Kama cheo hakipo kikatiba Ila bado kinaundwa kwa hoja kuwa 'Rais ana madaraka ya kufanya hivyo kwa katiba hiyo hiyo isiyokitambua hicho cheo' hilo ni tatizo kubwa mno.
Jibu lako ni lina sehemu mbili '' YES and NO'
Yes kwasababu Katiba haikutaja cheo cha Naibu Waziri Mkuu.
No kwasababu Katiba haikuzuia kuanzishwa kwa cheo hicho kama ilivyotoa haki ya kugawa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuwa Wizara Mbili. Katiba isiyomtaja Naibu Waziri Mkuu imempa Rais madaraka ya kuunda Wizara kwa kadri anavyoona inafaa.
Kuna 'conventional wisdom' kwamba kitu ambacho hakikutazwa kisheria basi kimeruhusiwa kisheria.
Naibu PM haingi baraza la mawaziri Ila bado itabidi awepo kwa kuwa ni waziri wa nishati...maajabu haya
Hapa ni suala la ufundi. Rais alijua kwamba Naibu Waziri Mkuu kama Manaibu wengine na kwa kuwa hana nafasi kikatiba hataweza kuingia Baraza la Mawaziri. Rais anafahamu ili awe ''effective' Naibu Waziri Mkuu ni lazima ahudhurie vikao ambavyo yeye ana hadhi kuliko Mawaziri. Njia aliyotumia ni kumpa uwaziri wa Nishati ili aweze kuingia katika Baraza la Mawaziri
.
Again, hakuna sheria aliyovunja kwasababu kilichompa nafasi ya kuunda Baraza la Mawaziri kwa kadri anavyoweza hakikumzuia kumpa mtu Naibu na Waziri Kamili at the same time ili atumie mwanya huo kuingia katika Cabinet.
Hali za 'ujanja ujanja' ni utamaduni wa Serikali za CCM, lakini si unique. Ikiwa tutamlaumu Rais tutakuwa hatumtendei haki kwasababu kuna mauza uza mengi katika jamii tunaishi nayo.
Mfano, polisi kumkamata mtu Ijumaa ili alale hadi Jumatatu ni mkomoeni lakini hawajavunja sheria kwasababu hatuna mahakama za wikiendi. Polisi hao hao watampeleka mtu kwa ofisi ya DCI halafu wanamrudisha Magereza kwa siku nyingine kwasababu saa 24 zinaanzia pale alipotoka kwa DCI
Ni mauza uza kama yale ya Wakurugenzi kufunga ofisi na kutoweka kabla ya muda wa kurudisha Form
So kuna mengi hili la Naibu Waziri Mkuu ni sehemu tu ya mauza uza
Katiba hii ya mwaka 1977 haiendani kabisa na wakati tulionao huo ndio ukweli.
Siyo kwamba haiendani ni kwamba haifai hata kwa bahati mbaya. Ukiisoma utabaki na maumivu ni afadhali usi isome kabisa. Mfano, Katiba hii haimzuii Rais kuwa na Baraza la Mawaziri 50 akitaka. Katina hii inamtambua Rais kama Amir Jeshi Mkuu lakini akiwa Zanzibar ni Amir Jeshi Mkuu Mwenza. n.k.
Katiba ya 1977 inatambua uwepo wa Wabunge na muda wa kutumikia. Katiba hiyo hiyo haielezi lini Mbunge anapaswa kupewa kiinua mgongo. Wapo watakaosema kuna sheria zinazohusu hili, lakini pia katiba ina sehemu imetaja masilahi ya Wafanyakazi fulani. Kwahiyo Katiba haikuweka ukomo wa Ubunge , kinachotokea kila miaka 5 wanazoa kiinua mgongo, akirudi tena kiinua mgongo akirudi tena kiinua mgongo.
Tunahitaji Katiba mpya sasa . Kenya katiba yao ina ukomo wa Idadi ya Baraza la Mawaziri na Watendaji.
Ruto alijaribu kuweka makatibu, Mahakama ikampiga chini.