The United Republic of Tanzania imeundwa na pande mbili kwa gharama ya upande mmoja kuji dissolve huku upande mwingine ukibaki. Tanganyika ilijigeuza mshumaa, ilijiangamiza kwa lengo la kuangazia wengine.
Hivyo, Muungano huu unampa Zanzibar kuwa access ya nafasi zote, maana Tanganyika ilishajiua hivyo kukabidhi kila kitu kwa Zanzibar, maana katika Muungano huu Zanzibar ndiye pekee aliye hai.
So, unapoongelea maliasili, taasisi, n.k Zanzibar ana mamlaka nazo zote, kama mmiliki upande mmoja, huku upande mwingine akiwa kama msimamizi maana Tanganyika ilipojiua iliacha watoto na wakebkadhaa ambao wote walendelea kulelewa na Zanzibar. Hapo ndipo hesabu za nyerere zilipopotea .
Laiti Tanganyika ingekuwepo au ingefufuka leo, basi hapo itakua sawa kusema kuna vitu vya Muungano. Ila kwa sasa, Zanzubar ndiye anayetambuliwa ni vile tu hawaijui nguvu yao.
Sasa hivi Zanzibar wana nguvu ya kuamua lolote ndani ya Muungano na watoto na wake watanganyika wakatakiwa kupokea tu maelekezo.
Kwa kuwa Tanganyika ilishakufa, sasa hivi serikali ya Muungano inabaki kuwa chombo kinachomsikiliza zaidi Zanzibar kabla ya kufanya maamuzi yoyote yale. Maana ndiye pekee aliye hai.