Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria

Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria

Huu ndio ukweli hata kama Mtapinga ila huyo PM wenu haaminiki na Mamlaka.Hapa mama amekwepa tuu kumfuta kazi ambapo ingepelekea Baraza zima la Mawaziri Kuvunjika na Serikali kuanza Upya.

Saizi bila shaka amepunguziwa majukumu Ili amulikwe vizuri.

Naunga mkono haya Mabadiliko Yako vizuri kasoro Kwa Pindi Chana na pia nilipendelea Byabato awe full Minister wa Nishati.
 
Rais mstaafu wa awamu ya nne alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje. Akawa mwanadiplomasia mahiri sana. Pia kuwepo kwake kwenye wizara hiyo kulimuepusha na vurugu za siasa za ndani. Akaja kuwa Rais baadae.

Bernard Membe almanusura angekuwa Rais mara baada ya kuhudumu kwa muda mrefu Wizara ya Mambo ya Nje. Akakshindwa na John Magufuli mwaka 2015.

Na sasa January Makamba amepelekwa Wizara ya Mambo ya Nje. Je ndio maandalizi ya kumpika kama Rais ajaye?
 
Ndio kilichobaki anachokiweza huyu Bibi.

Mtu anapo- underperform anahamishwa instead ya kuwekwa pembeni.

Huyo Bibi Tax naye karudishwa wizara aliyotolewa hata mwaka haujaisha.

Hicho cheo alichopewa huyo Biteko kina tija gani maana hakipo kikatiba na hata Mrema aliyewahi kukishika hakuna aliyepewa tena ikiwa ni tafsiri hakina manufaa

I only see the last kicks of a dying horse.
 
Hivi kwa nchi zetu hizi za Afrika ambazo zina lundo la nafasi za uongozi na bado ni masikini ambapo wengine wanasema umasikini wetu umesababishwa na laana, wengine ni utamaduni wa kutopenda kazi na mifumo mibovu ya kubana mafisadina kuleta uwajibikaji;

Kuna ulazima gani kuwa na nafasi ya Naibu Waziri Mkuu?
 
Back
Top Bottom