Mabadiliko ya mwonekano JamiiForums - Juni 2022

Nataka kuona post, Niki click Recent thread zinaonekana za mwanzo za mbele sio, anajua
 
Inakosesha ata raha yani... Mods na Bwana Melo bring back our JF!

Na kingine sisi ndo walaji na nadhani mmeshapata maoni, wengi wetu atujapenda maboresho yenu ya kipindi hiki!
 
Katika eneo ambalo halikuhitaji mabadiriko , ni kuihamisha general forum na kuiweka pembeni badala yake trending ndo inakuwa ya Kwanza , na pia kubadili font na kuyakuza maneno Yani kama vitabu vya darasa la pili kuandika ...boring Sana aisee
 
Ongezeni jukwaa la hoja mijadala ya kidini.
Hapa ni mambo yote kuhusu dini Ukristo, Uislamu, Uchawi, Rastafarian, nk.
 
Wamechemka sana... Inakosesha ata raha yani... Mods na Bwana Melo bring back our JF!

Na kingine sisi ndo walaji na nadhani mmeshapata maoni, wengi wetu atujapenda maboresho yenu ya kipindi hiki!
Mbona forum zipo
 
mi naomba Jf iende ifike mahala tuwe na option ya kuwa portal zetu wenyewe kama ilivyo Facebook na zinginezo... where we can login using genuine userID's.
 
where we can login using genuine userID's.
Halafu jukwaa la siasa liwe hatariii🙄
Ukitoa maoni flani, kutekwa nje nje!!!

Ila hata saivi ukiamua kutumia majina yako halisi humu inawezekana tu. Kuna wanaofanya Hivyo.

Hata huko Fb, Twitter... siyo kila mtu anatumia real name
 
app ya zamani nilikua siwezi kuplay media moja kwa moja kwenye app mpaka ni download sjui kama sasa mmelirekebisha hilo
 
Halafu jukwaa la siasa liwe hatariii🙄
Ukitoa maoni flani, kutekwa nje nje!!!

Ila hata saivi ukiamua kutumia majina yako halisi humu inawezekana tu. Kuna wanaofanya Hivyo.

Hata huko Fb, Twitter... siyo kila mtu anatumia real name
Tusiogope..mambo yamebadilika si kama wakati ule wajinga wajinga wanaua watu werevu.
 
Is it possible to have different italic options from this new current one?
 
Mods najua mmeshika mpini na sisi tumeshika makali lakini hamjatutendea haki kwa kuondoa Uzi wa kupigia kura muonekano mpya wa jamii forum niliouanzisha jana saa 7:20pm

niwe muwazi sijawahi soma vigezo & masharti vya JF lakini sizani kama kuna sheria nimeivunja kwa kuuweka huo uzi hapo jukwaani

kwa hisia zangu nahisi Uzi umeondolewa kwa sababu ya kuonekana kura nyingi zilikuwa zikionesha kutokufurahishwa na mwonekano mpya wa Jamii Forum

please Maxence Melo naomba angalia namna ya kuurudisha huo uzi au anzisheni nyie uzi mwingine wa kupigia kura mabadiliko ya mwonekano wa JF
 
Yan JF hata mimi kwasasa inanipa uzito sana na siifurahii kabisaaaa kila napopata wazo la kuingia..Yana it is BORING yan ni kama wameamua kuendana na features za kwenye Linked in na Quora..VERY VERY VERY BORING INDEED
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…