Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria

Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria

Haya, someni hapa

1C27DC7E-8889-4294-B782-167B8BC88604.jpeg
5DF333FD-BE22-4698-8140-26FCA62C2A93.jpeg
 
Membe alikuwa wizara gani?
Iyo hiyo aliko JM sasa..

Hata hivyo, najua unakoelekea. Kwamba, mbona sasa hakuwa Rais?

Dr Matola PhD, succession plan ya Jakaya Mrisho Kikwete ilikuwa Benard Membe ndio apokee kijiti..

However, Edward Lowassa alivuruga mipango hiyo kwa sababu ya makosa ya JK mwenyewe. Aidha nguvu ya CHADEMA by then ilikuwa ni tishio kuu kwa CCM..

Baada ya plan A kuvurugika, ilibidi itengenezwe plan B haraka na Bwana John P. Magufuli akawa ndiye better option ya CCM na jamaa ndio hivyo akawa ameokota embe dodo chini ya mgunga..!
 
Mtaniuliza vipi kuhusu Sukuma gang kurudi ulingoni, hilo nahitaji niwaambie tu ukweli kuna CCM asilia na CCM wajaji sasa asaivi chama kiko kwa Asilia na hawatarudia tena lile kosa la 2015 labda itokee dhoruba itakayoondoa kizazi chote hiki, Gang hawaji kuinuka tena habadani.

Mshauri wa masuala ya ndani sana.

Kuna siku mtanielewa tu.
 
Analipwa kwa kutumia kigezo gani?
Kikatiba nafasi hiyo haipo. Naibu Waziri Mkuu haingii katika Baraza la Mawaziri.

Sijui wanagawana vipi mapesa kwa jina la mafao lakini najua kuna kitu kinaitwa 'presidential appointees'
Hawa wana mafungu wanayolipwa ! Tunahitaji Katiba kuweka mambo sawa

Fikria kwamba Mbunge analipwa kiinua mgongo kila baada ya miaka 5. Akikaa Bungeni miaka 10 ,15 au 20 analipwa kila baada ya miaka 5. Hivi kazi gani nyingine tena unayoweza kupata ladha na utamu kama huo.
Ukiwaona wapo kimya Dodoma si kwasababu wana nidhamu ni kwasababu asali imewakolea wanahofia kupaliwa.

Tunahitaji Katiba ili kuweka mambo sawa. Kwanini Mbunge akopeshwe V8 na sehemu ya Mkopo walipe Wananchi tena kila baada ya miaka 5. Tuna tatizo kubwa sana , tunahitaji Katiba

JokaKuu
Kama cheo hakipo kikatiba Ila bado kinaundwa kwa hoja kuwa 'Rais ana madaraka ya kufanya hivyo kwa katiba hiyo hiyo isiyokitambua hicho cheo' hilo ni tatizo kubwa mno.

Naibu PM haingi baraza la mawaziri Ila bado itabidi awepo kwa kuwa ni waziri wa nishati...maajabu haya

Katiba hii ya mwaka 1977 haiendani kabisa na wakati tulionao huo ndio ukweli.

Pascal Mayalla JokaKuu zitto junior
 
Kama cheo hakipo kikatiba Ila bado kinaundwa kwa hoja kuwa 'Rais ana madaraka ya kufanya hivyo kwa katiba hiyo hiyo isiyokitambua hicho cheo' hilo ni tatizo kubwa mno.
Jibu lako ni lina sehemu mbili '' YES and NO'

Yes kwasababu Katiba haikutaja cheo cha Naibu Waziri Mkuu.

No kwasababu Katiba haikuzuia kuanzishwa kwa cheo hicho kama ilivyotoa haki ya kugawa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuwa Wizara Mbili. Katiba isiyomtaja Naibu Waziri Mkuu imempa Rais madaraka ya kuunda Wizara kwa kadri anavyoona inafaa.

Kuna 'conventional wisdom' kwamba kitu ambacho hakikutazwa kisheria basi kimeruhusiwa kisheria.
Naibu PM haingi baraza la mawaziri Ila bado itabidi awepo kwa kuwa ni waziri wa nishati...maajabu haya
Hapa ni suala la ufundi. Rais alijua kwamba Naibu Waziri Mkuu kama Manaibu wengine na kwa kuwa hana nafasi kikatiba hataweza kuingia Baraza la Mawaziri. Rais anafahamu ili awe ''effective' Naibu Waziri Mkuu ni lazima ahudhurie vikao ambavyo yeye ana hadhi kuliko Mawaziri. Njia aliyotumia ni kumpa uwaziri wa Nishati ili aweze kuingia katika Baraza la Mawaziri
.
Again, hakuna sheria aliyovunja kwasababu kilichompa nafasi ya kuunda Baraza la Mawaziri kwa kadri anavyoweza hakikumzuia kumpa mtu Naibu na Waziri Kamili at the same time ili atumie mwanya huo kuingia katika Cabinet.

Hali za 'ujanja ujanja' ni utamaduni wa Serikali za CCM, lakini si unique. Ikiwa tutamlaumu Rais tutakuwa hatumtendei haki kwasababu kuna mauza uza mengi katika jamii tunaishi nayo.
Mfano, polisi kumkamata mtu Ijumaa ili alale hadi Jumatatu ni mkomoeni lakini hawajavunja sheria kwasababu hatuna mahakama za wikiendi. Polisi hao hao watampeleka mtu kwa ofisi ya DCI halafu wanamrudisha Magereza kwa siku nyingine kwasababu saa 24 zinaanzia pale alipotoka kwa DCI

Ni mauza uza kama yale ya Wakurugenzi kufunga ofisi na kutoweka kabla ya muda wa kurudisha Form
So kuna mengi hili la Naibu Waziri Mkuu ni sehemu tu ya mauza uza
Katiba hii ya mwaka 1977 haiendani kabisa na wakati tulionao huo ndio ukweli.
Siyo kwamba haiendani ni kwamba haifai hata kwa bahati mbaya. Ukiisoma utabaki na maumivu ni afadhali usi isome kabisa. Mfano, Katiba hii haimzuii Rais kuwa na Baraza la Mawaziri 50 akitaka. Katina hii inamtambua Rais kama Amir Jeshi Mkuu lakini akiwa Zanzibar ni Amir Jeshi Mkuu Mwenza. n.k.

Katiba ya 1977 inatambua uwepo wa Wabunge na muda wa kutumikia. Katiba hiyo hiyo haielezi lini Mbunge anapaswa kupewa kiinua mgongo. Wapo watakaosema kuna sheria zinazohusu hili, lakini pia katiba ina sehemu imetaja masilahi ya Wafanyakazi fulani. Kwahiyo Katiba haikuweka ukomo wa Ubunge , kinachotokea kila miaka 5 wanazoa kiinua mgongo, akirudi tena kiinua mgongo akirudi tena kiinua mgongo.


Tunahitaji Katiba mpya sasa . Kenya katiba yao ina ukomo wa Idadi ya Baraza la Mawaziri na Watendaji.
Ruto alijaribu kuweka makatibu, Mahakama ikampiga chini.

 
Naona
Hii ilikuwa ni baada ya Nyerere kuondoka na Waryoba hakukaa muda kabla ya Msuya kuchukua usukani kama waziri mkuu.
Naona unachanganya mafaili sasa.

Enzi za utawala Mzee Mwinyi kulikuwa na Mawazili wakuu Watatu tu alianza Joseph Warioba(1985-1991), John Malechela(1991-1993) na Mzee Msuya(1993-1995).

Pia Manaibu waziri wakuu katika uongozi wa Mzee Mwinyi tulikuwa nao wawili tu ambao ni Salimu ambaye alikuwa Waziri wa ulinzi na Naibu waziri Mkuu(1986 Hadi 1989) pia na Mzee Mrema.

Lakini unapaswa ukumbuke Kabla ya uchaguzi wa Tanzania wa mwaka 1990 Salim A.Salim alikuwa Ethiopia teyari kama Katibu mkuu wa OAU na kuwaachia licheo lisilo na maana la kisiasa.
 
Naona
Naona unachanganya mafaili sasa.

Enzi za utawala Mzee Mwinyi kulikuwa na Mawazili wakuu Watatu tu alianza Joseph Warioba(1985-1991), John Malechela(1991-1993) na Mzee Msuya(1993-1995).

Pia Manaibu waziri wakuu katika uongozi wa Mzee Mwinyi tulikuwa nao wawili tu ambao ni Salimu ambaye alikuwa Waziri wa ulinzi na Naibu waziri Mkuu(1986 Hadi 1989) pia na Mzee Mrema.

Lakini unapaswa ukumbuke Kabla ya uchaguzi wa Tanzania wa mwaka 1990 Salim A.Salim alikuwa Ethiopia teyari kama Katibu mkuu wa OAU na kuwaachia licheo lisilo na maana la kisiasa.
Ni kweli.
 
Ila na elimu yake ukisikiliza vizuri ina connection na chenga nyingi sana😂

Bahati ni bahati... 😂
huyo Hana connection yoyote , Iko straight forward , kutoka o level , butimba tcc, certificate hapo hapo , akaenda china kupiga certificate, akarudi morogoro tc akapiga diploma , akarudi sauti kapiga degree na masters , SHIDA ipo wapi ? Kila kitu kipo wazi
 
Huyu jamaa ni mmoja ya watu wachche nchini wanaofaidi vilivho keki ya Taifa. Kwa mwezi sijui ana mishahara mingapi! Maana ana mshahara wa ubunge, uwaziri, unaibu Waziri mkuu! Kama huko kote hapati mishahara, basi posho nono hazikosekani.
Acha kabisa
 
Back
Top Bottom