Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria

Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria

Biteko
Yani naibu waziri mkuu at the same time ni waziri wa nishati..
Lakini kwenye unaibu waziri mkuu atashughulikia mambo ya uratibu wa serikali...
Kichwa lazima kikuzunguke[emoji3]
Naungana na jamaa mmoja hapa Jf alissema ukifuatilia siasa za Tanzania alafu ukawa comfortable bila ya stress basi jehanamu haitakuwa ngumu kuishi huko .
 
Angelina Mabula, nilikuwa najiuliza hivi huyo mama yetu kuruhusu hii wizara ya ardhi itumie mabilioni yote hayo kwa semina tuu badala ya kupima ardhi anaona ni sawa hasikii kichefuchefu.
 
Rais Samia Suluhu amefanya mabadiliko na teuzi za sura mpya kwenye baraza la mawaziri. Uapisho utafanyika September 1, Ikulu ndogo Zanzibar saa tano kamili asubuhi.
1. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Doto Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Awali alikuwa Waziri wa Madini.

2. Amemteua January Makamba kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Awali alikuwa Waziri wa Nishati.

3. Amemhamisha Balozi Pindi Chana kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Awali alikuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.

4. Amemhamisha Steven Byabato kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Awali, Byabato alikuwa Naibu Waziri wa Nishati.

5. Amemteua Jerry Silaa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Silaa ni Mbunge wa Ukonga, Dar es Salaam.

6. Rais amemteua Anthony Mavunde kuwa waziri wa madini, mwanzo alikuwa naibu waziri wa kilimo.

7. Prof Makame Mbarawa aliyekuwa waziri wa ujenzi na uchukuzi amekuwa waziri wa uchukuzi.

8. Innocent Bashungwa amekuwa waziri wa ujenzi, mwanzo alikuwa waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa.

9. Godfrey Kasekenya aliyekuwa Naibu waziri wa Ujenzi na uchukuzi ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa Ujenzi

10. Alexander Mnyeti ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa Kilimo

11. David Mwakiposa Kihenzile ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa Uchukuzi. Ni mbunge wa Jimbo la Mufindi

12. Judith Kapinga ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa nishati, ni mbunge wa viti maalum Ruvuma.

13. Dunstan Kitandula ameteuliwa Naibu Waziri wa maliasili na Utalii, ni mbunge wa Mkinga

14. Stergomena Tax amehamishwa wizara ya mambo ya Nje kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

15. Angellah Kairuki amehamishwa kutoka TAMISEMI na kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii

16. Dkt. Damas Ndumbaro amehamishwa kutoka Wizara ya Katiba ba Sheria na kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.




View: https://www.youtube.com/watch?v=7bLEuvgVGG4

======

View attachment 2733279
View attachment 2733280
View attachment 2733281
View attachment 2733282

Hivi hii Serikali ina Wizara ngapi.....!?
 
Kassimu majaliwa unapewa ujumbe hapa. Je unapwaya au hawakutaki? kwanini umepewa msaidizi Tena kinyume cha katiba?
Lakini uteuzi huu wa naibu waziri mkuu na huyo mnyeti ni danganya toto kwa wasukuma ambao wameoneka kuwa na mwitikio mkubwa katika oparesheni za Chadema na ni dhahiri hawataki kusikia kuhusu sa100.
Mimi napata shida kuelewa ufikiri wa viongozi wetu. Kuna vyeo vingine ukivitazama huoni maana yake, ni kupoteza pesa za walipa kodi tu.

Waziri Mkuu ofisi yake ina Waziri mwingine wanaita sijui Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu. Ana wasaidizi chungu mzima, sasa sijui tatizo ni nini au ni kupenyezana ili kupeana ulaji. Au ni danganya toto kwa watu wa eneo fulani.
 
Back
Top Bottom