Mabadiliko ya kweli yana gharama kubwa, yanahitaji mtu jasiri na mzalendo kweli kweli

Watanzania siyo watoto wa masikini.
Tumeambiwa "Nchi yetu ni tajiri"
Lakini pia umasikini hauhalalishi udikteta au ukoloni karne hii.

Sent from my XT1097 using JamiiForums mobile app
Rasilimali bila kusimamiwa vizuri haziwezi kuleta tija yoyote ( in abundance of water a fool is thirsty).

Utajiri wa rasilimali ni jambo moja na matumizi stahiki ya rasilimali hizo ili ziweze kuinua maisha ya wananchi ni jambo lingine.

Rais Magufuli amelisimamia hili vizuri na rasilimali zetu sasa zinatumika ipasavyo kutusaidia Watanzania. Mfano mzuri upo kwenye madini. Matokeo yameonekana haraka Sana, uchumi wa kati tushaingia. Unaachaje kwa mfano kumpa kura kiongozi wa mtindo huo?

#2020 kura kwa John
 
Mjomba siku zote iko hivi.ukiona kitu kinapambwa sana jiulize kulikoni.
Kamwe, narudia tena kamwe hatuwezi kuacha uongo utamalaki eti kwasababu ukweli utaonekana tuu. Hili sisi wazalendo wa kweli hatuwezi kuliacha lipite tuu. Ukweli utasemwa daima na fitina kwetu ni mwiko, daima tutaipinga.
 
W Wewe kumbe ni Lissu! Maana number zinakupita pembeni! Mabwawa ya umeme ya Mtera +....... Unayalinganisha na hili linalojengwa! Reli ya Tazara unailinganisha na SGR? Ndege pia? Hata muda wa mambo haya yalivyo tendeka unaulinganisha na muda wa viongozi waliopita! Mbona kasi ya utekelezaji wa maendeleo wa Magufuli ni zaidi? Nayo huioni? Lissu hapo unachemsha! Vua hiyo miwani na ujifunze hesabu maana kwa fani yako hesabu ni kikwazo!
 
Kamwe, narudia tena kamwe hatuwezi kuacha uongo utamalaki eti kwasababu ukweli utaonekana tuu. Hili sisi wazalendo wa kweli hatuwezi kuliacha lipite tuu. Ukweli utasemwa daima na fitina kwetu ni mwiko, daima tutaipinga
Kama unaamini katika ukweli basi nikukumbushe kuwa siku zote ukweli ni mfupi na uongo ni mrefu.Na ukweli unatabia yakujisimamia nakujidhihirisha wenyewe sio hadi uulazimishe au uuseme kwakuupamba.Unachokifanya wewe na wengine mnaounga mkono juhudi ni kutaka kuufundisha ukweli namna yakujiendesha kitu ambacho hakipo. Na wewe sio mzalendo ni mfuasi tu aidha wa mtu au chama cha siasa kimoja wapo.mzalendo wa kweli lazima ajue kanuni Ya Ukweli.
 
Kama ni hivyo tusingehitaji kujitetea mahakamani na kwingineko tunapoonewa
 
Jitu linaroho mbaya linakataa kuongeza mishahara miaka mitano utafikiri anatoa hela za mfukoni mwake au za baba yake au mama yake ,lakini njiani ni kumwaga hela kwa maigizo yasiyokuwa na kichwa Wala miguu.
 
Jitu linaroho mbaya linakataa kuongeza mishahara miaka mitano utafikiri anatoa hela za mfukoni mwake au za baba yake au mama yake ,lakini njiani ni kumwaga hela kwa maigizo yasiyokuwa na kichwa Wala miguu.
Kauli hizo ni kauli za kifisadi. Ndio mnavyosema, eti pesa hizi sio za baba yako au mama yako.

Halafu utendee haki ubongo wako. Hizo hela unazosema anamwaga ni Kiasi gani kulinganisha na mishahara? Pia kila kiongozi ana staili yake
 
Familia ya chini anawaza kujenga?
Hawali nyama mpaka sikukuu
Kila siku wanatafuta kula, kuvaa, hospitali na madaftar
 
Amani Msumari,

Hii ndo thinking ya masikini aka mnyonge, wengine wanajibana kuongeza uzalishaji (productivity) ,masikini anajibana kuwekeza kwenye dead investments. Now I understand why Americans hupenda kuongozwa na watu wenye fedha zao
 
Magufuli alimtumbua Profesa Assad baada ya report ya Profesa kuonesha mapungufu ya kifedha kwenye serikali ya Magufuli.

Point clear, black n white
Mwanga na giza haiwezekani kukaa kwenye chumba kimoja, Magu ni mwizi,mwongo na mnafiki asingeweza kufanya kazi na Prof Assad
 
Amefanya makubwa katika kipindi cha miaka mitano hii
Yes ameongeza USD 100.00 tu kwenye GNI,amekopa 40T sawa na budget ya nchi ya miaka miwili na sawa na makusanyo ya Kodi ya miaka mitatu na nusu.Amevuruga market systems za mazao ya korosho, kahawa,tumbaku,mbaazi etc.Amejenga barabara ya kilometer 17 Kimara- Kibaha for five years na haijaisha,kweli kapiga kazi
 
Kwa hio miaka 5 haijamtosha kuijenga nchi Bas apigwe chini waingie visionary leaders
 
Amani Msumari,

Hii ndo thinking ya masikini aka mnyonge, wengine wanajibana kuongeza uzalishaji (productivity) ,masikini anajibana kuwekeza kwenye dead investments. Now I understand why Americans hupenda kuongea na watu wenye fedha zao
Sijijui

Sikia, aki tena utajijua. Nenda kasome uzi wangu wenye kichwa cha habari "je ni kweli flyovers na ndege zetu hazina msaada wowote kwa mwananchi anayeishi Nanyamba au Kyabakari?

#2020 kura yangu kwa John
 
Kwa hio miaka 5 haijamtosha kuijenga nchi Bas apigwe chini waingie visionary leaders
Soma uzi wabgu "je ni kweli flyovers na ndege zetu hazina msaada wowote kwa mwananchi anayeishi Nanyamba au Kyabakari?
 
Kwahayo uliyoandika wewe huishi Tanzania
 
Mwanga na giza haiwezekani kukaa kwenye chumba kimoja, Magu ni mwizi,mwongo na mnafiki asingeweza kufanya kazi na Prof Assad
Kuwa na adabu inayostahili unapomuongelea kiongozi wa nchi. Inashangaza kuona huu ndio Uhuru wa habari mnaoutaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…