Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria

Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria

Kipindi kile tulikuwepo mkuu. Salim Alikuwa waziri Mkuu kwenye utawala wa Nyerere kwa mwaka mmoja tu tena baada ya Sokoine kututoka lkn baada ya Mzee Mwinyi kuingia Madarakani Salim alirudishwa kama Naibu waziri Mkuu[1986-1989] na waziri wa ulinzi huku Waziri Mkuu kipindi hicho akiwa Joseph Warioba.
Hii ilikuwa ni baada ya Nyerere kuondoka na Waryoba hakukaa muda kabla ya Msuya kuchukua usukani kama waziri mkuu.
 
Naona hujaielewa dhanna ya Reform and Rebuilding.

Hapo kwa Kassim Majaliwa, kilichositisha asipigwe chini ni mfumo tu, lakini ana "underperform" sana, juzi aliambiwa, usingoje maagizo kutoka juu.
Hovyoo..
 
Nakumbuka wakati Dr Augustine Lyatonga Mrema alipokuwa Naibu Waziri mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani

Alikuwa anacheza Wizara zote sijajua Dr Biteko atatumia style ipi

Ngoja tuone!

Mlale Unono 😀
 
Rais anao uwanda mpana wa kubadili wizara na kuwaweka Mawaziri kwa kadri atakavyo.

Kwa uzoefu wangu sikuwahi kusikia Kiongozi aliyewahi kuwa Naibu Waziri mkuu.

Hata hivyo kama Rais ana Makamu wake iweje Waziri mkuu asiwe na Naibu?

Nilipochanganyikiwa zaidi ni Kiongozi mmoja kuwa Naibu Waziri na Waziri ktk serikali hiyohiyo. Inawezekanaje?

Kwamba Pale bungeni na huko mitaani hakuna wanachama wa CCM wenye weledi kiasi cha kumtwisha majukumu mazito ndugu Dotto?

Tuombe Mungu uteuzi huu uwe na malengo ya kuimarisha ustawi wa wananchi wote na si kumdhoofisha mtu flani kwa manufaa ya watu wachache.
Mrema alikuwa naibu WM enzi za mwinyi. Uteuzi wa mrema ulitokana na utendaji wake wakati akiwa waziri wa mambo ya ndani.
Ila huu uteuzi wa Biteko una walakini nahisi majaliwa ni tishio 2025.
 
Biteko
Yani naibu waziri mkuu at the same time ni waziri wa nishati..
Lakini kwenye unaibu waziri mkuu atashughulikia mambo ya uratibu wa serikali...
Kichwa lazima kikuzunguke😀
Hahahahah🤣🤣
 
Kwa panga pangua hii ya mawazkri watoto wetu wa shule ya msingi wanapata tabu sana kwenye somo la uraia
 
Rais Samia Suluhu amefanya mabadiliko na teuzi za sura mpya kwenye baraza la mawaziri. Uapisho utafanyika September 1, Ikulu ndogo Zanzibar saa tano kamili asubuhi...
1693414345016.png

AND Maryam Salim - Planning Commissioner - Ms. Maryam Salim is the Country Manager of the World Bank for Cambodia. Ms. Salim has more than 20 years of experience in the World Bank, during which she has led a number of Program and Policy reform initiatives.

Prior to this position, Ms. Salim was Country Manager of the World Bank for Albania, and she held various other positions, including Advisor in the Office of the Chief Executive Officer and Senior Vice President for Operations. She worked also as Operations Advisor and Program Leader for Investment Project Financing. Ms. Salim joined the Bank as a Young Professional in 1998 and has worked in health and social protection programs in the Africa, Europe and Central Asia, and East Asia and Pacific Regions.

A Tanzanian national, she holds a Master's in International Economics and International Relations from the Johns Hopkins University's Paul H. Nitze School of Advanced Studies and a Juris Doctor from Georgetown University.
 
Ali Hassan Mwinyi enzi zake aliwahi kumteua marehemu Augustine Mrema kwenye nafasi kama hiyo!!
Mrema mpka amekufa anafuatilia mafao yake bila mafanikio Kwasababu ya cheo chake hakitambuliwi
 
Hali kadhalika amemteua Lucas Mwashambwa Waziri wa Kujipendekeza na Mapambio Mitandaoni
Huyo mnafiq hawezi kuteuliwa hata ubalozi wa nyumba kumi. Ana ID za kuwapiga spana magamba na I'd ya kutafutia ugali ambayo anaweka namba ya simu
 
Duh! Mbona Mzee Mrema sasa waligoma kumlipa mafao yake ya unaibu waziri mkuu ?....
Analipwa kwa kutumia kigezo gani?
Kikatiba nafasi hiyo haipo. Naibu Waziri Mkuu haingii katika Baraza la Mawaziri.

Sijui wanagawana vipi mapesa kwa jina la mafao lakini najua kuna kitu kinaitwa 'presidential appointees'
Hawa wana mafungu wanayolipwa ! Tunahitaji Katiba kuweka mambo sawa

Fikria kwamba Mbunge analipwa kiinua mgongo kila baada ya miaka 5. Akikaa Bungeni miaka 10 ,15 au 20 analipwa kila baada ya miaka 5. Hivi kazi gani nyingine tena unayoweza kupata ladha na utamu kama huo.
Ukiwaona wapo kimya Dodoma si kwasababu wana nidhamu ni kwasababu asali imewakolea wanahofia kupaliwa.

Tunahitaji Katiba ili kuweka mambo sawa. Kwanini Mbunge akopeshwe V8 na sehemu ya Mkopo walipe Wananchi tena kila baada ya miaka 5. Tuna tatizo kubwa sana , tunahitaji Katiba

JokaKuu
 
Back
Top Bottom