Waziri Mkuu?
wacha ugaidi na upotoshaji
 
Naona hujaielewa dhanna ya Reform and Rebuilding.


Hapo kwa Kassim Majaliwa, kilichositisha asipigwe chini ni mfumo tu, lakini ana "underperform" sana, juzi aliambiwa, usingoje maagizo kutoka juu.
Nakuelewa sana mama.!
 
Ulifanya vizuri kule Utumishi na ulisaisia sana kusimamiwa Haki za Watumishi.

Huku Tamisemi ndio Kuna uonesi zaidi , nadhani Watumishi wamepata mtu wa kumlilia shida wakasikilizwa.
 
Watoto wawalala hoi ambao ndio wajenga nchi kwa kodi wanazotoa wanazidi kusota mitaani kwa kukosa ajira,badala ya kupanga mipango ya kuwanusuru na msoto wa kukosa ajira ndio kwanza wanafikria mbinu za kupeana ulaji wenyewe kwa wenyewe,naibu waziri mkuu ndio nini kama siyo kupeana ulaji?wakati hata cheo cha makam wa rais nacho hakina tija yoyote kwa nchi.
Nakumbuka hata Kibaki aliwahi kutengeneza hicho cheo cha naibu PM na kumpa Uhuru Kenyatta, enzi hizo walipounda serikali ya mseto baada ya kutokea mgogoro wa uchaguzi na Odinga akawa PM. Utaona kwamba kuunda hiyo nafasi kunalenga kumkwepa PM na kumtumia naibu PM...........kwa maneno mengine Maja atabaki kuwa PM jina.​
 
Acha ujinga. Huyu ndo mkombozi wetu baada ya kuteswa na jiwe miaka mitano bila mishahara kuongezeka Wala ajira mpya zozote. Sasa hivi ajira ni kila pahala hasa sector binafsi ambayo ilikuwa imekufa kabisa kifo Cha Mende.

Sasa hivi utalii inaajiri kwa Kasi mno na waliosoma tourism wanasema mama has rescued them. Sector ya bank inaajiri kwa mamia kwa Sasa baada ya kupulia mashine k a miaka mitano ya jiwe.

Mpaka ameamua kuwarudishia pesa zilizoobwa kwenye akaunti za Hawa wamiliki wa bureau de change. Sasa hatusikii watu kuuawa ovyo ovyo na watu wasiojulikana.
Wacha ugaidi na Upotoshaji wa Makusudi.

Ushindwe
 
Rais Samia Suluhu amefanya mabadiliko na teuzi za sura mpya kwenye baraza la mawaziri. Uapisho utafanyika September 1, Ikulu ndogo Zanzibar saa tano kamili asubuhi.
1. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Doto Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Awali alikuwa Waziri wa Madini.

2. Amemteua January Makamba kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Awali alikuwa Waziri wa Nishati.

3. Amemhamisha Balozi Pindi Chana kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Awali alikuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.

4. Amemhamisha Steven Byabato kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Awali, Byabato alikuwa Naibu Waziri wa Nishati.

5. Amemteua Jerry Silaa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Silaa ni Mbunge wa Ukonga, Dar es Salaam.

6. Rais amemteua Anthony Mavunde kuwa waziri wa madini, mwanzo alikuwa naibu waziri wa kilimo.

7. Prof Makame Mbarawa aliyekuwa waziri wa ujenzi na uchukuzi amekuwa waziri wa uchukuzi.

8. Innocent Bashungwa amekuwa waziri wa ujenzi, mwanzo alikuwa waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa.

9. Godfrey Kasekenya aliyekuwa Naibu waziri wa Ujenzi na uchukuzi ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa Ujenzi

10. Alexander Mnyeti ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa Kilimo

11. David Mwakiposa Kihenzile ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa Uchukuzi. Ni mbunge wa Jimbo la Mufindi

12. Judith Kapinga ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa nishati, ni mbunge wa viti maalum Ruvuma.

13. Dunstan Kitandula ameteuliwa Naibu Waziri wa maliasili na Utalii, ni mbunge wa Mkinga

14. Stergomena Tax amehamishwa wizara ya mambo ya Nje kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

15. Angellah Kairuki amehamishwa kutoka TAMISEMI na kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii

16. Dkt. Damas Ndumbaro amehamishwa kutoka Wizara ya Katiba ba Sheria na kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.




View: https://www.youtube.com/watch?v=7bLEuvgVGG4

======

View attachment 2733279
View attachment 2733280
View attachment 2733281
View attachment 2733282

Naibu Waziri Mkuu Hiki cheo kiko kikatiba?
 
Back
Top Bottom